Kwani Makonda alitenda dhambi ngapi? Mbona anataka kuombewa na kila mtu?

Kiukweli sijawahi kuona mtu anayetaka kuombewa na kila dhehebu, huyu ni wa kwanza , yaani ukivaa msalaba au Baraghashia , au ukishika Tasbih au Rozali basi atakuvamia umuombee!

Kwanini anataka aombewe na kila mtu , alitenda Makosa gani? Je ni mzima au amepata matatizo ya Ubongo , hivi hawa wanadamu anaotaka wamuombee wenyewe ni waadilifu kiasi gani?

Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu , Njia pekee ya kusamehewa na Mungu ni kukiri makosa hadharani na kuwaomba radhi kwa mdomo wako wote uliowakosea , vinginevyo ni sawa kutwanga maji kwenye kinu .

Angalizo kwa viongozi wa dini , na angalizo hili mlizingatie , si kila mtu ni wa kukaribishwa mazabauni , mkiendelea hivi mtakumbana na adhabu ya Mungu waziwazi.

Hata sisi waumini wenu hatutakubali mtudhalilishe kwa kuwakumbatia wachafu na wauaji , TUTAWAONDOA KWENYE HIVYO VYEO KAMA ILIVYOWAHI KUTOKEA HAPO AWALI , JIHESHIMUNI

View attachment 2831702View attachment 2831703
He is Guilty in his Heart
 
Anatafuta uungwaji mkono. Anajua sehemu kubwa ya jamii ilishamkataa sasa anatafuta namna ya kurudi. Hayo maombi ni gia tu anajua watanzania ukiwatajia mambo ya Imani wengi watakuamini.
 
Kiukweli sijawahi kuona mtu anayetaka kuombewa na kila dhehebu, huyu ni wa kwanza , yaani ukivaa msalaba au Baraghashia , au ukishika Tasbih au Rozali basi atakuvamia umuombee!

Kwanini anataka aombewe na kila mtu , alitenda Makosa gani? Je ni mzima au amepata matatizo ya Ubongo , hivi hawa wanadamu anaotaka wamuombee wenyewe ni waadilifu kiasi gani?

Kwa Mujibu wa Maandiko Matakatifu , Njia pekee ya kusamehewa na Mungu ni kukiri makosa hadharani na kuwaomba radhi kwa mdomo wako wote uliowakosea , vinginevyo ni sawa kutwanga maji kwenye kinu .

Angalizo kwa viongozi wa dini , na angalizo hili mlizingatie , si kila mtu ni wa kukaribishwa mazabauni , mkiendelea hivi mtakumbana na adhabu ya Mungu waziwazi.

Hata sisi waumini wenu hatutakubali mtudhalilishe kwa kuwakumbatia wachafu na wauaji , TUTAWAONDOA KWENYE HIVYO VYEO KAMA ILIVYOWAHI KUTOKEA HAPO AWALI , JIHESHIMUNI

View attachment 2831702View attachment 2831703
Damu za watu zinamuandama
 
Hakuna upako bila kufanya toba ya kweli. Na toba ya kweli, kwanza ni kuwapigia magoti uliowadhulumu, ndipo uende nyumbani mwa bwana kuupata utakaso. Vinginevyo, anavyozidi kuwafool viongozi wa dini, anazidi kuchota laana badala ya baraka.
Nyiewatu mnaejifanya watakatifu ndio mawakala wa shetani in advance!.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom