Kwamba tangu tumepata uhuru huyu ndie Rais ambae wananchi wanamchukia na hawamkubali?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
7,748
Reaction score
10,288
Nimefuatilia mijadala ya watu sehemu mbali mbali na kugundua kuwa huu wa utawala wa Mama watu wanasema hawaukubali.

Mbaya zaidi wanasema tangu tumepata uhuru huyu ndie mkuu wa nchi anayechukiwa na raia wake !

What is going on?
 
Sijui kuhusu utawala wa Mwalimu. Nianzie kwa Mwinyi ambako tayari nilikua najielewa. Utawala wa Mwinyi ulisemww, wa Mkapa ulisemwa, wa Kikwete wote tunakumbuka ulibagazwa sana, wa Magufuli halikadhalika. But kiukweli pamoja na tawala zote izo kuwa zinasemwa bado wananchi hawakupotrzs iman na serikali zao na kutoziunga kwa kiasi kikubwa kama ilivyo awamu hii.
 
Product ya Magu.. Kila kitu kina asili yake
 
Magufuli alichukiwa sana na kuna wengi ambao hawakuwa wakimpenda ila pia alikuwa na kundi kubwa la wananchi ambao walimpenda hasa watu wa hali ya chini hadi akawa anajiita rais wa wanyonge.

Lakini kwa Samia inaonekana wasiomkubali ni wengi zaidi ndio maana anapitia hii misukosuko, ni kweli hakuna anayependwa na watu wote ila kwake wanaompenda ni wachache kuliko wasiompenda.
 
Product ya Magu.. Kila kitu kina asili yake
Mbona husemi JPM ni product ya JK? Maana utekaji ulianza wakati ule? Kuna kitu ambacho huwa hamkifikirii. Motivation na Enhancement factor. CCM system hasa baada ya Mtandao Group.

Precedence; baada ya kundi lile kubadiri system na kuwa na Mtandao kila group au awamu inaanza na yake, hadi mifuko ijae

System ya CCM itaendelea hivi hivi, na sasa imefikia kilele uwe insider or outsider, wote ni risky,

King Maker wako pale plae
 
Nimefuatilia mijadala ya watu sehemu mbali mbali na kugundua kuwa huu wa utawala wa Mama watu wanasema hawaukubali.

Mbaya zaidi wanasema tangu tumepata uhuru huyu ndie mkuu wa nchi anayechukiwa na raia wake !

What is going on?

Nimefuatilia mijadala ya watu sehemu mbali mbali na kugundua kuwa huu wa utawala wa Mama watu wanasema hawaukubali.

Mbaya zaidi wanasema tangu tumepata uhuru huyu ndie mkuu wa nchi anayechukiwa na raia wake !

What is going on?
Amepata kura 31 milioni lakini 🤣🤣🤣
 
Huyu ndie anapendwa na watanzania kuliko yeyote yule ushindi wa kishindo wa 97 sawa tu na asilimia 100 inaonesha jinsi anavyopendwa hata kuzidi nyerere
 
Nafikiri hata yeye anawaza kwamba imekuwaje, Ila kiukweli uongozi wa Rais Samia unachukiwa sana, ukikuta kikundi cha watu 10 labda mmoja au wawili ndio watamtetea, angalau au asiwepo kabisa wa kumtetea.

Binafsi nimeridhisha na maswala mawili hakika yanayogharimu uongozi wa bi mkubwa, kwanza kabisa UTEKAJI hili swala kama kuna aliyemshauri kusilence wapingqji wake kwa staili hii inabidi amfukuze kazi ikibidi na yeye ampoteze.
Majivuno na Dharau: Viongozi wa awamu ya mama wamekuwa na viburi sana, Dharau kwa wananchi kiasi unajiuliza hawa hawajui kwamba mishahara yao ni kodi zetu? mifano ipo mingi, hamieni Burundi, ambia mumeoa akuzalishe etc......lkn pia usalama wa raia na Mali zao, Jeshi la Polisi limekuwa likilalamikiwa sana, hili halina mjadala, tunatokaje hapa kwenye hii Kona? CCM wenyewe wanasubiri miujiza.
 
Exaxtly
 
Sijui kuhusu utawala wa Mwalimu. Nianzie kwa Mwinyi ambako tayari nilikua najielewa. Utawala wa Mwinyi ulisemww, wa Mkapa ulisemwa, wa Kikwete wote tunakumbuka ulibagazwa sana, wa Magufuli halikadhalika. But kiukweli pamoja na tawala zote izo kuwa zinasemwa bado wananchi hawakupotrzs iman na serikali zao na kutoziunga kwa kiasi kikubwa kama ilivyo awamu hii.
Hakuna utawala utakaokosa lawama au kukosolewa. Hili ni 100% given kwani kufanya makosa ni moja ya kanuni za maisha. Tatizo liko kwenye kiwango cha kutopendwa. Huyu ''form four D moja'' hapendiki hata kidogo. Mtaani kila mtu anamwona hafai. Amejaribu kuzima upinzani wote na kubaki yeye huku akijitangaza kwa kila namna lakini raia ndiyo wanazidi kumchukia.
 
Amepata kura 31 milioni lakini 🤣🤣🤣
Inawezakuwa katika hiyo milioni 31 nyingi ni kura za majini ndio maana pamoja na idadi kubwa hiyo ya kura ila kama hawaonekani hao watu.

Unajua asili ya binadamu ni ubinafsi

Kipindi cha Magu alichukiwa na matajiri,wasomi wengi,wapinzani na CCM wengine ambao aliwanyima ulaji.

Upande wa wananchi wa kawaida wanaopiga mishe zao mtaani wasiokua na mambo ya vyama usingewaambia chochote kuhusu Magu wakakuelewa na hili ni kundi kubwa zaidi na lilimpenda Magu kwa ubinafsi wao tu bila kujali uminywaji wa demokrasia,utekaji n.k

Kwa awamu hii nadhani wameungana hawa wananchi wa kawaida,wapinzani na wasomi wengi kuuchukia huu utawala,amebaki na wanufaika wa mfumo either direct au inderict m.f machawa,ndugu,jamaa wa viongozi n.k
 
hata hao viongozi sio kwamba wanampenda , bali wanampenda kinafiki na kumpa sifa za kinafiki ilimradi mambo yao yaende
 
Nimefuatilia mijadala ya watu sehemu mbali mbali na kugundua kuwa huu wa utawala wa Mama watu wanasema hawaukubali.

Mbaya zaidi wanasema tangu tumepata uhuru huyu ndie mkuu wa nchi anayechukiwa na raia wake !

What is going on?
Pole pole alikua anamshauri vizuri uyu mama kuliko wanaomzunguka , bila kumumunya maneno polepole angesikilizwa ,wenda kuna mambo ndani ya nchi yangekua sawa bila kujali ni mwana ccm.

Lissu ameshauri vizuri mno , nagundua kwa sasa nchi hii inataka mazombi tu , maana wenye busara ,hekima ,hawatakiwi kabisa
 
Back
Top Bottom