Kwanini ajali nyingi zinazotokea mataa Mbezi Beach huwa zinaua tu Vijana walioanza kufanikiwa kimaisha na kiutajiri?

Kwanini ajali nyingi zinazotokea mataa Mbezi Beach huwa zinaua tu Vijana walioanza kufanikiwa kimaisha na kiutajiri?

Karibia 85% ya Ajali mbaya zinazotokea hapo Mataa ya Mbezi Beach Jirani na Kanisa la KKKT huwa zinachukua tu Uhai ( Zinaua ) Vijana ambao Wameshaanza Kutusua ( Kutoka ) Kimaisha.

Na kwanini zote ziwe ni eneo hilo hilo na hapo hapo Mataa upande wa Barabara ya Kuelekea Rainbow au pale kwa CDF Mstaafu Rubani Mahiri wa Ndege Vita Jenerali Robert Mboma tu?

Kuhusiana na hili nililoliweka hapa nitapenda nitapenda nipate Majibu ya Kisayansi ( Kitaalam ) na yale ya Imani zetu za Uswahili Uswahili / Uenyeji Uenyeji kwani huenda tukapa Suluhisho juu ya eneo hilo ( hili ) kuwa Machinjioni kwa Vijana wanaoanza Kutajirika na Kufanikiwa Kimaisha.

Cc' Bujibuji Simba Nyamaume na nategemea sana Uchambuzi wako kwani 95% ya Maisha yako na hata Kulewa Kwako huwa ni eneo hilo hilo tena 'Sometimes' ukiwa na Ndugu zangu ( wa Kizanaki ) na Mademu zenu Wasioeleweka.
My experience as hiyo ni njia yangu! Watu wengi wanaopata ajali eneo hilo huwa wamekunywa na pia ajali nyingi huwa late night.
Ntakupa mfano: last week jumamos going to jumapili nilikuwa na flight ya mwanza ya saa kumi na moja asubuh… nilitoka home saa 9 tulipofika hapo njia panda ya tank bovu tulikuta ajali ya fuso na paso ya silver, too bad wa kwenye paso alikuwa anasalimiana na Bwana Yesu ( mliopita hapo mida hiyo nadhani mliona ajali husika) As usual chanzo cha ajali was ulevi!
 
Nakubaliana nawe 100% kwa hili kwani Yule Tajiri wa Kihaya alikufa hapo hapo akiwa Chakari na Kidemu ndani na huyu Dogo wa Juzi ( Mchagga ) aliyesafirishwa Jana na anazikwa leo nae alikuwa Chakari akitokea katika Harusi.

Na kwa Spidi Kali aliyokuwa nayo walipofika SUPA Lugalo Mdogo wake alimtaka ampishe ili aendeshe Yeye ila Marehemu akakataa.

Mdogo Mtu alipoona Kaka yake ( Marehemu ) hasikii na anaenda Spidi akaomba ashuke Kwa Komba ili atembee kwa Miguu hadi Kwao na amuache Kaka yake Cha Pombe na Mbishi aendeshe peke yake.

Aliposhuka tu akiwa anatembea pembezoni haikupita hata Dakika 5 akasikia Mlio Mkubwa hapo Mataa ambapo Lori aina ya Fuso ilikuwa imeshakokiwa na Kuigonga Gari ya Kaka yake ( Marehemu ) na alipowahi eneo la Tukio kuona kumetokea nini akakuta ni Gari ya Kaka yake imegongwa upande ule ule wake akiwa Kaumia vibaya ( ila Madereva Boda Boda wa pale wakimchomolea Simu na Wallet yake ) na kumuwahisha Lugalo Hospital ambapo alifia Njiani na sasa kuwa ni Historia.
Noma Sana jamaa tumemuaga majuz hapo mbez beach Mungu ampe pumziko jema E ...Yule wife sio kidemu mkuu
 
Daaaah mwamba umeua aisee
Brother kama tuna magari na tunapenda starehe,show off kwamba nadrive nalo ni janga linalouwa vijana wengi.
Ni bora kumhire dereva akuendeshe hadi nyumbani na umkodie boda asepe zake home yake.
 
My experience as hiyo ni njia yangu! Watu wengi wanaopata ajali eneo hilo huwa wamekunywa na pia ajali nyingi huwa late night.
Ntakupa mfano: last week jumamos going to jumapili nilikuwa na flight ya mwanza ya saa kumi na moja asubuh… nilitoka home saa 9 tulipofika hapo njia panda ya tank bovu tulikuta ajali ya fuso na paso ya silver, too bad wa kwenye paso alikuwa anasalimiana na Bwana Yesu ( mliopita hapo mida hiyo nadhani mliona ajali husika) As usual chanzo cha ajali was ulevi!
Sure.

Kipande ambacho kimekula roho za watu wengi ( si madereva wa malori, baiskeli, pikipiki, bajaji, gari ndogo, Watembea kwa miguu nk.) bila kujali usiku au mchana ni kwenye sehemu ya karibu na ZEBRA ya kuingia mabibo hostel.

Na nyingi zinahusisha kutoka ubongo.
 
Mshana Jr pandisha ule uzi wako wa 2014 wa Jems mtoto wa Dando.

The same area more and more wasanii na vijana wengi wameishia pale.

Ni eneo korofi, au halipendi pombe au pana yao waliyoweka
Mtoto wa Dando alipatia ajali kijitonyama
 
Back
Top Bottom