Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Hata NSSF, NHIF kuna document lakini bado pesa zinapigwa na ikifika wakati wa uhitaji wa pesa hizo unakuta hamna kitu. Hatuna mifumo na sheria nzuri za kutunza pesa kama hizo; wakati mwingine wakuu wa nchi wanajifanya kukozikopa hali hawarudishi, wengine wanabeba tu kama za kwao. Naamina unakumbuka sakata la waziri fulani kujichotea mamilioni NSSF na wakati mwingine wahuni hao hao wanachota hadi hazina au benki kuu.
Daaah aisee inasikitisha sana mkuu...
 
Sasa kwa sababu za hapo juu unawekeza wakati huna uhakika huko mbele kuna nini?
Mkuu, life is full of uncertainties lakini bado watu wanafanya makubwa wakijua wataishi mpaka miaka 90. Ukiwaza sana kufa kufa utakuwa haufanyi maendeleo mkuu
 
Kwa haya yanayotokea sishauri kabisa...kama unakopesha kwa hela ya kodi yako bado unapigwa penalt ,value retantion fee unategemea nn?

Unaweza weka na bado wakakuletea mambo ya admistration fee na value retantion fee
 
Kwanini wanufaika wasiende mahakamani?
 
Mimi naona tu sasa hivi bodi ya mkopo ijielekeze zaidi kusaidia vijana kuwasomesha kwenye vyuo vya ufundi maana kule malipo ni kidogo then hao vijana wapewe mikopo nafuu ya kuanza miradi then wao wakitaka kujiendeleza vyuo vikuu wajisomeshe maana tayari washapewa msingi wa kujiajiri. Sioni sababu ya kuendelea kuteketeza pesa kuwasomesha watu ili kupata kazi za ofisini wakati hata uhitaji haupo ambapo inapelekea serikali kupugiwa kelele kila siku itoe ajira ambazo nafasi hakuna.
 
Mimi naona tu sasa hivi bodi ya mkopo ijielekeze zaidi kusaidia vijana kuwasomesha kwenye vyuo vya ufundi maana kule malipo ni kidogo then hao vijana wapewe mikopo nafuu ya kuanza miradi then wao wakitaka kujiendeleza vyuo vikuu wajisomeshe maana tayari washapewa msingi wa kujiajiri.
Kama pesa hakuna kwa mtaani kujiajiri napo hakuna maana pia. Just imagine umesomea "Welding and Fabrications" (Fundi mageti na milango) alafu unakuja mtaani na hakuna mtu anayejenga nyumba? Hata kama wanaojenga ni wachache lakini kumbuka huo ujuzi hauna wewe peke yako. Kazi ni za kugombania.

Solutions ya kukosa ajira ni kwamba serikali ipunguze miradi ama speed ya utekelezaji wa miradi, watumishi wapewe posho na allowances kisha wao ndio walete matumizi huku mitaani...
 
Kama ungekuwa unaelewa elimu ya msingi ilifanywa bure kwa sababu ya umaskini uliotopea usingifikiri 8000 kwa mtoto mmoja kwa mwezi ni pesa ndogo kwa mafukara.
 
Kama ungekuwa unaelewa elimu ya msingi ilifanywa bure kwa sababu ya umaskini uliotopea usingifikiri 8000 kwa mtoto mmoja kwa mwezi ni pesa ndogo kwa mafukara.
Kama umasikini ndio hoja ya msingi, mbona elimu ya juu sio bure? Alafu kumbuka kuna wazazi wanasomesha watoto kwenye private schools na bado watoto hao hao wanakuja kuomba mikopo ya elimu wanapohitimu kidato cha sita.
 
Sioni sababu ya kuendelea kuteketeza pesa kuwasomesha watu ili kupata kazi za ofisini wakati hata uhitaji haupo
Hata hizo kazi za kujiajiri kwa sasa uhitaji ni mdogo sana kwa maana waliokuwa wanakula wali mara tano kwa week sasa wakaula mara tatu au mbili tu kwa maana hawana tena pesa kama zamani.
 
Asilimia ngapi ya wanafunzi wanofika elimu ya juu wanaweza kusoma bila mikopo, kutembeza bakuli au kudanga?
Kwa nini HESLEB ihangaike na watu wanaosomesha watoto wao shule binafsi? Kama ni mkopo na sio msaada kuna shida gani mtu yeyote akiomba?
Kama umasikini ndio hoja ya msingi, mbona elimu ya juu sio bure? Alafu kumbuka kuna wazazi wanasomesha watoto kwenye private schools na bado watoto hao hao wanakuja kuomba mikopo ya elimu wanapohitimu kidato cha sita.
 
Kama ungekuwa unaelewa elimu ya msingi ilifanywa bure kwa sababu ya umaskini uliotopea usingifikiri 8000 kwa mtoto mmoja kwa mwezi ni pesa ndogo kwa mafukara.
Vp kwa zile familia zenye uwezo wa kati wa kifedha/ambazo sio fukara zinazoweza kumudu hiyo 8,000 kwa mwezi?
 
Kwa nini HESLEB ihangaike na watu wanaosomesha watoto wao shule binafsi?
Kwani ni wapi nimesema hiyo HESLEB yako badala ya HESLB ihangaike na watu wanaosomesha watoto wao shule binafsi?

Wapo wanaosomesha watoto shule binafsi kisha wanakuja kufilisika huko mbeleni.
 
Kama ni mkopo na sio msaada kuna shida gani mtu yeyote akiomba?
Unampa mkopo mtoto kutoka katika familia masikini, atakuja kuulipa kwa pesa ipi? Ndio maana nimesisitiza suala la account ya malengo
 
Kama lengo ni kusomesha watoto wa maskini, kwanini wasiongeze asilimia flani kidogo kwenye bei za vocha, cement, sukari etc.. ili hicho kinachopatikana kisaidiane na kinachorudishwa na walionufaika ili wengine wapate?

Hapa lengo pia linakua kupunguza mzigo wa wanufaika kurudisha mkopo ukiwa na riba za ajabu ajabu.

Ni mtazamo wangu tu lakini
 
Kama lengo ni kusomesha watoto wa maskini, kwanini wasiongeze asilimia flani kidogo kwenye bei za vocha, cement, sukari etc.. ili hicho kinachopatikana kisaidiane na kinachorudishwa na walionufaika ili wengine wapate?
Mkuu, hauoni kama wakiongeza tena bei za vocha na sukari watakuwa wanamkandamiza tena masikini kwa maana hatoweza kumudu gharama ya bidhaa hizo za msingi?...
 
Mkuu, hauoni kama wakiongeza tena bei za vocha na sukari watakuwa wanamkandamiza tena masikini kwa maana hatoweza kumudu gharama ya bidhaa hizo za msingi?...
Mkuu, na ndio maana nikataja hizo bidhaa za msingi ili kila mtu achangie, nikiwa na maana hiyo rate ya kuchangia itakua as minimal as possiblea.. itakua ngumu mwanzoni( kama ilivyokua imeongezwa ile % ya rea kwenye malipo ya TANESCO) lakini baada ya muda watu watazoea
 
Mkuu, masikini sisi tuna changamoto nyingi sana kuanzia kumudu gharama za elimu, afya, maji safi, etc.

Sasa endapo serikali ikiamua kuongeza percentage katika bidhaa kwa lengo la kukusanya pesa za kutatua changamoto zetu tulio masikini, ifatika wakati kila bidhaa itakuwa aghali za hakuna mtu ataweza kumudu.

Kumbuka elimu ya msingi ni darasa la saba tu mkuu.
 
Back
Top Bottom