Kwangu mimi hiyo ndiyo hotuba ya maana kuliko zote zilizopata kuhutubiwa na Hayati mzee Nyerere

Kwangu, The Best ni ile aliyoitoa Songea, wakati anaitangazia Dunia kuwa, sasa tunaingia vitani kupambana na Idd Amini. Na pia, ile ya Mei Mosi 1995 kule Mbeya.
 
Hivi unajua advanced technology ya muisrael, unajua support anayopewa ili kuisupress middle east by the way talking about Ujamaa unajua kitu kinaitwa Kibbutz (Huu ni mfano wa vijiji vya ujamaa na mashamba ya ujamaa) Israel ndio waanzilishi na viongozi wengi wa sasa walikulia kwenye hizo Kibbutz
Kuna nchi ngapi za kiarabu pia ziko jangwani hazipati mvua na zina uchumi mzuri? Ni visingizio tuu.
Unajua kitu kinaitwa Black Gold AKA OIL ? basi hizo nchi they have plenty of the stuff...., Pia tofautisha nchi ambayo imezoea Ukame hence kuwa prepared na inayopigwa na njaa / ukame wa ghafla all plans zinatoweka na nguvu zote kuwekezwa kwenye kulisha raia
 
Kama Nyerere anapewa sifa ni sawa pia akipewa lawama. Kwa nini apewe sifa za umoja na uzalendo wa Watanzania lakini asipewe lawama za kuliacha taifa limefilisika na umasikini wa Watanzania?
Ulitaka akuachie Tshs ngapi kwenye akaunti yako binafsi ? Kuhakikisha tu baba au babu yako amesoma bila kuhitaji mikopo na kutokuuza nchi kwa mikataba mibovu ya madini na so called wawekezaji unaona hio haitoshi ?

Au alifilisi vipi alikwenda kwenye mbuga za wanyama na kuua tembo wote na Simba ? au Alihamisha mlima Kilimanjaro uende Rwanda ?
 
Nonsense
 
Wahuni gani waliivuruga wakati Nyerere alikuwa madarakani na hakuwa na upinzani? Alichotaka kufanya kilifanyika. Kwa hiyo matokeo yake ni yeye alaumiwe.
 
Tumia economic indicator yoyote ile utaona Nyerere alifeli kiuchumi. Nimeshasema Nyerere kasomesha watu bure lakini uchumi ulimshinda. Na hao unaosema wamefilisi mbuga za wanyama nani aliwarithisha nchi? Nani alikataa upinzani na demokrasia tangu nchi inapata uhuru?
 
Sera za kijamaa za China zilikufa na Mao Zedong. Walifungua uchumi wao wawekezaji wakamwagika kule. Nyerere alizing'ang'ania sera za ujamaa mpaka mwisho.
Kama sera za kijamaa China zilikufa na Mao,na Nyerere ana miaka mingapi tangu afariki?.
Na kuna mabadiliko gani ya kiuchumi Tanzania so far.
 
Ukame wa ghafla? Ina maana Nyerere alipanga mvua kunyesha kila mwaka? Yeye ni Mungu au? Unafikiri ukame wa ghafla hautokei sehemu nyingine duniani ni sisi tuu tuliupata?
 
Kama Nyerere anapewa sifa ni sawa pia akipewa lawama. Kwa nini apewe sifa za umoja na uzalendo wa Watanzania lakini asipewe lawama za kuliacha taifa limefilisika na umasikini wa Watanzania?

Lawama sawa apewe bila kusahau mazuri aliyoyafanya.

Shida ni pale unapoongea like the guy did nothing. Hapohapo unamrushia zaidi lawama hata kwa yale ambayo yanatakiwa yawe yamebadilishwa na waliofuatia.

Naheshimu maoni na mawazo yako sana tu, lakini heshima ya huyo mzee si ya kutilia shaka.
 
Ukame wa ghafla? Ina maana Nyerere alipanga mvua kunyesha kila mwaka? Yeye ni Mungu au? Unafikiri ukame wa ghafla hautokei sehemu nyingine duniani ni sisi tuu tuliupata?

Naomba utuwekee muongozo mkuu, tufanye Nyerere katutumbukiza na anastahili lawama zote hadi kutufikisha hapa.

Wewe ungefanyaje ungechukua kijiti baada ya yeye kung'atuka madarakani?
Tupe mpango wako ambao waliofuatia hawakuufuata na lawama anarudishiwa Nyerere?

Ikiwa China waliachana na Ujamaa na sasa hivi wametupiga gape, wamepatia wapi na sisi tumekosea wapi mtaalam.
 
Kama sera za kijamaa China zilikufa na Mao,na Nyerere ana miaka mingapi tangu afariki?.
Na kuna mabadiliko gani ya kiuchumi Tanzania so far.
Siyo kwamba nasifia uchumi wa sasa ila wakati wa Nyerere hali ilikuwa mbaya sana. Watu walisota sana. Mwinyi alivyoingia na kuanza economic reforms kidogo tukapata pumzi. Maana waya ulikua mkali sana. Walioishi enzi za Nyerere wanajua umasikini tuliokuwa nao.
 
Nimeshampa mpa sifa zake Nyerere alizostahili. Alisomesha watu bure, alileta umoja na uzalendo ila kwenye uchumi alifeli na Ujamaa wake. Kwenye mambo ya demokrasia alifeli. Huu ndiyo ukweli tusikatae.
 
Nimeshampa mpa sifa zake Nyerere alizostahili. Alisomesha watu bure, alileta umoja na uzalendo ila kwenye uchumi alifeli na Ujamaa wake. Kwenye mambo ya demokrasia alifeli. Huu ndiyo ukweli tusikatae.
Sema mtizamo wako ila sio ukweli. Ndio maana kila mmoja anatoa maoni tofautitofauti kuhusu mtu huyo huyo mmoja.

And let me remind you, he once said he did a lot of mistakes, a good number of them. But dwelling on those mistakes instead of good ones and move on would be a fatal mistake.
 
Ukame wa ghafla? Ina maana Nyerere alipanga mvua kunyesha kila mwaka? Yeye ni Mungu au? Unafikiri ukame wa ghafla hautokei sehemu nyingine duniani ni sisi tuu tuliupata?
Ulizia katika kipindi cha hivi karibuni Tanzania ilipigwa na Ukame miaka ipi na hadi kupelekea misaada ya ugali wa yanga (mahindi ya njano) na watu kupelekea kufunga mikanda No matter hio hali ikitokea lini au wapi nchi lazima itetereke ukizingati hicho ni kipindi ambacho machinery ni pilau inasukumwa na ngombe na sio tractors let alone combined harvesters.....

In short it was Hard Times.... Na sio Bongo tu nchi nyingi zishapitia huko at one time or the other
 
Swali gumu maana hata ningechukua kijiti, mfumo na taasisi alizojenga Nyerere bado zipo. Walichofanya Wachina ni kuwakamata wale waliofanya cultural revolution walihukumiwa kifo na wengine walifungwa maisha. Hapa ukijaribu kufanya hivyo nchi itavurugika.
 
Katika hiyo miaka 21 aliyokuwa madarakani, huo ukame wa ghafla unaotumia kama kisingizio ulitokea miaka mingapi?
 
Sawa lakini mazuri aliyofanya Nyerere kila siku yanaimbwa na yanatumika kwenye propaganda za CCM. Mabaya yake yanafukiwa. Hatuwezi kuendelea kama hatutazami wapi tulikosea na wapi tulifanikiwa. Angalia jinsi Wamarekani wanavyowajadili hao mababa zao wa taifa, wanawaita watu waliomiliki watumwa ingawa pia walifanya mazuri. Mazuri na mabaya yao yanawekwa wazi.
 
Itakuwa ni myopic thinking kwa kutokuona hasara ya kubinafsisha nguzo kuu za uchumi wa Nchi..., Kampuni / Sekta kubwa ni too big to fail... yaani hata leo tukimpa mtu achukue Tanesco na miondombinu yake akifanikiwa atakula yeye pesa na shareholders wake aki-fail ni wewe na mimi Kodi zetu zitatumika ili kumpa ruzuku ili aendelee kufanya kazi Win / Win kwake na ndio kilichotokea / kinachotokea mara kwa mara tangu enzi na enzi hata enzi za British East Africa Company was too big to fail...,

Matokeo ya kampuni ambazo ni too big to fail ni kodi za mwananchi zinatumika kulea matatizo yakitokea faida ikitokea wanakula wachache
 
Mbili kati ya kampuni tano kubwa duniani kwa mapato ni state owned (China).
Hakuna ujamaa china
1. State Grid
2. China National Petroleum
3. Sinopec Group
4. China State Construction
5. ICBC
Hizi ni kampuni tano kubwa China zote zinamilikiwa na serikali ya China 100%. Huu ni ubepari gani?
 
Naunganisha tgo gb 72 za mwaka mzima ambapo kila mwez utapata GB 6 kwa siku 14 kwa mwaka mzima Bei Pm. ( Malipo kabla ya kazi).
Pia naunganisha free call tgo kwa miaka 2 ( malipo baada ya kazi)
[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]Only for seriously people.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…