Gaijin
JF-Expert Member
- Aug 21, 2007
- 11,812
- 5,298
sidhani kama kukubali mapungufu ni kujidharau.... hebu niambie aliyosema rejia kama kuna issue au ukilinganisha na perforamance za akina charles kitwanga, siphia simba nk??
sidhani kama kukubali mapungufu ni kosa
ila kujiona uko juu ya wenzako ni tatizo kubwa sana... na chracters zake ni nyingi sana, we just need to look in the mirror asubuhi especially after sala ili kupata wisdom zaidi ya kujijua
gaijin... i always respect you and i ahve called you "teacher" many times before but like many of your caliber (and mine), we forget that macho yataona mbali sana, lakini hayawezi kuona hata lips zilivyokaa wala uchafu wa kisamvu wa kwenye meno hadi yaone kioo
Awali ya yote, kukosoa Mawaziri Kivuli wa Chadema hakumaanishi tunakubaliana na Mawaziri wa Kikwete. Tushamwita Ngeleja kilaza, mchemfu, bogus na majina mengine mengi,na wapo waliosema anastahili hata kuchukuliwa hatua za ki-mob fulani hivi. Sophia Simba kwangu naona hana hata hadhi ya kujadiliwa, ni substandard hata kwa standards za serikali ya Kikwete. Ghasia? ....nae ni mule mule tu fungu la kurehemewa.
Tatizo lililopo ni sisi kutaka vigezo vinavyotumika kuwakosoa kina Ngeleja na Ghasia, visitumike kwa wabunge wengine wa Chadema. Tunapowakosoa hao wa CCM huwa "tunajiona tupo juu ya wenzetu" pia, au hii dhana inakuja tunapokosoa wabunge fulani fulani wa CHADEMA? Juzi tu hapo nilimnukuu Lema kuwa kajiita mwenyewe "makini" na ilizua mjadala mrefu, na sikuona pahala kuambizana kuwa tunachofanya ni kujiona "uko juu ya Lema" , wala suala hili sijawahi kulisikia tunapomkosoa Zitto Kabwe!
Mimi nampa respect Regia kama nnavyompa Kiongozi mwengine wa mwananchi, lakini hilo halinifungi kukosoa anayofanya wala kutafakari ingekuwaje angekuwa Waziri wa Vijana na Kazi. Hiyo ni haki yangu kikatiba. Na ukizingatia kuwa tayari mwenyewe alishasema hastahili kupewa Wizara yoyote, utaona kuwa tafakari yangu ya mustakbali wa Taifa iwapo Chadema ingeshinda, inakuwa justified.
I LOVE YOU AND I HOPE THAT YOU STILL LOVE ME AND YOU WILL TAKE A STEP FORWARD TO BUILD AT LEAST ONE LAYER OF SUPPORT TO PEOPLE IN NEED WHILE ADVISING THEM CRITICALLY RATHER THAT JUST CLINGING ON ONE SIDE OF THE LADDER
Amma kwa hili tupo pamoja sana, na nipo tayari kuchukua sio a step tu, bali steps nyingi mno kuhakikisha ninatoa support kwa watu wenye kuhitaji msaada.
*Unaniambia kuwa Mbunge wetu ni miongoni mwa people in need?