MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,996
Kwa wale wakongwe wa Jamiiforums wananifahamu kuwa mimi ni mmoja wa watu tulikuwa nyuma ya aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Rais Magufuli tokea kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM mpaka alipoitwa na Mwenyezi Mungu. Rais Magufuli amenifundisha mengi sana mazuri na mabaya lakini kikubwa zaidi alichonifundisha ni Ujasiri na kujiamini katika kufanya maamuzi na ameacha mijadala ambayo haitaisha sio nchini pekee bali hata nchi za nje.
Kifo cha Rais Magufuli kama vifo vya wapendwa kwanza kilianza kwa kutia mshangao, baadaye kuhudhunisha na mwishoni kuukubali ukweli na kuangalia ya mbele. Mbele niliyoiangalia ni utawala ujao baada ya Rais Magufuli huku nikijua vizuri siasa za nchi yetu zilivyo.
Baada ya Rais Samia kuingia madarakani na kuanza kupanga ''safu yake'' ya uongozi huku akitoa maagizo ya hapa na pale. Wale tulikuwa tunaitwa MATAGA wakati wa utawala wa Rais Magufuli tukaongezewa jina jingine na kuanza pia kuitwa ''sukuma gang''.
Kwa wasiozijua siasa za nchi hii walituona kama ''laughing stock'' huku wakimhimiza Rais Samia kuhakikisha ''anatufagia'' katika serikali yake na tukilalamika tunaambiwa tuende Chato kwa “mungu” wetu ambaye ameshakufa.
Tulikuwa tunaambiwa “mama” anaponya majeraha...furaha imerejea nchini...”mama” anafuta legasi za mwendazake..
Nilijua ni muda tu hizi pongezi kwa Rais Samia zikiambatana na kicheko, kejeli na matusi kwa wanawaita MATAGA na sukuma gang zitapotea kwa sababu hawajui kitakachowakuta mbele ya safari yao ya kisiasa!
Miezi minne baada ya kifo cha Rais Magufuli wale waliokuwa wanatucheka na kutukejeli kwa sasa wanalia na hata yale majina ''waliotubatiza'' kwa sasa wameyasahau na yamepotea kwa haraka sana!
Waliokuwa wanatucheka na kutukejeli mpaka wakaanza kuchora katuni za kejeli lakini hawakujua kama ''atakapotumaliza sisi'' basi watafuata wao! Wahenga walisema, kulia kupokezana!
Sisi kwa sasa hatucheki wala kukejeli bali tunashangaa na kuuangalia huu mchezo wa kisiasa mpaka dakika za mwisho!
Kwa sasa najiuliza, kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''MATAGA'' na ''sukuma gang''?
Siasa za nchi hii zinakwenda kwa haraka sana!
Tusijekushangaa sana watakapoanza kumkumbuka Marehemu Magufuli huko mbele ya safari ya kisiasa!