Kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''sukuma gang''; Je, kwa sasa ni zamu ya waliokuwa wanafurahia na kufanya sherehe!

Sifurahii fikra za kufanya chochote kwa kuegemea ukabila.

Lakini nawe umekuwa miongoni mwa wajinga kiasi cha kushindwa kujua hata takwimu. Hiyo 25% kuwa ni wasukuma, unaota au umedanganywa na wajinga wenzako, na wewe kwa ujinga ukainuka nayo hivyo hivyo bila ya kuhakikisha.

WIKIPEDIA
The Sukuma are a Bantu ethnic group from the southeastern African Great Lakes region. They are the largest ethnic group in Tanzania, with an estimated 10 million members or 16 percent of the country's total population. Sukuma means "north" and refers to "people of the north." The Sukuma refer to themselves as Wasukuma (plural) and Msukuma (singular).
Wikipedia ? .... You are indeed a clown
 
Mkuu, kwa hilo hauko peke yako, tuko wengi na hatutorudi nyuma. Hata tukikosa mengine yote, basi tutamuenzi Hayati Rais John Pombe Magufuli kwa kusimamia ujasiri aliotufundisha na kujiamini kuwa tunaweza.
Rest in peace uncle Magu, till we meet again 💪🏿
Jamani ujasiri tu hautoshi kwenye utawala bora
 
Kumekuwa na vita Kali sana inayoendelea mpaka sasa Kati ya wafuasi wa Hayati Dr. Magufuli na wafuasi wa Rais wa sasa Mh. Mama Samia Suluhu huku wafuasi wa Mama Samia na wale wote ambao hawakuipenda Serikali ya JPM ukiwemo Upinzani, wanawaita wafuasi wa hayati JPM jina la "Sukuma Gang".

Tanzania ni nchi ya kipekee barani Afrika ambayo imejengwa kwa misingi mizuri ya kutokubaguana kimakabila. Lakini mpaka sasa imejengwa taswira kuonesha kwamba wasukuma ndio watu ambao hawakubaliani na mwenendo mzima wa serikali ya awamu ya 6 kitu ambacho si cha kweli kwasababu wafuasi wa JPM sio Wasukuma pekee wapo maeneo mengi ya Tanzania.

Jina la 'Sukuma Gang' likome! Ni bora kuita wafuasi wa serikali ya awamu ya tano kuliko kutaja kabila. Huu Upuuzi unatoka wapi kwa watu waliofanikiwa kuondoa ubaguzi wa kikabila?

Kaka Aisee nimecheka sanaaa
Eti jina La Sukuma gang likome...[emoji1][emoji1][emoji1][emoji851][emoji23]
Umenikumbusha Supika alivyosemaga Mwenzako kama halitaki jina Kwanini Uendee Kumuita...Nadhani alikuwa akimwanbia cAG..[emoji41][emoji23]
 
Kwa wale wakongwe wa Jamiiforums wananifahamu kuwa mimi ni mmoja wa watu tulikuwa nyuma ya aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Rais Magufuli tokea kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM mpaka alipoitwa na Mwenyezi Mungu. Rais Magufuli amenifundisha mengi sana mazuri na mabaya lakini kikubwa zaidi alichonifundisha ni Ujasiri na kujiamini katika kufanya maamuzi na ameacha mijadala ambayo haitaisha sio nchini pekee bali hata nchi za nje.

Kifo cha Rais Magufuli kama vifo vya wapendwa kwanza kilianza kwa kutia mshangao, baadaye kuhudhunisha na mwishoni kuukubali ukweli na kuangalia ya mbele. Mbele niliyoiangalia ni utawala ujao baada ya Rais Magufuli huku nikijua vizuri siasa za nchi yetu zilivyo.

Baada ya Rais Samia kuingia madarakani na kuanza kupanga ''safu yake'' ya uongozi huku akitoa maagizo ya hapa na pale. Wale tulikuwa tunaitwa MATAGA wakati wa utawala wa Rais Magufuli tukaongezewa jina jingine na kuanza pia kuitwa ''sukuma gang''.

Kwa wasiozijua siasa za nchi hii walituona kama ''laughing stock'' huku wakimhimiza Rais Samia kuhakikisha ''anatufagia'' katika serikali yake na tukilalamika tunaambiwa tuende Chato kwa “mungu” wetu ambaye ameshakufa.

Tulikuwa tunaambiwa “mama” anaponya majeraha...furaha imerejea nchini...”mama” anafuta legasi za mwendazake..

Nilijua ni muda tu hizi pongezi kwa Rais Samia zikiambatana na kicheko, kejeli na matusi kwa wanawaita MATAGA na sukuma gang zitapotea kwa sababu hawajui kitakachowakuta mbele ya safari yao ya kisiasa!

Miezi minne baada ya kifo cha Rais Magufuli wale waliokuwa wanatucheka na kutukejeli kwa sasa wanalia na hata yale majina ''waliotubatiza'' kwa sasa wameyasahau na yamepotea kwa haraka sana!

Waliokuwa wanatucheka na kutukejeli mpaka wakaanza kuchora katuni za kejeli lakini hawakujua kama ''atakapotumaliza sisi'' basi watafuata wao! Wahenga walisema, kulia kupokezana!

Sisi kwa sasa hatucheki wala kukejeli bali tunashangaa na kuuangalia huu mchezo wa kisiasa mpaka dakika za mwisho!

Kwa sasa najiuliza, kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''MATAGA'' na ''sukuma gang''?

Siasa za nchi hii zinakwenda kwa haraka sana!

Tusijekushangaa sana watakapoanza kumkumbuka Marehemu Magufuli huko mbele ya safari ya kisiasa!

View attachment 1870346
Yaani wewe ni kati ya waliokuwa wanamuabudu Jiwe , sijui hali yako kwa sasa ikoje wallah tena !!
 
Pamoja na kuitwa "Sukuma gang" sisi ndio wengi, uchaguzi wa haki wa kidemokrasia nchi ni yetu. Alitupigania wote ila tu watu wazuri hawaishi mda mrefu.
 
Kwa wale wakongwe wa Jamiiforums wananifahamu kuwa mimi ni mmoja wa watu tulikuwa nyuma ya aliyekuwa Rais wa Tanzania wa Awamu ya Tano, Rais Magufuli tokea kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM mpaka alipoitwa na Mwenyezi Mungu. Rais Magufuli amenifundisha mengi sana mazuri na mabaya lakini kikubwa zaidi alichonifundisha ni Ujasiri na kujiamini katika kufanya maamuzi na ameacha mijadala ambayo haitaisha sio nchini pekee bali hata nchi za nje.

Kifo cha Rais Magufuli kama vifo vya wapendwa kwanza kilianza kwa kutia mshangao, baadaye kuhudhunisha na mwishoni kuukubali ukweli na kuangalia ya mbele. Mbele niliyoiangalia ni utawala ujao baada ya Rais Magufuli huku nikijua vizuri siasa za nchi yetu zilivyo.

Baada ya Rais Samia kuingia madarakani na kuanza kupanga ''safu yake'' ya uongozi huku akitoa maagizo ya hapa na pale. Wale tulikuwa tunaitwa MATAGA wakati wa utawala wa Rais Magufuli tukaongezewa jina jingine na kuanza pia kuitwa ''sukuma gang''.

Kwa wasiozijua siasa za nchi hii walituona kama ''laughing stock'' huku wakimhimiza Rais Samia kuhakikisha ''anatufagia'' katika serikali yake na tukilalamika tunaambiwa tuende Chato kwa “mungu” wetu ambaye ameshakufa.

Tulikuwa tunaambiwa “mama” anaponya majeraha...furaha imerejea nchini...”mama” anafuta legasi za mwendazake..

Nilijua ni muda tu hizi pongezi kwa Rais Samia zikiambatana na kicheko, kejeli na matusi kwa wanawaita MATAGA na sukuma gang zitapotea kwa sababu hawajui kitakachowakuta mbele ya safari yao ya kisiasa!

Miezi minne baada ya kifo cha Rais Magufuli wale waliokuwa wanatucheka na kutukejeli kwa sasa wanalia na hata yale majina ''waliotubatiza'' kwa sasa wameyasahau na yamepotea kwa haraka sana!

Waliokuwa wanatucheka na kutukejeli mpaka wakaanza kuchora katuni za kejeli lakini hawakujua kama ''atakapotumaliza sisi'' basi watafuata wao! Wahenga walisema, kulia kupokezana!

Sisi kwa sasa hatucheki wala kukejeli bali tunashangaa na kuuangalia huu mchezo wa kisiasa mpaka dakika za mwisho!

Kwa sasa najiuliza, kwani ''Mama'' amemalizana na sisi tuliokuwa tunaitwa ''MATAGA'' na ''sukuma gang''?

Siasa za nchi hii zinakwenda kwa haraka sana!

Tusijekushangaa sana watakapoanza kumkumbuka Marehemu Magufuli huko mbele ya safari ya kisiasa!

View attachment 1870346
🥶🥶
 
Laa 'Ilaaha 'Illa Allaahu Wahdahu La Shareeka Lahu, Lahul Mulku Wa Lahul Hamdu Yuhyi Wa Yumeet Wahuwa A'la Kulli Shay'iin Qadeer.
 
Kwa kuogopa kulia tena, sisi tulioitwa sukuma gang hatucheki wala kukejeli bali tunaangalia mchezo unavyochezwa!
Shida ni kwamba, walifikiri sisi ni bendera kufuata upepo. Hawakujua Juu ya Magufuli ulikuwa ni Utambuzi uliovuka upeo wao wafuata upepo.
Acha tuwaachie uwanja waliouzoea tuwe watazamaji, na Tutaona mengi bado.
 
Back
Top Bottom