Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya jambo la haraka kumuondoa Naibu Waziri wa Madini, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzungumza na kufanya kazi

Haijalishi alikuwa nani wala ni nani mimi naona sawa tu hata wangeondolewa wote maana wao ni kuongea tu maagizo toka juu na kurusha mikono juu mbele ya kamera za luninga lakini matatizo ya wananchi hawatatui kabisa huyu hata kusoma tu kiapo kilichotayarishwa na watu wengine hawezi. Maagizo toka juu atafikishaje kwa wananchi ili wapongeze na kusifia juhudi na mafanikio ya Awamu? Waende wote tubaki na Rais wetu mpendwa na matatizo yetu miaka 5 ijayo!
 
Basically Rais hakuwa na options nyingi na hii ya kutengua ni sahihi tu.

Kile kitendo cha kujiumauma mbele ya camera hakikuwa sawa na wala Rais hawezi kulaumiwa kwa aliyoyafanya. Imagine scenario angesamehewa na akaja kushindwa tena..
Yule mwana mama mbona alikuwa anakoseakosea ila hakuna hata Onyo basi ndio kwanza alimsifia.
 
Ilitakiwa katiba ibadilishwe wapendekezwe na rais ila wapigwe drills bungeni au na kamati maalumu wakivuka vihunzi ndio rais awateue rasm na kula kiapo.
Hapana tufuate Rasimu ya Waryoba yenye maoni ya wananchi yanayotaka Mawaziri wasiwe Wabunge ili kumpa Rais Uwanja mpana wa kuteua Mawaziri bora kutoka kuwa Jamii ya Watanzania milioni 60 waliopo na kuthibitishwa na Bunge. Kulazimisha Rais kuteua Mawaziri 46 toka Wabunge 250 tu matokeo yake ndo hayo wateuliwa wanashindwa hata kuapa na kutenguliwa hadharani na wanaopenyeza ndo wanakuwa mizigo kwa wananchi wakiendeleza umasikini usiyoisha. Aende tu Wabunge hata wakina Kibajaji na Msukuma wa kujaza hiyo nafasi wapo wengi wa Chama chake kuwahi kutokea tangu Uchaguzi wa 1995. Shida iko wapi?
 
Kuna ushirikina unahusika. Huwezi jua yamaa kusogelea tu pale zike irizi za meko zikaanza kumchapa fimbo..maana yake asingeweza kufanya naye kazi.
 

Rasimu ya Warioba Haina tena nafasi. Ajiandae kumjibu Nyerere kwanini alitaka kuuvunja muungano huko sote tutakokwenda
 
Hiyo hali hutokea Watu wengi hata Jacob Zuma akishindwa kusoma na kutamka " in the begining" kuna Mkurugenzi alitamka " mimi ni Mkuruzenzi mpya x2" , Barack Obama nae alishindwa kuapa vizuri hata Magufuli mwenyewe alishindwa kutamka neno " Entrepreneur" hili Rais kateleza ajifunze kutokana na hili kosa!
 
Hawezi kuongea kivipi? Huyu ambaye ameshika nyadhifa byingi kabla hata ya kugombea ubunge bila shaka alikutwa na maswahibu ya kisaikolojia yaliyomfanya atekewe na kushindwa kuzungumza. Rais angetafakari kumpa nafasi nyingine.
Haiwezekani akawa kiongozi mzuri kwa ngazi ya uwaziri kama akipata mshtuko kidogo tu anakengeuka kwa muda mrefu vile.....yaani alipewa muda mrefu kurudia kuapa bado akashindwa...hafai
 
kuchapia ni tofauti na kushindwa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…