Kwangu mimi hiyo ndiyo hotuba ya maana kuliko zote zilizopata kuhutubiwa na Hayati mzee Nyerere

Watu wengi wavivu wanapenda vya bure ndio maana walikimbilia socialism..

Mwendazake ni mfano mzuri wa incompetent leader kama jamaa alivyomtolea mfano Nkrumah,Magu kaacha lundo la madeni with nothing to show off,miaka 6 imeisha hakuna hata mradi alioanzisha uliofikia japo 50% .

Matokeo yake Samia anatafuta pesa za kulipa madeni na kumalizia miradi ambayo ni tembo mweupe..

Hii incompetence ya leadership ni janga Sana,watu hawataki kuruhusu wenye akili wajadiliane afu wafikie muafaka wa namna ya kwenda,pia issue ya ego kwa Africans ni tatizo kubwa Sana..
 
State inamiliki vitu gani?
China, the world's second largest economy, has the largest number of state-owned enterprises (SOEs) in the world – over 150,000.
In many other countries, especially in the West, the number of SOEs is much smaller, normally in single digits.
According to the Fortune Global 500 list 2020, 117 of the global top 500 companies are based on the Chinese mainland and 91 of those are SOEs. There are 121 companies from the United States in the top 500, but none of them are government-owned.

 
Maisha ya kuiga yatawaharibu,,Wachina sio Watanzania wao ni model yao na inaonekana ku work kwao tuu .

Pili aina hiyo ya Mashirika ya China hayapo hapo kutoa huduma kwa watu maskini wa China bali yako kufanya biashara kama mashirika mengine.

Sasa Ili yawe na ufanisi lazima uatatumia mbinu zile zile za kipepari ,yataajiri CEO mzuri na ku recruit competent staffs ambao watalipwa vizuri.

Tzn hapa Tulikuwa na Mashirika ya hivyo enzi za JK kama shirika la nyumba,mashirika ya pensheni nk ambayo yalikuwa yanajiendesha kibiashara but alivyoingia mtu wenu incompetent akavuruga kila kitu.
 
Ni kweli watu wana dhani Kwame Nkuruma ni shujaa sana, nilisoma mahali jamaa alikua na wivu na umoja wa africa mashariki akawa anaupiga vita
 
Maisha ya kuiga yatawaharibu,,Wachina sio Watanzania wao ni model yao na inaonekana ku work kwao tuu .
Hakuna nchi iliyogundua mfumo wake kuutengeneza hii mifumo ipo kulingana na wakati na different models kulingana na different ideologies hata Wachina sio Forefathers wa Socialism; UK pia walijaribu at one time or another..., all in all you can not privatize your commanding heights of your economy ni kama kuweka rehani maisha ya nchi

Marekani hadi prisons at one time or another walizi-privitize ili private sectors waziendeshe kilichotokea pamoja na hao kupewa ruzuku ila kuna malpractise za kutosha mpaka kupelekea wengine kufungwa kesi ndogo ndogo ili tu numbers ziongekeze...., kuna nchi waliprivitise shirika la reli (ili kuongeza faida na hao shareholders ku-cut costs) kukapelekea ajali kuongezeka n.k.

Huko tunakosema capitalism is working is not working that much either Unashangaa Marekani kuna homeless people wa kutosha wakati kuna nyumba tatu tupu for every one homeless person... Na kama nilivyosema hapo awali mafanikio ya hizi nchi nyingi ni faulo wanazocheza na marginalization ya poor countries..., bila wahindi kushona mashati ya Nike huko India na kulipwa peanuts unadhani huko wangefurahia mashati ya Nike, bila kupata raw materials kwa bei za kutupwa wangeweza kustain maisha yao ya kifahari ?

Na ingawa tunawaita mabepari bado wana vitu kama foodstamps na other welfare programs (jambo ambalo kwenye Ubepari per se haipo hivyo; that's socialistic features)
 
Mzalendo pekee aliyeishi katika mawazo ya ujamaa, hawa wengine ni wazalendo uchawara wanaishi kwenye majumba ya kifahari, wanamiliki biashara wanapiga madili hafu wanakwambia wao ni wazalendo
 
Marekani mpaka leo kuna magereza yana milikiwa na private companies. Ila dhana ya ubepari ni ile binadamu amezaliwa huru muache aishi huru hata kama kuna mipaka. Na hio ideology inaongeza innovation
 
Maisha ya kuiga yatawaharibu,,Wachina sio Watanzania wao ni model yao na inaonekana ku work kwao tuu .

Pili aina hiyo ya Mashirika ya China hayapo hapo kutoa huduma kwa watu maskini wa China bali yako kufanya biashara kama mashirika mengine.
Unajua maana ya State owned ? kwahio yakifanya biashara alafu faida anachukua CEO au inalisaidia taifa kwa ujumla ? Kumbuka hizo ni kampuni kubwa na hazifanyi kazi nchini kwao tu bali world over kwa faida ya uchina kwa jumla
Sasa Ili yawe na ufanisi lazima uatatumia mbinu zile zile za kipepari ,yataajiri CEO mzuri na ku recruit competent staffs ambao watalipwa vizuri.
Kwahio Ujamaa unamaanisha kuajiri uncompetent staff na kuwa na CEO mbaya, kulipa vizuri ni subjective kuna Mabenki ya Marekani ambayo yalikuwa yanalipa bonuses kulingana na on paper kampuni inafanyaje, kilichotokea kila mtu anajua (refer Global Crisis iliyotokea miaka michache iliyopita)

Pia kumbuka socialism on paper lakini socialism nyingi zilizokuwa zikifanyika ni capitalists in socialist clothes yaani wachache kujilimbikizia mali na kuwanyonya wengine
Tzn hapa Tulikuwa na Mashirika ya hivyo enzi za JK kama shirika la nyumba,mashirika ya pensheni nk ambayo yalikuwa yanajiendesha kibiashara but alivyoingia mtu wenu incompetent akavuruga kila kitu.
Kwahio unaona shirika la nyumba lililojengwa kwa misingi ya affordable housing for all ambayo sasa hivi lingepunguza shida ya watu kupanga nyumba lilivyochukuliwa na asset zake ili lianze ku-compete na private sectors kwa kufanya hizo nyumba sio affordable tena ndio umahili ? Nyumba ngapi wamejenga zimekuwa magofu kwa watu kushindwa kupanga kutokana na kodi zao... Tukija kwenye mashirika ya pensheni na kuanzisha white elephant projects ili watu wapige pesa bila kufanya due dilligence ndio inayopelekea mifuko hii kupumilia mashine...,
 

Ukiangalia majanga makubwa yote duniani ni pesa ya umma ndio iliyokwenda kuokoa kampuni binafsi Raia. Socialism save capitalism.

2008 credit crunch kampuni nyingi, benki, sekta za kutengeneza magari zilipewa mikopo na kusimamia na serikali.

100% capitalism :- ungeacha viwanda, benki,biashara zife watu wasioweza kujitegemea wafariki.

Wakati wetu wa Pandemic zjangs la Corona, kampuni nyingi zimepewa kipato kila mwezi, ziliondolewa kodi na wakazi wote wamelipwa kukaa ndani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Chanjo ni bure. Serikali inagharimia. Makazi kuna nyumba za serikali za bei nafuu, ukiwa huna kazi, unaumwa unapewa pesa za kujikimu, afya na elimu bure.

Huu ni ujamaa, kusaidia wakati wakati wa matatizo ulio na asilimia fulani ya upebari.

Ili jamii iwe na ustaarabu lazima iwajali watu wake wote, hata wa chini kabisa.
 
Mzalendo pekee aliyeishi katika mawazo ya ujamaa, hawa wengine ni wazalendo uchawara wanaishi kwenye majumba ya kifahari, wanamiliki biashara wanapiga madili hafu wanakwambia wao ni wazalendo

Hawajali hata familia zao, wakulima, walipotoka,majirani zao hakuna uzalendo wowote hapo.

Wanakwambia CCM/Tanzania ina wenyewe ingawaje wenyewe wamesomeshwa na kupata dhamana ya kuongozaTaifa.

Wamepanda ngazi, wamefika juu wameipiga teke. Hawaitaki wengine wapande ngazi hiyohiyo.
 
Marekani mpaka leo kuna magereza yana milikiwa na private companies. Ila dhana ya ubepari ni ile binadamu amezaliwa huru muache aishi huru hata kama kuna mipaka. Na hio ideology inaongeza innovation
Ndio maana nikasema practically hakuna 100 percent socialism au 100 percent capitalism ni mixed economies

Mimi sina neno na kila Bill Gates au Tesla, Google, Amazon kuleta innovation na kufaidika na nguvu zao, ila hio ni tofauti na kusema huu mgodi ni wangu au hili ziwa ni langu au hiki kijiji chote ni changu sababu babu yangu aliniachia thus hakuna mtu kulima hapa au kuchota maji

Tatu maendeleo ya hawa mabepari wamepiga hatua kwa marginalizion ya watu au nchi fulani in a competitive world watu wanaenda kwenye nchi za mbali na kuwanyonya na kuharibu mazingira kuweka sumu ili tu wapate faida for their shareholders

By the way current innovation nyingi zimetokea kwenye army sababu ya investment kubwa pia nyingine mfano graphical user interface (iliyopita kwa apple mpaka windows) ilitokea kwenye research ya vyuo vikuu kwahio innovation is pushed by investments na mara nyingine ni state money au big corporations inayosaidia hizo research and developments
 
Hawajali hata familia zao vijijini,majirani yao hakuna uzalendo wowote hapo.

Wanakwambia CCM/Tanzania ina wenyewe ingawaje wenyewe wamesomeshwa na kupata dhamana ns Taifa.
Hafu hao wanaiomba inawenyewe ndiyo waliojaa kashfa za rushwa na kuuziana/kujimilikisha mali za chama kihuni
 
Kwani ujamaa wa Tzn na jinsi state enterprises zinavoendeshwa huoni kwamba zimeajiri incompetent staff ? Kujuana kumezidi na upuuzi kama huo.
 
Msiojiamini na ambao hamjafikia viwango vya ustaarabu ndio mnaona privatisation ni kuuza Nchi ,walio na mfumo huo wameuzaje sasa hizo Nchi?
 
Ujamaa wa Nyerere mwenyewe aliandika kwenye kitabu chake. Kwa nini Nyerere hakuiga economic reforms za China wakati bado anatawala? Unamuongelea mythical Nyerere wa propaganda za CCM, siyo Nyerere wa kweli. Nyerere mpaka mwisho wa maisha yake alikuwa ni true believer wa Ujamaa wake.
 
Msiojiamini na ambao hamjafikia viwango vya ustaarabu ndio mnaona privatisation ni kuuza Nchi ,walio na mfumo huo wameuzaje sasa hizo Nchi?
You can not privatize commanding heights of the economy (private sectors zinaweza zikafanya kazi sambamba na state owned (kuna ugumu gani wa private sectors kuanzisha chao from scratch)? Mfano kuliko ku-private infrastructure ya reli unaweza ukaruhusu private trains kwenye reli ya taifa (unless private companies wana-own ya kwao, wametengeneza wenyewe ) Au huwezi kwenye ndege ukawapa watu exclusivity ya routes (unawaruhusu wa-compete sambamba) in short kuzigawa commanding heights ni kukaribisha ujanja ujanja na upigaji kwa faida ya wachache..., Unadhani Russia baada ya USSR kuanguka watu walivyojigawia migodi na maliasili ya taifa kama njugu (ndio umepata hawa kina Roman Abramavich) Ingawa nadhani Putin alianza kuwabana baadhi (ingawa na yeye wanasema ni mpigaji) kurudisha keki ya taifa....
 
Hali ya uchumi sasa hivi walaumu hao hao CCM waliorithishwa nchi na Nyerere. Halafu kama tulikuwa hatuna wataalamu wa kuendesha nchi kwa nini Nyerere alikuwa na kiherehere cha kutawala? Alivyokuwa anagombea uhuru aliulizwa kama tuko tayari kujitawala. Visingizio vya ukame hata siku moja sivikubali. Angalia nchi kama Israel iko jangwani kabisa lakini uchumi wao umekua. Kuna nchi ngapi za kiarabu pia ziko jangwani hazipati mvua na zina uchumi mzuri? Ni visingizio tuu.
 
Kama Nyerere anapewa sifa ni sawa pia akipewa lawama. Kwa nini apewe sifa za umoja na uzalendo wa Watanzania lakini asipewe lawama za kuliacha taifa limefilisika na umasikini wa Watanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…