Kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''sukuma gang''; Je, kwa sasa ni zamu ya waliokuwa wanafurahia na kufanya sherehe!

Kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''sukuma gang''; Je, kwa sasa ni zamu ya waliokuwa wanafurahia na kufanya sherehe!

Mkuu, kwa hilo hauko peke yako, tuko wengi na hatutorudi nyuma. Hata tukikosa mengine yote, basi tutamuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa kusimamia ujasiri aliotufundisha na kujiamini kuwa tunaweza.
Rest in peace uncle Magu, till we meet again [emoji1548]
Acha nilie kidogo kupunguza maumivu. Enzi za mwendazake 5000 ilinunua unit 41.3. Leo napata unit 21 tu.

Magufuli kwanini umekufa?
 
Huu uhuru tulionao humu JF inapelekea baadhi yenu kuandika pumba na mashudu tupu

Msihangaike na kupambana na legacy ya Magufuli, huyu mtu katokea kukubalika sana kwa Watanzania walio wengi,,, aliyoyafanya kwa miaka yake michache yameonesha kiwango cha juu cha upendo, uzalendo kwa kupigania maslahi ya Taifa hili ili kila mmoja anufaike

Mfano mdogo tu kaondolewa Kalemani na kuwekwa January Watanzania walio wengi wameonekana kutokufurahishwa na hili ukizingatia miezi michache tu mbele tumeanza kupata shida ya umeme

Mwisho kabisa, Mamá Samia na Makamu wake Dr Mpango ni zao la Magu
 
Mimi siwezi kumkumbuka magufuli kwa roho yake mbaya huyo mama hata aboronge vipi hatofikia nusu ya magu
 
Hii ya kusema Magufuli alikubalika na Watanzania wengi, ni kauli ya kipuuzi isuyokuwa na uthibitisho wowote. Yawezekana alikubalika na watu wengi hapo kwenye jamii yako, siyo kwa Watanzania wengi. Yapo maeneo mengi na wapo watu wengi ambao wanamwona Magufuli ilikuwa ni laana kwa Taifa.

Wewe ni mpuuzi sana, nakuona kila siku unamtukana Magufuli na wasukuma hata na ID yako ya zamani (Bams).

Magufuli alikubalika na wengi kwa kazi zake, maskini, makabila yote, watu wote.

Mwambie Mama yako afanye kazi kubwa kuliko Magufuli, atapendwa na wengi.

Wewe mpuuzi unaweza kushinda uchaguzi wowote bila hao unaowatukana kila siku.
 
Wewe ni mpuuzi sana, nakuona kila siku unamtukana Magufuli na wasukuma hata na ID yako ya zamani (Bams).

Magufuli alikubalika na wengi kwa kazi zake, maskini, makabila yote, watu wote.

Mwambie Mama yako afanye kazi kubwa kuliko Magufuli, atapendwa na wengi.

Wewe mpuuzi unaweza kushinda uchaguzi wowote bila hao unaowatukana kila siku.
Kwa kifupi, jamaa alikubalika na watu WAJINGA na WAPUMBAVU TU.
 
Kwa wale wakongwe wa Jamiiforums wananifahamu kuwa mimi ni mmoja wa watu tulikuwa nyuma ya aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Rais Magufuli tokea kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM mpaka alipoitwa na Mwenyezi Mungu. Rais Magufuli amenifundisha mengi sana mazuri na mabaya lakini kikubwa zaidi alichonifundisha ni Ujasiri na kujiamini katika kufanya maamuzi na ameacha mijadala ambayo haitaisha sio nchini pekee bali hata nchi za nje.

Kifo cha Rais Magufuli kama vifo vya wapendwa kwanza kilianza kwa kutia mshangao, baadaye kuhudhunisha na mwishoni kuukubali ukweli na kuangalia ya mbele. Mbele niliyoiangalia ni utawala ujao baada ya Rais Magufuli huku nikijua vizuri siasa za nchi yetu zilivyo.

Baada ya Rais Samia kuingia madarakani na kuanza kupanga ''safu yake'' ya uongozi huku akitoa maagizo ya hapa na pale. Wale tulikuwa tunaitwa MATAGA wakati wa utawala wa Rais Magufuli tukaongezewa jina jingine na kuanza pia kuitwa ''sukuma gang''.

Kwa wasiozijua siasa za nchi hii walituona kama ''laughing stock'' huku wakimhimiza Rais Samia kuhakikisha ''anatufagia'' katika serikali yake na tukilalamika tunaambiwa tuende Chato kwa “mungu” wetu ambaye ameshakufa.

Tulikuwa tunaambiwa “mama” anaponya majeraha...furaha imerejea nchini...”mama” anafuta legasi za mwendazake..

Nilijua ni muda tu hizi pongezi kwa Rais Samia zikiambatana na kicheko, kejeli na matusi kwa wanawaita MATAGA na sukuma gang zitapotea kwa sababu hawajui kitakachowakuta mbele ya safari yao ya kisiasa!

Miezi minne baada ya kifo cha Rais Magufuli wale waliokuwa wanatucheka na kutukejeli kwa sasa wanalia na hata yale majina ''waliotubatiza'' kwa sasa wameyasahau na yamepotea kwa haraka sana!

Waliokuwa wanatucheka na kutukejeli mpaka wakaanza kuchora katuni za kejeli lakini hawakujua kama ''atakapotumaliza sisi'' basi watafuata wao! Wahenga walisema, kulia kupokezana!

Sisi kwa sasa hatucheki wala kukejeli bali tunashangaa na kuuangalia huu mchezo wa kisiasa mpaka dakika za mwisho!

Kwa sasa najiuliza, kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''MATAGA'' na ''sukuma gang''?

Siasa za nchi hii zinakwenda kwa haraka sana!

Tusijekushangaa sana watakapoanza kumkumbuka Marehemu Magufuli huko mbele ya safari ya kisiasa!

View attachment 1870346
Ila Magufuli aliwadanganya sana nyie wapambe wake , yaani aliwaaminisha kwamba katiba si lolote na mkaamini , ilibaki kidogo sana muanze kumuabudu kuliko Mungu
 
Kwa kifupi, jamaa alikubalika na watu WAJINGA na WAPUMBAVU TU.

Nyie wenye akili mnashindwa kutupa Maji, umeme, kuthibiti mfumuko wa bei, mbolea, vifaa vya ujenzi, wapi mmefanikiwa hata kidogo tu.

Maisha ya watu wa kawaida yamekuwa magumu sana.

Pumbavu sana wewe na genge lako.
 
Nyie wenye akili mnashindwa kutupa Maji, umeme, kuthibiti mfumuko wa bei.

Maisha ya watu wa kawaida yamekuwa magumu sana.

Pumbavu sana wewe na genge lako.
Genge gani tenaa!? Mimi ni C H A D E M A . mlitaka nchi ya kijani. Haya sasa, mmepewa na magugu maji..
 
Unapigania nini? Maisha mazuri, sera rafiki kusaidia Watanzania wengi, wote au genge dogo.
Sorry Brother! Najua sisi sote ni Watanzania[emoji1241] lengo letu ni moja.. Naweza kuhisi maumivu unayopitia. Ila yote heri, Tanzania [emoji1241] itakuja kuwa nchi tunayoitaka.
 
Sorry Brother! Najua sisi sote ni Watanzania[emoji1241] lengo letu ni moja.. Naweza kuhisi maumivu unayopitia. Ila yote heri, Tanzania [emoji1241] itakuja kuwa nchi tunayoitaka.

Maumivu yangu ni kwa Watanzania wengi. Maisha yao, kuwasaidia wainuke, wasimame.

Nchi iwe na sera, uongozi, utawala, mazingira, yatakao saidia wengi.
 
Back
Top Bottom