figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,132
- 64,416
Samia Suluhu Hassan ameutaka Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kuimarisha nafasi ya mabunge katika kushughulikia changamoto za dunia, akisema mvutano wa kisiasa na kijiografia, migogoro na kutokuwa na uhakika kiuchumi vinazidi kuhitaji ushirikiano wa kimataifa.
Ujumbe huo wa Samia ameutoa usiku wa leo Jumatatu Oktoba 5, 2026, kwa njia ya video wakati wa Mkutano wa 153 wa IPU unaofanyika jijini Arusha. Katika ukumbi.
Samia amewakilishwa llive na Mwigulu Nchemba huku yeye akitumia zoomš¤£
Rais Samia amesema kaulimbiu ya mkutano huo ya: "Kuimarisha utawala bora na kuwezesha jamii kupitia ujumuishi, imani na fursa kwa wote," inaendana kwa kiasi kikubwa na hali ya dunia kwa sasa.
Amesema dunia inakabiliwa na sintofahamu za kisiasa na kijiografia, migogoro ya muda mrefu pamoja na changamoto za kijamii na kiuchumi zinazodhoofisha jitihada za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.
MY TAKE
Anaona aibu kwa yaliyotokea 29.10.2025. Na bado..
Wabunge wa Dunia nzima wapo Arusha Tanzania. Na yeye aliwahidi kwamba atafuungua mkutano wao. Lakini kaishia kumtuma Mwigulu. Yeye kaongea kwa zoom.
Kaanza kuishi kama digidigi.. Anaogopa hata kukutana na dunia.. Bila shaka anajutia kilichofanyika.. Atajificha hadi lini?
Swali : Mbona kama afya yake mgogoro?