Kwako waziri wa TAMISEMI, angalieni na namna ya kuwachuja wanaoomba kazi za ualimu walau hata kwa "Online aptitude test"

Ni wazo zuri hila ni la ghali sanaaa japo ni kizuri ni ghalama lakini fikili cc wengine wa nanjilinji uku kupiga cm tu lazima upande gari uende tafuta mtandao mahala je hyo Online Aptitude Test Itakuwaje? Hapo sasa serikali kwanza itaanza na poject za kuboresha huduma za kimawasiliano kwanza nchi nzima ni ghalama zaidi ya hata wanavyofanya utumishi kukusanya watu dodoma
 
Huez mjaji mtu ubora wake kwa mtian wa siku moja kwa vitu vya miaka tano nne na tatu alotumia kusoma, Hii si njia bora kwann usiseme watumie GPA?
 
Jambo limgine chuo ndio chenye dhamana ya kutambua ubora ndio mana alifaulu na kupewa cheti cha taaluma husika manaake anafaa kufanya kazi husika
 
Yaani vigezo vya kuomba kazi viongezwe salary ile ile

Maboresho haya yaanzie kwenye mshahara na mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji

Ukiweza hilo ongeza vigezo hata kwenye harusi tunazochangia tumeomba wapunguze maia na marembo mengi waongeze nyama watu wanachangia ety
Hahaha
 
Huez mjaji mtu ubora wake kwa mtian wa siku moja kwa vitu vya miaka tano nne na tatu alotumia kusoma, Hii si njia bora kwann usiseme watumie GPA?
Sitaki kuzungumzia kabisa GPA lakini niseme kwamba wenye GPA za kawaida ndio wenye uwezo mzuri zaidi kuliko wenye kubwa kwa sababu wenye GPA kubwa wengi wametumia mbinumbinu kuzipata.

Nawakubali sana wazungu, kwenye Mashirika yao wakitafuta mtu GPA sio hata kigezo ila utapimwa kwa skills na competencies zako.

Umesema huwezi kumjaji mtu kwa mtihani wa siku moja, vipi huko ulipopita haikutumika mitihani tena isiyongua masaa 2 kukugredi? Kwa nini kwenye mchakato huu kisiwepo kigezo bora Cha mchujo badala ya upendeleo na kujuana kutapoweza kufanyika?
 
Jambo limgine chuo ndio chenye dhamana ya kutambua ubora ndio mana alifaulu na kupewa cheti cha taaluma husika manaake anafaa kufanya kazi husika
Ingekuwa ni hivyo basi kusingekuwa na haja ya interview kufanyika na badala yake watu waombe HR meneja ajichagulie anayetaka maisha yasonge mbele.

Tusikubali tu kwamba Jambo I zuri kwa sababu una maslahi nalo ,angalia kwa picha kubwa zaidi. Ebu fikiria, una GPA nzuri sana Tena sana na uzoefu wa kutosha ,umeomba kazi vigezo vyote vya kuitwa kwenye usaili unavyo tena na zaidi lakini mchakato wa usaili haukuwepo na ukaja kusikia nafasi ilipata mtu na mbaya zaidi unaambiwa jina lililetwa mezani moja tu. Nataka utumie picha hii kuangalia kusudi la mada hii, Je utajisikiaje?
 
Mhe.Rais wa JMT,
Mhe.Waziri wa TAMISEMI

Nawapongeza kwa jitihada zenu katika kutengeneza na kutoa fursa za ajira nyingi sana katika kada ya ualimu na Afya. Ni ishara njema katika kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mhe. Waziri wa TAMISEMI, maoni na mapendekezo haya ni kwa ajili ya ofisi yako ikiwa kama ofisi inayoratibu mchakato wa ajira za ualimu na Afya zilizotangazwa hivi karibuni. Maoni yangu yatasimamia katika mchakato wa kuomba mpaka kupangiwa vituo.

Ni ukweli usiopingika ,usaili au mtihani ni moja ya njia nzuri ya kupata watu walio bora na usaili ni moja ya mchakato muhimu katika ajira.

Hali imekuwa tofauti kwa ajira za TAMISEMI, labda pengine kutokana na wingi wa wanaoomba au kuwapunguzia gharama waombaji ,usaili au mitihani huwa sioni ikifanyika. Je, mna uhakika gani mliyepatia ajira ni bora kuliko mliyemuacha?

Utaratibu huu wa kuchuja na Kuwapatia ajira bila kuwepo usaili au mitihani lazima utaingiwa na dosari za upendeleo na kupatikana kwa watu wasio na sifa na wenye sifa kuachwa.

Ni vema utaratibu ukabadilishwa ili kutoa fursa sawa kwa waombaji na uangaliwe utaratibu wa kuwafanyia walau "ONLINE APTITUDE TEST" waombaji utazamwe. Kila muombaji ashiriki kwenye test kwa walau hata ya somo moja la atakalofundisha.

Pia katika utaratibu huu wa ONLINE APTITUDE TEST sio lazima waombaji labda walioomba kufundisha' biology' wafanye test ya aina moja, ili kuepusha kupeana majibu au udanganyifu wanaweza kupewa test tofauti au kama ni test ya aina moja mpangilo wa maswali ubadilishwe baina ya waombaji.

Tutumie walau njia hii kuondoa upendeleo wa aina yoyote au lawama kwamba nilikosa huku nikiwa Nina sifa.

Matumaini maoni haya yatakuwa ni msaada katika upatikanaji wa watumishi bora na sahihi.

Ahsante.
Usichotaka kukikubali ni kuwa mtu aliyehitimu chuoni ana uwezo wa kufanya kazi katika fani yake!! Mtihani wa ziada ni kuongeza tu gharama isiyokuwa ya lazima!! Na usumbufu usiokuwa wa lazima!! Hongera Tamisemi kwa kuliona hilo!! Miaka yote waalimu na madaktari hawafanyiwi usaili!! Walishahitimu vyuoni na wameitioa viindi vya mafunzo kwa vitendo!!
 
Sitaki kuzungumzia kabisa GPA lakini niseme kwamba wenye GPA za kawaida ndio wenye uwezo mzuri zaidi kuliko wenye kubwa kwa sababu wenye GPA kubwa wengi wametumia mbinumbinu kuzipata.

Nawakubali sana wazungu, kwenye Mashirika yao wakitafuta mtu GPA sio hata kigezo ila utapimwa kwa skills na competencies zako.

Umesema huwezi kumjaji mtu kwa mtihani wa siku moja, vipi huko ulipopita haikutumika mitihani tena isiyongua masaa 2 kukugredi? Kwa nini kwenye mchakato huu kisiwepo kigezo bora Cha mchujo badala ya upendeleo na kujuana kutapoweza kufanyika?
Hakuna uendeleo!! Kigezo kinachotumika ni: Aliyehitimu mwanzo apatiwe ajira mwanzo!! Waliohitimu pamoja apatiwe ajira kwanza mwenye umri mkubwa!! Hii imekaa vizuri!!
 
Huez mjaji mtu ubora wake kwa mtian wa siku moja kwa vitu vya miaka tano nne na tatu alotumia kusoma, Hii si njia bora kwann usiseme watumie GPA?
GPA za kuchonga ni nyingi sana!! Utaratibu wa sasa ni wa haki. Aliyehitimu mwanzo kwa masomo yanayofanana anapatiwa ajira kwanza!! Waliohitimu pamoja mwenye umri mkubwa anapatiwa ajira kwanza!! Wakigombea nafasi moja waliohitimu amoja na wanalingana miaka hapo ndipo GPA inaamua!! Hii imekaa vizuri sana. Hii ni foleni!
 
Ni wazo zuri hila ni la ghali sanaaa japo ni kizuri ni ghalama lakini fikili cc wengine wa nanjilinji uku kupiga cm tu lazima upande gari uende tafuta mtandao mahala je hyo Online Aptitude Test Itakuwaje? Hapo sasa serikali kwanza itaanza na poject za kuboresha huduma za kimawasiliano kwanza nchi nzima ni ghalama zaidi ya hata wanavyofanya utumishi kukusanya watu dodoma
Ukute na wewe umeomba hizi ajira
 
Nitumie uzi kuipongeza Serikali kuonesha kujali na kuwa wasikivu kwa maoni yatolewayo. Kupitia Rasimu ya muswada wa Elimu suala la usaili kwa walimu limeangaliwa kwa jicho la kipekee kabisa.

Nikiwa kama mtanzania, nafarajika kusikia na kuona habari hizi njema kabisa na ni matumaini yangu mpango huu utazalisha walimu walio competent na wenye uwezo na kadiri Mungu atakavyotujalia tutaona matokeo na matunda yake.

Ahsante
 
Jamaa ulikuwa na wazo zuri sana ,we ni futurist ombi lako naona sa hivi limefanyiwa kazi Kuna watu wenye IQ ndogo walikuwa Wana Pinga ushauri wako
 
Mhe.Rais wa JMT,
Mhe.Waziri wa TAMISEMI

Nawapongeza kwa jitihada zenu katika kutengeneza na kutoa fursa za ajira nyingi sana katika kada ya ualimu na Afya. Ni ishara njema katika kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mhe. Waziri wa TAMISEMI, maoni na mapendekezo haya ni kwa ajili ya ofisi yako ikiwa kama ofisi inayoratibu mchakato wa ajira za ualimu na Afya zilizotangazwa hivi karibuni. Maoni yangu yatasimamia katika mchakato wa kuomba mpaka kupangiwa vituo.

Ni ukweli usiopingika ,usaili au mtihani ni moja ya njia nzuri ya kupata watu walio bora na usaili ni moja ya mchakato muhimu katika ajira.

Hali imekuwa tofauti kwa ajira za TAMISEMI, labda pengine kutokana na wingi wa wanaoomba au kuwapunguzia gharama waombaji ,usaili au mitihani huwa sioni ikifanyika. Je, mna uhakika gani mliyepatia ajira ni bora kuliko mliyemuacha?

Utaratibu huu wa kuchuja na Kuwapatia ajira bila kuwepo usaili au mitihani lazima utaingiwa na dosari za upendeleo na kupatikana kwa watu wasio na sifa na wenye sifa kuachwa.

Ni vema utaratibu ukabadilishwa ili kutoa fursa sawa kwa waombaji na uangaliwe utaratibu wa kuwafanyia walau "ONLINE APTITUDE TEST" waombaji utazamwe. Kila muombaji ashiriki kwenye test kwa walau hata ya somo moja la atakalofundisha.

Pia katika utaratibu huu wa ONLINE APTITUDE TEST sio lazima waombaji labda walioomba kufundisha' biology' wafanye test ya aina moja, ili kuepusha kupeana majibu au udanganyifu wanaweza kupewa test tofauti au kama ni test ya aina moja mpangilo wa maswali ubadilishwe baina ya waombaji.

Tutumie walau njia hii kuondoa upendeleo wa aina yoyote au lawama kwamba nilikosa huku nikiwa Nina sifa.

Matumaini maoni haya yatakuwa ni msaada katika upatikanaji wa watumishi bora na sahihi.

Ahsante.
Dua lako limejibiwa
 
Ahsante mama, Rais Samia kwa kusikiliza ushauri huu. Mungu akuweke na utakumbukwa kama kiongozi Bora wa Taifa hili. Mimi nakuita Magareth Thatcher mwanamapinduzi na mwanamabadiliko ya kweli
 
N
Mhe.Rais wa JMT,
Mhe.Waziri wa TAMISEMI

Nawapongeza kwa jitihada zenu katika kutengeneza na kutoa fursa za ajira nyingi sana katika kada ya ualimu na Afya. Ni ishara njema katika kupunguza tatizo la ajira nchini.

Mhe. Waziri wa TAMISEMI, maoni na mapendekezo haya ni kwa ajili ya ofisi yako ikiwa kama ofisi inayoratibu mchakato wa ajira za ualimu na Afya zilizotangazwa hivi karibuni. Maoni yangu yatasimamia katika mchakato wa kuomba mpaka kupangiwa vituo.

Ni ukweli usiopingika ,usaili au mtihani ni moja ya njia nzuri ya kupata watu walio bora na usaili ni moja ya mchakato muhimu katika ajira.

Hali imekuwa tofauti kwa ajira za TAMISEMI, labda pengine kutokana na wingi wa wanaoomba au kuwapunguzia gharama waombaji ,usaili au mitihani huwa sioni ikifanyika. Je, mna uhakika gani mliyepatia ajira ni bora kuliko mliyemuacha?

Utaratibu huu wa kuchuja na Kuwapatia ajira bila kuwepo usaili au mitihani lazima utaingiwa na dosari za upendeleo na kupatikana kwa watu wasio na sifa na wenye sifa kuachwa.

Ni vema utaratibu ukabadilishwa ili kutoa fursa sawa kwa waombaji na uangaliwe utaratibu wa kuwafanyia walau "ONLINE APTITUDE TEST" waombaji utazamwe. Kila muombaji ashiriki kwenye test kwa walau hata ya somo moja la atakalofundisha.

Pia katika utaratibu huu wa ONLINE APTITUDE TEST sio lazima waombaji labda walioomba kufundisha' biology' wafanye test ya aina moja, ili kuepusha kupeana majibu au udanganyifu wanaweza kupewa test tofauti au kama ni test ya aina moja mpangilo wa maswali ubadilishwe baina ya waombaji.

Tutumie walau njia hii kuondoa upendeleo wa aina yoyote au lawama kwamba nilikosa huku nikiwa Nina sifa.

Matumaini maoni haya yatakuwa ni msaada katika upatikanaji wa watumishi bora na sahihi.

Ahsante.
aunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom