Kuna Binti mmoja yuko 32yrs old sasa amekata tamaa kabisa namuona anakonda kwa mawazo anadai mwanaume yoyote atakayetokea mbele yake ..anaolewa
Na swali analojiuliza kila leo kwa nini yeye haolewi???
Nimejaribu kuuliza kisa nini hasa anadai umri wake umeenda sana ,anahitaji kuwa na family, anahitaji kupata mtoto
Kwani ukikaa bila kuoa au kuolewa ni tatizo wanajamii ?
Hebu tumsaidie dada huyu kimawazo
Mwambie kuoa/kuolewa ni majaliwa na pengine ni mapenzi ya mtu.
Wapo wengi ambao wanalazimishwa na wengine kuoa au kuolewa..hawataki lakini wapo wale ambao wanalilia kupata mtu wa kumwoa au kuolewa nae na wahapati kama ilivyo kwake..
Umri si tija, hata kibibi kinaweza kuolewa na inategemea na chaguo lake. Iwapo amefikia katika ngazi ya kuhisi anazidi kuzeeka na hapati mtu wa kumweka ndani kama mke, akikurupuka atajikuta pengine hiyo tamaa ya kuolewa ikamletea majuto makuu katika maisha yake yote kwani (i) anaweza kuolewa na mtu ambaye si chaguo sahihi (ii) anaweza kupata mtu ambaye hakujiandaa kuoa lakini kalazimisha na mazingira kwa maana kuwa kampata huyo mwanamke "desperate"
akamtega kwa jambo ambalo litamfanya amwoe tu ikiwa ni pamoja na kumsogezea mpaka "mimba" au mambo yetu haya ya "chienyeji" nk (iii) anaweza kupata mtu ambaye hatashindwa kumchunguza kwa makini mienendo ya maisha yake (wapo wababa wengi wajane hii leo mtaani kwa macho waona afya zao zipo makini lakini walishaathirika na hao wanatafuta watu wa jinsi hii ambao wanakimbilia kuolewa).
Kama alibugi huko nyuma kwa kuchagua chagua, asikurupuke kusema akipatikana yeyote tu atazaa au kulewa nae kama amekaa zaidi ya miaka kumi na kitu tokea awe "mtu mzima" (kufikia ngazi ya usichana), anaweza kujua kuwa maisha yana kurasa nyingi kuliko hata mistari ya maandiko ya kitabu kama "Biblia". Kila kukicha kuna somo lake la kujifunza, na pengine tunajifunza vibaya sana na kujiona kama dunia imetulaani pale tunapoangukia mikononi mwa watu ambao tunapaswa kuishi nao kila siku (mke/mume) ambapo kumbe hawakuwa wa chaguo letu. Hapo tunakuwa tumejifunga, tukitaka kuchomoka, tayari CV inakuwa inavurugika kama si kujiongezea doa....
Wapo wanawake/Wanaume wanaoishi kwa matarajio kuwa yeye ataolewa au kuolewa na mtu wa hadhi, mwanekano, au wa kutoka tabaka fulani kimaisha..jambo hili lina faida na madhara yake ...na moja ya madhara ndi hiyo ya kujikuta unazeekea "nyumbani"(kwa wazazi) na inapotimu wakatin fulani unakuja kubaini kuwa wewe ulipaswa kuoa au kuolewa na yeyote tu kwani hata angekuwa na mali, elimu, wa dini yako, wa kabila lako, wa rangi au sura fulani nk, ndoa huwa ni zaidi ya hayo unayodhania kichwani kwako kwa wakati huo, ndoa ni furaha na Amani .....hivyo visipokuwepo mengine yote utayaona kama "mavi"..
Aombe Mungu, asikate tamaa na kujiachia kama wengine wanavyoonekana mitaani katika zama hizi za ndoa za "copy and paste" staili...eti nioe au niolewe kisa fulani kaoa/kaolewa, mimi nitachekwa.