Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya jambo la haraka kumuondoa Naibu Waziri wa Madini, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzungumza na kufanya kazi

Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya jambo la haraka kumuondoa Naibu Waziri wa Madini, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzungumza na kufanya kazi

Yeye ndi

Yeye ndiye aliyemchagua na yeye ndiye aliyemuondoa tatizo lipo wapi? Tuvimiliane maana yake una muhali wewe nchi haitaenda kwa kuvumiliana
Tuvumiliane katika ukosefu wa weledi wenye athari kubwa kwa maslahi mapana ya nchi!A big NO,hii sio awamu ya akina Vasco Dagama,hapa kazi tu,kama huwezi kazi,kule!
 
Siamini kama watu wa vetting hawakuwa na taarifa sahihi za huyu jamaa,chamsingi Rais kabla ya kusema pale angechunguza kwanza........
 
Naambiwa jamaa kumbe alipigwa na stroke wakati wa uchaguzi hvo hayuko fit 100%.
Na ameshika nyashifa mbalimbali hadi TFF amekuwa akisafiri na team.
TFF ni chaka Mkuu,ni kuwekana tu.Anyway aliyehusika kumchomekea Rais kihiyo kama huyo naye anastahili kuwajibishwa.Hatuwezi kuendelea hivi.
 
Naambiwa jamaa kumbe alipigwa na stroke wakati wa uchaguzi hvo hayuko fit 100%.
Na ameshika nyashifa mbalimbali hadi TFF amekuwa akisafiri na team.
TFF ni chaka Mkuu,ni kuwekana tu.Anyway aliyehusika kumchomekea Rais kihiyo kama huyo naye anastahili kuwajibishwa.Hatuwezi kuendelea hivi.
 
Hapana .nimeambiwa Ndulane alipata stroke kipindi cha uchaguzi.
Sawa,kama walijua alipata stroke,kwa nini walimchomeka,si wangeacha apone kwanzaa.....!Wana haraka gani?No,waliomchoneka watafutwe, wawajibishwe,hawako makini.Wameliabisha taifa.Si tunaonekana sasa kwamba watanzania wote ni vihiyo,no haikubaliki.Tukio hili lina very far reaching repercussions.
 
ikitokea tukamuchagua Rais siku ya uapisho akashindwa kabisa kuapa je atapisha ama uchaguzi utarudiwa??
 
Sawa,kama walijua alipata stroke,kwa nini walimchomeka,si wangeacha apone kwanzaa.....!Wana haraka gani?No,waliomchoneka watafutwe, wawajibishwe,hawako makini.Wameliabisha taifa.Si tunaonekana sasa kwamba watanzania wote ni vihiyo,no haikubaliki.Tukio hili lina very far reaching repercussions.
Suspect no 1 atakuwa Ni KsK
 
Waziri siyo mtendaji bali anashughulika zaidi na sera sasa kama hawezi kuongea then he is unfit for the position.
Acha uboya wewe, mbona Magu mwenyewe hawezi nyoosha sentensi tano za kingereza so naye hafai
 
Brother kuwa muangalifu na taarifa zako.sio kilwa kusini ni kilwa kaskazini!Aligombea kilwa kaskazini
 
Mm nahic jamaa huoni wake ni hafifu inawezekana Yale maandishi alikuwa anashindwa kuyaona vizur
 
Kushindwa kuongea ni kitu tofauti kabisa na kushindwa kusoma mistari michache. Huyu kashindwa kusoma hata baada ya kuachwa ajikusanye

Kama hawezi kucontrol emotions mbele ya camera, bora tu abakie na ubunge wake akakae benchi la nyuma kabisa
Kama ungefuatilia historia yake ya utendaji kazi, wala usingeandika hayo uliyoandika, ila kwakuwa kuna watu kila jiwe alifanyalo lazima mu support, sawa!! Kweli kwa mtizamo wa kibinadamu, hilo lilikuwa na kufanya utengue uteuzi wake?!!
 
ikitokea tukamuchagua Rais siku ya uapisho akashindwa kabisa kuapa je atapisha ama uchaguzi utarudiwa??
Haiwezekani Rais aliyechaguliwa kushindwa kuapa,that is unthinkable mkuu. Hata hivyo swali lako lina nia mbaya:kujaribu kuonyesha kwamba kitendo alichofanya Rais si sahihi,kwa hiyo tuvumiliane.

Nisisitize,maamuzi aliyofanya Rais ni 100% correct.Wengine wanasema alipata stroke huko nyuma,basi atibiwe kwanza apone,hatuwezi kufanya makosa kwenye masuala ya msingi.
 
Kwani wewe unafikiri ukiweza kunyoosha kiingereza basi wewe ni intelligence enough? Mkuu argue construstively!!
Yaani mkuu Watanzania dah!Yaani sijui kwa nini tunashindwa kuelewa kwamba Kingereza ni kama Kigogo,Kinywamwezi,Kizaramo nk.,it's just a language like any other. Walichofanya Waingereza ni kukipaisha Kingereza ili kionekane kwamba it is associated with sophistication and intelligence, hakuna lolote.People need to wake up.
 
Francis Ndulane alikuwa Mhasibu Mkuu wa Tanroads Mkoa Lindi, Magufuli alipo ingia Madarakani kama Rais akamteua kuwa Mkurugenzi wa Mji Ifakara.

Mwaka huu akagombea ubunge, kwenye kura za maoni ndani ya chama akashika nafasi ya tatu kwa kupata kura 21 nyuma ya Ahmed Raphael Bongi aliyekuwa amshindi wa kwanza kwa kura 155 ambaye alikuwa ni Mhasibu mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Ila kamati kuu ya CCM ikarudisha jina aliyeshika nafasi ya tatu Francis Ndulane kuwa mgombea jimbo la Kilwa kusini.

Rais Magufuli mwenyewe ameunda Baraza lake baada ya kupita takriban wiki 3 baada ya uchaguzi kupita ,hivi bila shaka alijidhihirisha kuwa ni mtendaji mzuri.

Kilichompata ndugu yetu kinaweza kumpata mtu yeyote katika mazingira yoyote mathalani ni jambo furaha hivo mhusika alikuwa yuko temper.

Mh. Francis Kumba Ndulane. Mbunge wa Kilwa kaskazini - CCM aliyekuwa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Nishati, kwa bahati mbaya ameondolewa katika nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kushindwa kuapa. Mh Ndulane anaonekana katika video akisoma kiapo kwa kusitasita kama anakigugumizi (stama).

Kilichompata Mh. Ndulane kisaikolojia kinaitwa ' Occasional Anxiety'. Kiufupi ni hali ya wasiwasi isiyotarajiwa inayomkuta mtu kufuatia jambo fulani kumpata au kulazimika kulifanya.

Jambo hilo laweza kuwa geni kabisa au kutokana na uzito wake likawa na mvuto mkubwa kijamii. Mazingira haya hutufanya baadhi yetu kuingiwa na wasiwasi hatimaye kushindwa kulifanya kwa ufanisi unaotarajiwa.

Katika mazingira ya uanafunzi, baadhi wanapokuwa katika vyumba vya mitihani ya taifa hukumbwa na hali hii. Hukuta hata mwanafunzi anashindwa kushika kalamu na kujikuta vidole vikitoa jasho huku mkono ukitetemeka,saa zingine hutokea wakati wa ku-present kitu ,niliwahi kusoma na msichana yani alipoingia panel alizimia kabisa.

Baadhi yetu tumeshuhudia katika mazingira ya vyuo vikuu, wanachuo wenzetu wakishindwa kusimama mbele ya wanafunzi wenzao na kuzungumza. Ipo mifano mingi.

Hali hii huwa haina kusema umesoma shahada (degree) ngapi. Ni tendo kisaikolojia. Katika matukio kama ya kuhutubia, kuapishwa nk.ndio maana ili kupunguza uwezekano wa kutukia kitu kama hicho, watu hulazimika kufanya kitu kinaitwa ' rehearsal' kabla ya tukio husika.

Tusimshambulie mh. Francis Ndulane kama mtu wa ajabu kwakuwa kilichomtokea, kimewatokea wengi na kitawapata wengi.

Tusimfedheshe. Tumfariji, hasa ukizingatia kapoteza fursa adhimu ambayo wengine huitafuta kwa udi na uvumba,wengine hutoa hadi kafara.

Hapo washauri wa Mh.Rais wanatakiwa kumshaauri vizuri haikupaswa hatua ya kumwondoa iwe kwa haraka vile. Lile ni jambo la kawaida sana.

Hakuna uhusiano kati ya utekelezaji majukumu kwa ufasaha na uwezo wa kuzungumza na ikizingatiwa kwa Ndulane nafasi kubwa kama ile nadhani ni ngeni na ni mara ya kwanza kwake kuteuliwa kuwa naibu waziri , lkn wkt mwingine feelings na namna mtu anavyolichukulia jambo kwa uzito mkubwa huweza kumfanya yeyote akakutwa na hali ile hali...ukichukulia ule ukali wa Magufuli wa kuwatukana mawaziri wapumbavu ndo basi kabisa Ndulane alitaka afanye haraka amalize.

Hata leo Biden alikuwa anaapisha baadhi ya watendaji kuna mama alikuwa anakosea hadi lugha lakini hamkumuondoa.

Tujifunze kuvumiliana.
Thats why there is always a room for the second chance.
Najua washauri wa Rais watamshauri ampatie jamaa nafasi ya pili..Majaliwa na Makamu wa Rais kasi kwenu.

Labda amemsaidia mapema. Maana kwa uoga huo, uwaziri wa nini?
Halafu JPM alivyo....kaenda tena nje ya bunge ili waendelee kurogana
 
Kama ungefuatilia historia yake ya utendaji kazi, wala usingeandika hayo uliyoandika, ila kwakuwa kuna watu kila jiwe alifanyalo lazima mu support, sawa!! Kweli kwa mtizamo wa kibinadamu, hilo lilikuwa na kufanya utengue uteuzi wake?!!
Basically Rais hakuwa na options nyingi na hii ya kutengua ni sahihi tu.

Kile kitendo cha kujiumauma mbele ya camera hakikuwa sawa na wala Rais hawezi kulaumiwa kwa aliyoyafanya. Imagine scenario angesamehewa na akaja kushindwa tena..
 
Back
Top Bottom