Kwanini Addiction ni ngumu kuacha hata kama unajua madhara yake

Kwanini Addiction ni ngumu kuacha hata kama unajua madhara yake

Nomadix

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
2,411
Reaction score
6,646
Habari zenu wakuu
Mwaka unaenda kasi sana njaanuary hioo inaishia
...
Kuna mambo mengi ambayo unakuta mtu anajua kabisa madhara yake au kama hajui hata akishaambiwa madhara yake bado haachi, mfano mambo kama:

-Kujichua, wapo wanaodai inafaida ili wajifariji lakini ukweli unajulikana ina madhara makubwa kiroho,kiafya, na kisaikolojia, licha ya kujua hivyo wanaofanya hivyo hawaachi. kwanini?

-unywaji wa pombe, wapo wanatumia pombe na vilevi wanajua madhara yake lakini inakuwa ngumu kuacha, wengine wanajua ila wanabisha licha ya makampuni kusisitiza kunywa kistaarabu wanakunywa kupitiliza wanapata madhara (mf. kupoteza pesa nyingi,hangover kali,kichwa kuuma,matatizo ya moyo,wengine wanaharisha sana) ila hawaachi

-Kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke/mume wa mtu
Madhara yake sote tunayafahamu na pengine tunajutia hii tabia lakini sasa kuacha huwa sio rahisi why?

-Kuwa na wapenzi wengi na kufanya ngono zembe
magonjwa ya zinaa,UTI sugu madhara mengine tunayajua
Kwanini bado inakuwa ngumu kuacha hizi tabia na zinginezo japo madhara tunayajua/yanatupata?
 
Huwa kuna maumivu unapitia ukijaribu kuacha,

Sio lazima yawe maumivu ya kimwili, yanaweza kuwa ya kiakili, hisia, n.k.

kuacha addiction inabidi usuke upya ratiba zako, kubadili mazingira, mtindo wa maisha, n.k. sio kitu kidogo.

Mlevi wa pombe huwa kuna arosto anaipata akitaka kuiacha koo linawaka moto hii hali inaweza kudumu mwezi, wengi hawamalizi wiki, inakuwa ngumu kuwaacha marafiki zake wanaokunya pamoja, inakuwa ngumu kutafuta vya kufanya mda aliozoea kunywa, inakuwa ngumu kubadili mtindo wa maisha, n.k.

Mlevi wa data kuna maumivu akipoteza simu anapitia maumivu ya kisaikolojia yupo tayari kusafisha chumba kizima aipate simu yake aliyosahau alipoweka, inakuwa ngumu kuacha circle yake ya mtandaoni aidha watu anaochat nao, watu maarufu anaowafatilia,n.k., inakuwa ngumu kutafuta vitu vingine vya kufanya, n.k. wale mazombi wa games ndio balaa, ukimnyanganya simu anaweza kukutukana hata kama mdogo.
 
Back
Top Bottom