Bahati wewe ndio hufuatilii. Wanaohangaika mitandaoni ni ninyi. Kila mmoja kavimba macho na kushupaza shingo. Kila sekunde mnapandiza uzi wa kuwatukana. Sisi CCM haituhusu! Kwani kufukuzana mmeanza leo? Na nakuhakikishia kama alivyosema Mwl. Nyerere ya kwamba ukila nyama ya binadamu huwezi kuacha, tunatarajia mtafukuzana sana. Kila mtu kwa wakati wake.
Wakati huhuo, Katibu Mkuu wa CCM anawaambia wanachama na viongozi wa CCM wajipange kwa uchaguzi wa 2025, ninyi mnafukuzana na kukejeliana. Uchaguzi ukifika, nani kwenye akili timamu anaweza kuwapa kura? Endeleeni kuwatukana. Sisi tupo tunaijenga CCM yetu kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025!