Kwamba Tumefikia Mahala Mfanyabishara Anabembelezwa Kulipa Kodi?

M
Mkuu sijakuelewa emu andika kwa utulivu sijaipata hoja yako vizuri
 
Watu wanakamuliwa kodi kibao halafu reports za CAG zikitoka wahuni wamepuna kila mahali na mnaishia kusema STUPID, sasa kwa nini msiwabembeleza watu kuendelea kulipa?

Hizo kodi hazijaandikwa kwenye msahafu hivyo zinazungumzika.
 
Tukiacha unafiki, nasema, tukiacha unafiki upo uwezekano tukaliangalia hili jambo[Kufuata na kuheshimu sheria za nchi]kwa kina na kwa tija za Mustakhabali wa nchi.

Serikali inawakemea wafanyabiashara kana kwamba wanahalalisha uasi wao....yaani, kwamba kwa kulainisha mwenendo wao usiofaa kama jibu la uvunjaji wao wa sheria, na kisha kuvunja na kukandamiza sheria au kanuni zingine, inatoa picha kuwa ni poa kufanya kitendo hicho au vingine vya namna hiyo ya uvunjaji wa sheria halafu Ukapata same response.

Hiyo ni hatari.



Tuheshimu na Kutii Sheria za Nchi. Two wrongs don't make a aright au hatutabakia na Sheria.
 
Nilifunga duka kariakoo yaani watoza ushuru wanataka rushwa kila mwezi leo wamekuja na hiki kesho na kile sasa hivi nauzia Lusaka hakuna tatizo nikipakia mzigo nikishusha sio kama huko unalipia mzigo unaposhusha TRA kibao wanataka rushwa pana Mkongo niliwahi muelekeza aje anunue Suti hapo si walikamata mzigo wake akipeleka Jangwani upelekwe Tunduma wazee waliupeleka mpaka yard wakisema kapewa risiti ya hela ndogo na duka halijui taarifa za kwenye risiti sio sahihi mkuu jamaa ilibidi atoe hela ya nauli ya mzigo analalamika mpaka kesho wakati SA SARS ndio walinzi wa wageni hawawezi kufanya huo ujinga hata iweje Tanzania TRA wanaua biashara kwa maujinga yao...
 
Hapo bandarini bila enforcement nani atalipa? Kwani Kila mzigo unaingia kutoka bandarini? Mzigo unaozalishwa kiwandani au Kwa mtu binafsi itakuaje?

Task force inazuia na magendo Sasa ngoja tuone nani atazuia magendo huko mipakani nk.

Kiwanda gani kinauza mali bila TRA kujua? TRA wameajiri watu wa aina gani ambao hawana fikra wala ubunifu zaidi ya kutumia task forces?
Basi TRA ivunjwe. Task force iwe rasmi kukusanya kodi. Maana pengine hawana watu wenye maadili wala uwezo wa kuifanya kazi hiyo, bila kutumia janja jana ya kutengeneza mazingira ya kupokea rushwa
 
Daah Bongo kiboko kodi la Chevrolet ya 2014 wanataka 40m tutaendelea kuendesha vibebi walker na kuvisifia tu na kikipata ajali ndogo tuu kinaondoka na watu...ndio maana wengi wanapenda kukwepa kodi hizo kodi zao sio rafiki kabisa..
 
Daah Bongo kiboko kodi la Chevrolet ya 2014 wanataka 40m tutaendelea kuendesha vibebi walker na kuvisifia tu na kikipata ajali ndogo tuu kinaondoka na watu...ndio maana wengi wanapenda kukwepa kodi hizo kodi zao sio rafiki kabisa..
Mazingira ya hii nchi ni magumu sana, yaani kodi zipo kumkomoa mwananchi na si kufanya awe na hali bora.
 
hizo kodi wanalipa wao tu wafanyabiashara wa kariakoo? mim ningekuwa kiongoz ningetoa siku 3 maduka yote yawe yamefunguliwa duka ambalo litakuwa limefungwa basi litavunjwa na atapewa mtu mwingine mwenye uwezo wa kulipa kodi kuendelea na Biashara
 
Mzigo unaoshuka kutoka bandarini unalipwa kodi kisha kupelekwa godauni yanini tena kuufuata mzigo huo huko?
 
Mfanyabiashara anapogoma kumbuka pia anakutetea na wew kwenye bei ya bidhaa isiwe kubwa [emoji35][emoji35] [emoji856][emoji35] inabd tuwaangu mkono kama kweli hizo kodi ni za manyanyaso

N:B kumbuka mfanyabiashara halip kodi analipa n mteja[emoji2484]
 
M

Mkuu sijakuelewa emu andika kwa utulivu sijaipata hoja yako vizuri
Nasema hivi
1.Waajiri Watumishi wengi Ili wawepo Hadi kwenye ngazi ya kata
2.Wapewe vitendea kazi kama magari na pikipiki
3.Hao maofisa watafanya kazi za enforcement na usajili wa biashara
4.Hao maofisa watakuwa wanafanya ukaguzi Kwa manunuzi yote ya mtu mmja mmja kama Wana risiti Kwa oparesheni,Vituo vya uzuizi.
 
Mzigo unaoshuka kutoka bandarini unalipwa kodi kisha kupelekwa godauni yanini tena kuufuata mzigo huo huko?
Mzigo unaozalishwa ndani ya Nchi inakuaje? Mfano mazao ya misitu Hayatendi bandarini hiyo enforcement mtafanyaje?
 
Nafikiri kama mfanyabiashara ameshakadiriwa na mamlaka ya mapato,hakuna sababu ya kuwatumia task force kufuatilia tena kwa sababu hizi kodi zinalipwa kwa awamu nne katika kipindi cha mwaka mmoja, sheria ya kodi iweke wazi kama mtu ameshakadiriwa basi watumishi wa TRA wasiwasumbue na kukamata shughuli zao kwa Sababu wameishakadiriwa kiwango cha kodi watakacholipa kwa mwaka mzima.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Taskforce inatumika kuhakikisha mfanyabishara anatoka risiti Ili kupima Ukiwa wa biashara yake kumbuka Hawa hawana taarifa za kifedha kama financial statements.
 
Kodi yenyewe ndio ya kununulia V8? Nani atakuwa na ari ya kulipia bila shuruti? Vikosi ni vya rushwa na ubambikiaji Kodi zisizo na msingi.
 
Kodi yenyewe ndio ya kununulia V8? Nani atakuwa na ari ya kulipia bila shuruti? Vikosi ni vya rushwa na ubambikiaji Kodi zisizo na msingi.
Hata ingekuwa ni ya kununulia wali wa Watoto wa shule hakuna mtu anapenda kulipa for willing.
 
Wafanyabishara wanasema hawataki kulipa kodi kwa nguvu, wanataka wampewe uhuru wa kulipa kodi, wanasema EFD inaua biashara hawazitaki. Kesho utasikia EFD zinafutwa kariakoo.

Hii nchi ina safari ndefu sana.
 
CCM ni serikali ya hovyo sana, hawako serious katika kuendeleza hii nchi yetu. Unamnyenyekea mfanya biashara ambaye anaitapeli nchi kweli? Kamata hawa watu tia ndani, uone kama wengine hawatoshika adabu, ulipaji kodi ni muhimu na ni wajibu wa kila mtu kulipa na asiyelipa aswekwe ndani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…