Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Kwani Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) haiwezi kuwa na accounts za malengo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza?

Kwaio mwanangu akifeli?? Mana unataja mtiririko tu
Sio kufeli peke yake, anaweza pia kufa. Akishindwa kuendelea na masomo (kufeli au kufa) unarudishiwa pesa zako au unafanya transfer kwa mwingine ambaye bado anasoma.
 
Hapo unataka kuja kuwalaumu bure wakila pesa zako. Huduma za hivyo zipo, mabenki wanazo.
Ikifanywa na HESLB faida inaenda serikalini lakini ikifanywa na banks faida ni ya taasisi binafsi.

Mimi sipo humu kushauri taasisi binafsi mimi ninaongelea mambo ya nchi yangu tu.
 
Habari zenu waungwana wa humu jamiiforums

Kwanini Bodi ya mikopo ya elimu ya juu (HESLB) isianzishe campaign ya kuhamasisha wazazi kuanza kuwalipia watoto wao pesa kidogokidogo katika accounts maalum ya bodi wangali wakiwa bado wanasoma elimu ya msingi (Darasa la Kwanza)?

Jenga picha mtoto anasoma darasa la kwanza kwa miaka saba (7) kisha baada ya kuhitimu anajiunga na kidato cha kwanza mpaka cha nne kwa miaka minne (4) ambacho kwa sehemu kubwa hapa Tanzania ndicho kiwango cha elimu ambacho wanafunzi anaruhusiwa kujiunga na chuo cha ufundi kama amekosa fursa ya kuendelea na Advanced Level.

MATHEMATICAL BREAK DOWN
==========
Idadi ya miezi ndani ya mwaka: 12

Idadi ya miaka atakayosoma mwanafunzi kabla ya kujiunga na elimu ya juu/ufundi: 11

Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa kila mwezi: 8,000/=

Makusanyo ya mwaka mzima kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 8,000 = 96,000

Makusanyo ya miaka 11 kwa mwanafunzi mmoja - 12 x 11 x 8,000 = 1,056,000

Kutokana na takwimu niliyoipata humu humu jamiiforums: "Wanafunzi 947,221 wa darasa la saba kutoka shule 17,051 za Tanzania bara, wanatarajia kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kesho Jumatano na keshokutwa Alhamisi Septemba 12, 2019"

Just assume kwamba wanafunzi walioanza la kwanza ndio haohao waliomaliza darasa la saba na hakuna aliyekufa wala kuacha shule na idadi kamili ni 947,221.

Makadirio ya makusanyo ya mwezi kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 947,221 = 7,577,768,000

Makadirio ya makusanyo ya mwaka mzima kwa wanafunzi wote wa darasa la kwanza - 8,000 x 12 x 947,221 = 90,933,216,000

Kwa makusanyo kama haya kwa mwezi kwa wanafunzi wote takribani shilingi 90,933,216,000 bodi ya mikopo wanaweza kuwekeza hii pesa katika fixed deposits kwenye banks za kibiashara pamoja na kununua "government securities" na kupata returns kubwa na za maana tu kila baada ya miezi sita au mwaka.

Kama familia ina wanafunzi wawili mmoja akifa pesa zinahamia kwenye account ya mdogo/kaka yake.

Ndugu zangu, mimi sio mtaalam sana wa hesabu na uchumi lakini bila shaka idea yangu mtakuwa mmeielewa. Ninawakaribisha kwa michango zaidi pamoja na kukosolewa (Constructive Criticism)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Ni wazo zuri lakini nadhani hilo wazo mzazi mmoja mmoja kwa nafasi yake alifanyie kazi, kwa nini tusihamasishe wazazi kufungua akaunti za malengo za watoto wao na kuweka utaratibu mzuri wa hizo fedha kwenye mabenki badala ya kutegemea bodi ya mikopo
 
Lengo langu mimi ni kwa bodi kukusanya pesa kisha ku-reinvest katika hizo banks au kwa kununua securities kama vile bonds na wao kupata fedha za kujiendesha.
 
Ikifanywa na HESLB faida inaenda serikalini lakini ikifanywa na banks faida ni ya taasisi binafsi.

Mimi sipo humu kushauri taasisi binafsi mimi ninaongelea mambo ya nchi yangu tu.
Nakuelewa mkuu, lakini track record ya haya mashirika ya umma si unaiona, leo wastaafu ambao practically speaking walikuwa "wanaweka" hela waje kutunzwa uzeeni wanasumbuliwa utafikiri wanafanyiwa hisani.
 
Sawa mkuu, I understand your concern.
 
Back
Top Bottom