Kwanini Aluminium furnitures ni ghali sana?

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Nimejiuliza swali hilo kila mara.
Nini kinasababisha Aluminium furnitures kuwa ghali sana.
My observation ni kuwa they are not labour intensive...ni kata unganisha kirahisi and all is done!
Au. Material yanyewe ndiyo ghali?
 
Wanasema dirisha linalouzwa 230,000 materials zake zinagharimu kama 50,000 tu au pungufu. Ni upigaji na kwasababu bei iliokuwepo imezoeleka na kukubalika.
 
Sababu ni ujinga wa walaji au ujinga wa wateja ndio maana mafundi wanatumia fursa hiyo kuwapiga bei kubwa wateja. Kama una mradi wako wa aluminum furniture zama sokoni mwenyewe angalia bei za material ya aluminium na vioo kwa bei ya jumla na uvinunue kutokana na mahitaji kwa kumtumia mtaalamu unamlipa kidogo halafu tafuta fundi yeye kazi yake ni kutengeneza tu.
 
Mkuu si kweli kwamba dirisha linalouzwa 230000 material yake 50000 ingekuwa hivyo basi mafundi wangekuwa matajiri sana.
Nimefanya hii biashara naijua tena kipindi hicho square meter tulikuwa tunapiga 150000 na material zilikuwa cheap zaidi ya sasa lakini bado isingewezekana dirisha la 230000 material kuwa 50000.
 
Kitu kinachochimbwa mamia ya mita chini ya ardhi, ukakiyeyushe, tutengeneze umbo lake ni lazima kiwe ghali kuliko mbao ambazo zipo juu ya ardhi na uandaaji wake ni wa haraka
aluminum ni cheap kuliko mbao hasa madirisha. Ukiweka madirisha ya mbao kwa mfano mninga itakuwa ghali zaidi ya aluminum. Labda upvc ndiyo inaweza kuwa ghali zaidi na sijui kwanini materials zake ni ghali wakati ni maplastic fulani
 
Hizo mbao zenyewe unaensa huko vijijini kumejaa miti lakini Mlango unaambiwa bei laki 2 na 50. Sasa si bora Aluminium laki 3 na 50 unachapa. Hamsumbuani usafirina mlango una shine
 
Sababu ni ujinga wa walaji au ujinga wa wateja ndio maana mafundi wanatumia fursa hiyo kuwapiga bei kubwa wateja. Kama una mradi wako wa aluminum furniture zama sokoni mwenyewe angalia bei za material ya aluminium na vioo kwa bei ya jumla na uvinunue kutokana na mahitaji kwa kumtumia mtaalamu unamlipa kidogo halafu tafuta fundi yeye kazi yake ni kutengeneza tu.
Mmh.....haya ndio yale ya kufayatua Tofali mwenyewe kwa kuogopa kununua. Unaokoa kidogo sana na unapoteza muda mwingi
 
Nimejiuliza swali hilo kila mara.
Nini kinasababisha Aluminium furnitures kuwa ghali sana.
My observation ni kuwa they are not labour intensive...ni kata unganisha kirahisi and all is done!
Au. Material yanyewe ndiyo ghali?
Rahisi sana mafundi wanajiona profishenal sana
 
aluminum ni cheap kuliko mbao hasa madirisha. Ukiweka madirisha ya mbao kwa mfano mninga itakuwa ghali zaidi ya aluminum. Labda upvc ndiyo inaweza kuwa ghali zaidi na sijui kwanini materials zake ni ghali wakati ni maplastic fulani
Hizo material zinaagizwa kutoka Ulaya na China, kodi kibao.

Upvc na aluminium zinapendeza sana. Nyumba ikipigwa inavutia mno
 
Rahisi sana mafundi wanajiona profishenal sana
Si kweli watu mnaongea tu. Kutengeneza dirisha la aluminum unahitaji materials hizi: cill, jam, mosquito, lock, rollers, rubber ya vioo, ruber ya wavu wa mosquito, kioo, mosquito net, rivert, screws.
Hapo hujaweka umeme na labor charge na umeme. Ninachoweza kukwambia, kama mtu akikwambia gharama labda 3.5, kama kazi ingeenda sawa hapo anaweza kupata faida ya lak 4-8.
Hii kazi nimeifanya naijua na nina mpango wa kurudi baada ya kuwa nje ya game kwa miaka kama nane.
 
Mkuu si kweli kwamba dirisha linalouzwa 230000 material yake 50000 ingekuwa hivyo basi mafundi wangekuwa matajiri sana.
Nimefanya hii biashara naijua tena kipindi hicho square meter tulikuwa tunapiga 150000 na material zilikuwa cheap zaidi ya sasa lakini bado isingewezekana dirisha la 230000 material kuwa 50000.
Milango ya bafuni na vyooni inatakiwa kuwa na vipimo gani ili iwe migumu kuharibika
 
Back
Top Bottom