Kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani?

Baki hivyo wakati akina Manji mabilionea walikuwa na maeneo hadi kuwa diwani wa Mbagala kuu.
Mabilionea wana maeneo Mbagala kwa ajili ya biashara zao (warehouses, factories & yards) lakini sio kwa makazi yao.

Halafu huko Mbagala cheap labour ni wengi na ardhi ni bei rahisi ndo maana wanakuja kuwekeza

Baada ya hapo wanarudi zao Masaki, Mbezi Beach, Oysterbay, Mikocheni, Mbweni, Madale kupumzika na familia zao
 

nchi hizo zina utajiri mkubwa rasilimali Mafuta ila bado Hizo nchi hazina maendeleo kuzizidi nchi ambazo sio za kiislamu.

nchi zinazoongoza kwa maendeleo na utajiri duniani kwa lugha nyingine nchi zenye uchumi mkubwa zinaitwa G7 countries

hakuna nchi hata moja katika hizo ulizozitaja ambayo imefikia level ya kuingia G7 countries

hizo nchi ukizilinganisha na Tanzania utaona zina maendeleo maana zinatuzidi , ni sawa na Burundi wanaiona Tanzania ina maendeleo. ila kwenye level za kidunia hizo nchi hazina maendeleo ya kuzizidi non muslim countries.

nitajie nchi gani hapo ina maendeleo kuzidi G7 countries?
 
Sasa mkuu wazaramo kupiga ngoma kila jumapili ndio ifanye nyumba zisipangike.?? Naona pamoja na yote serikali pia ya kulaumiwa kwa hili linalo endelea
 
Sasa mkuu wazaramo kupiga ngoma kila jumapili ndio ifanye nyumba zisipangike.?? Naona pamoja na yote serikali pia ya kulaumiwa kwa hili linalo endelea

watu wenye uwezo huwezi wapangisha sehemu kwenye ngoma ngoma na makelele..

mbagala yote sizani kama kuna nyumba ya kuishi ya kufikia Kodi laki 4 kwa mwezi
 
Sasa mkuu wazaramo kupiga ngoma kila jumapili ndio ifanye nyumba zisipangike.?? Naona pamoja na yote serikali pia ya kulaumiwa kwa hili linalo endelea
Hawa jamaa walion'gan'gania mbagala sio PA kuishi Kuna engo wako sahihi ila wamejaa mihemko ndo mana hoja haionekani. Mm binafs mbagala nataka kuhama Lakin hawa watu wa kusaidiw sio kutengwa. Ni binadam pia, tatizo Wana Mila zinazopingana na maendeleo
 
🤣🤣🤣 sawa mkuu
 
Maendeleo nini? Naomba kujua hilo
 
Kwanza kabisa mnatakiwa mjue mbagala ni kubwa, si kila matatizo unayosikia mbagala basi ni mbagala yote, kuna maeneo mbagala watu wanaishi zao kwa utulivu tu
 
watu wenye uwezo huwezi wapangisha sehemu kwenye ngoma ngoma na makelele..

mbagala yote sizani kama kuna nyumba ya kuishi ya kufikia Kodi laki 4 kwa mwezi
Huijui mbagala. Hiv mnajua nyumba aliyopanga jokate (kwa mamunyange) Analipa kias gan Kwa mwez?
 
Mtu anayeijua dar hawezi kuishi mbagala,bora nikae kibaha
Wewe uliyekuja dar kwa msaada wa elimu unaleta wenge .. kijijini kwenu c mlikuwa mnalala na mbuzi leo unajifanya wa kishua
 
Ukiisikia hii kauli unaweza kufikiri muongeaji anatokea Montreal, Canada, kumbe unaweza kukuta yupo zake Simiyu ndaaani huko amepozi mbele ya tembe lao anaponda watu kama hivi. Mitandao bwana!
Yaani hapa nashangaa sana, sijui wanaichukuliaje Mbagala, na wengi wanaokoment negative humu wako huko kwenye vyumba vya kupanga kinondoni mkwajuni
 
Kwamba mtu auze nyumba/eneo lake Kariakoo, Ilala ama Magomeni kwa zaidi ya milioni 700 ama hata bilioni then ashindwe kwenda kununua kiwanja Mbezi, Madale ama Tegeta kwa bei ya milioni 30 ama 50?
Hivi unawajua wazawa wa Dar Wandengereko Wazaramo na Wamanyema mkuu?Hao nyumba ikiuzwa wakishapata hela zao kwanza wananunua magari ya kifahari wanawatafuta wale mademu waliokuwa wanawakataa wakati wakiwa bado fukara wanazitumia kwenye starehe.

Wakiona zimebaki 10mill ndo wanastuka wanaenda kununua popote so ponapona yao ni huko Mbagala,kiwanja 700K inajengwa nyumba ya 7mill isiyokuwa na ramani 2.3mill iliyobaki anaita ngoma na ndugu zake anasherehekea kuhamia kwenye nyumba yake ya rumu mbili iliyojengwa kwenye kiwanja 12×12 isiyokuwa na hata sehemu ya kuanikia nguo huku ana familia ya watoto sita.
 
Mtu anayeijua dar hawezi kuishi mbagala,bora nikae kibaha
Mbagala unaijua vizuri wewe au unaandika tu kwa kusimuliwa. Leo Mbagala rangi 3 unaijua Bei ya fremu? Bila milion 1 hupati frem, Kijichi Bado ni Mbagala lakin Kiwanja mpaka milion 100, hiyo Zachkem hupati kiwanja, lazima umvue mtu bila milion 200 hutoi mtu wewe unaongea nini
 
Kama mbagala haina thamani ili uthibitishe kuwa ni kweli ulizia bei ya kiwanja , otherwise ni blablaa tuu
 
Ndugu yangu humu kwenye JF watu wengi sio wakazi au wazaliwa wa DAR ES SALAAM a.k.a Mzizima utapata taabu kuwaelimisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…