Kwanini asilimia 98 ya watanzania wanaojua Kingereza wanaongea Broken!! Tumerogwa au

Kwanini asilimia 98 ya watanzania wanaojua Kingereza wanaongea Broken!! Tumerogwa au

Kuna shida Gani, Sasa hivi suala la kuongea Kingereza limezidi kuwa kubwa kadiri siku zinavyozidi kusogea, Sasa hivi yani watanzania wengi Wana elimu ya form four au six , Ila wengi hawajui Kingereza, na hao wachache wanaojitahidi au tumasema wanakijua asilimia kubwa zaidi ya 98 ukiwasikiliza wanaongea Broken English japo anaeleweka lakini broken c sana mfano waziri wa elimu Prof. ndalichako, hata lisu ana kizungu kizuri lakini anachapia akiongea muda mrefu, mama Samia anaupiga mwingi kwasababu anasoma, katika kusoma ni rahisi kuliko free style.
Wakenya wanafanyaje, na hizi aibu zetu tunaziweka wapi, sababu hata Mwalimu wa lugha Dr.Lwaitama anachapia Kingereza. Wanaosoma shule za English Medium ni wachache mno 0.0x , wengi ni mashule ya serikali ambapo hata walimu hawajui Kingereza, SoMo la English linafundishwa kwa kiswahili , yaani wanafundishwa Cha kujibia mtihani.

Ukienda You tube , Mtanzania akaongea Kingereza atapata comments mbaya sana, Kuna wakati Hadi wanasema lisu anawahUtubia mabeberu c watanzania.

Angalau Mkapa alikuwa anakipiga chenyewe
Mshangae mtu akishindwa lugha yake lakini hizi za kujifunza ukubwani. Kuchapia kupo maana siyo lugha yako lakini bwana yule alizidi alafu "eti" alikuwa na PhD.
 
Kuna shida Gani, Sasa hivi suala la kuongea Kingereza limezidi kuwa kubwa kadiri siku zinavyozidi kusogea, Sasa hivi yani watanzania wengi Wana elimu ya form four au six , Ila wengi hawajui Kingereza, na hao wachache wanaojitahidi au tumasema wanakijua asilimia kubwa zaidi ya 98 ukiwasikiliza wanaongea Broken English japo anaeleweka lakini broken c sana mfano waziri wa elimu Prof. ndalichako, hata lisu ana kizungu kizuri lakini anachapia akiongea muda mrefu, mama Samia anaupiga mwingi kwasababu anasoma, katika kusoma ni rahisi kuliko free style.
Wakenya wanafanyaje, na hizi aibu zetu tunaziweka wapi, sababu hata Mwalimu wa lugha Dr.Lwaitama anachapia Kingereza. Wanaosoma shule za English Medium ni wachache mno 0.0x , wengi ni mashule ya serikali ambapo hata walimu hawajui Kingereza, SoMo la English linafundishwa kwa kiswahili , yaani wanafundishwa Cha kujibia mtihani.

Ukienda You tube , Mtanzania akaongea Kingereza atapata comments mbaya sana, Kuna wakati Hadi wanasema lisu anawahUtubia mabeberu c watanzania.

Angalau Mkapa alikuwa anakipiga chenyewe

Kwa nini wazungu 100% wanaojua Kiswahili wanaongea broken? Wamelogwa? Hapo ndo utagundua uwezo wako WA kufikiri ndo umelogw
 
^breakthrough^ ni mpasuko pitilivu 🙂 Just kidding. ^mwelekeo mpya^ au ^ufanisi^

But, great comment!
Mwalimu mwenyewe anayefundisha kafeli aidha darasa la saba au Kidato cha nne point hafifu ila kaenda chuo cha ualimu nako anafundishwa kiswahili machache kiingereza.
Mtaani kunazungumzwa kiswahiliEnglish!!
Sasa mtoto anaenda shule anafundishwa EnglishSwahili! Akirudi kwa nyumba ashasahau.!
Yaani kote ni shida.
Na tabia iliyokuwepo huko nyuma sana ya kupeana kazi mtoto wa mjomba, shangazi, shemeji huku Vikaratasi nenda kamwone bosi kumechangia sana hali hizi ukiachilia Siasa!!

Tuna safari ndefu sana.
 
Kama mimi huku,nikiwa namsikiliza mtu akinisemesha namwelewa vizuri sana na kichwani nakuwa najua kabisa namna ya kumjibu ila sasa nikianza kufungua mdomo yote sijui ni yanakimbia au nisemeje maana hiyo broken yake ni ya kiwango cha lami,ila at least tunakielewa vibaya kama kinazungumzwa halafu hujui kinachosemwa.

Inavunja sana moyo but siyo lugha yetu so hatuna cha kupoteza (kujifariji tu)
Nikute nimelewa sasa
[emoji23][emoji2960]
 
Upo sahihi kabisa mkuu

Nyerere alifanya kosa kubwa kuamua lugha ya kiswahili iwe ndio lugha ya kufundishia mitaala yetu

Kiingereza mtoto anaanza kujifunza kama somo na lugha ya kusomea anapoingia kidato cha kwanza ambapo kimsingi umri wa kujifunza lugha unakua umepita.

Mtoto wa form I anajifunza kiingereza kama foreign language ambapo hawezi ku acquire skills za native speaker

Nyerere aliamue afundishe kiswahili as unifying factor hiyo ilikua ni hofu isiyo na sababu maana kwa uhalisia sio kama Watanzania wanaoongea kiswahili wangekisahau kwasababu tu eti kiingereza kinatumika katika taasisi za elimu kama lugha ya kufundishia

Matokeo yake hakuna lugha yoyote kati ya kiswahili na kiingereza ambayo inaeleweka kwa ufasaha na wanafunzi wetu.

Wito wangu ni kwamba bado hatujachelewa. Mitaala ya masomo yote( ukiondoa Kiswahili chenyewe) iwe kwa lugha ya kiingereza kuanzia shule za awali hadi elimu ya juu. Hakuna atakaye kisahau kiswahili

Usimlaumu sana Nyerere. Humtendei haki. Alifanya sehemu yake sana tu. Nchi kama Zimbabwe na SA, kwa mfano, lugha mama ni lazima hadi vyuo vikuu, but angalia ngeli yao kwa sehemu kubwa ^imenyooka,^ tofauti ya Bongo ^imenyonyoka.^
 
Na hili wimbi la wakenya waliojaa Nchini Sasa baada ya b.mkubwa kufungua nchi tutakoma
 
Mkoloni aliyekuja bongo alikuwa na kigugumizi au matatizo mengine ya kiukoo na ni tofauti na aliyeenda Kenya, Zambia , uganda, maliwi na South Afrika. Hapa bingo hata usome uwe profesa lazima ulimibunakuwa mzito na kuchanganya tense ni suala la kawaida au kutafuta msamiati wa kuongea hata sekunde kadhaa pale unapobanwa kuongea chenyewa kwa dakika 30 mfululizo. Ila mbongo alivyo na mbwebwe mwambie aongee kiswahili atachanfanya you know kibao hasa wadada wa mjini hata wale waliosoma sant medium nao vilevile
 
Naona wewe umeona lugha tu. But mfumo wote wa elimu, to say the least, ni BOGUS. We lack visionary leaders. Huwezi kuzungumzia maendeleo kokote, bila kuweka kipaumbele katika elimu. Never!

JKN alizungumza na kuandika mengi sana kuhusu elimu. Na juhudi zake za kuinua elimu zilikuwa kubwa zaidi kuliko za viongozi wote waliomfuata kwa pamoja.

^Aliyepata fanaka ya kupata elimu ajue anawiwa na mamilioni ya Watanzania ambao hawajui hata kusoma na kuandika. Tukishirikiana, anayejua kusoma na kuandika akamfundisha asiyejua, taifa hili litapiga hatua ya maendeleo haraka, na bila shaka tutashindana na Dola ya Ulaya na Amerika^ ~ JKN.
Kiukweli tatizo kubwa kwangu naloliona ni lugha ya kufundishia.

Nikilinganisha na mataifa ninayoyafahamu bado naona wanapotushindia ni lugha ya kufundishia.
 
Mleta mada kwenye kiswahili ndiyo kuna makosa makubwa mno yanafanywa na wazungumzaji kuliko hata kwenye kiingereza. Lkn kwa kuwa watanzania hawakijali kiswahili na wanakinyenyekea sana kingereza ndiyo maana hawoni.

Mfano; Nimemkuta hayupo.

Hii sentensi ina makosa makubwa mno. Kama ingetamkwa kwa kingereza mzunguzaji angetangazwa na TBC kuwa amezungumza broken. Lkn kwa kuwa ni kiswahili ambacho hakuna anayekinyenyekea husikii watu wakipiga kelele.

Mleta mada ni miongoni mwa watu wanaokinyenyekea zaidi kingereza. Hii inashangaza sana. Na tabia hii ipo nchi zilizoathiriwa na tabia ya kuabudu vya wakoloni.

Ndiyo maana ukienda Uingereza huwezi kusikia waingerza wakizodoana kwa kushindwa kuongea kijerumani, kihispania, kifaransa, kiitaliano, kichina,.n.k.

N.B. Makosa ktk lugha yapo ktk kila jamii. Makosa haya ndiyo hupelekea lugha kukua. Hata waingereza wanaharibu Sana kingereza ktk mazungumzo yao ya mtaani. Baadaye makosa hayo yakizoeleka Sana hufanywa kuwa kingereza sanifu.
 
Usimlaumu sana Nyerere. Humtendei haki. Alifanya sehemu yake sana tu. Nchi kama Zimbabwe na SA, kwa mfano, lugha mama ni lazima hadi vyuo vikuu, but angalia ngeli yao kwa sehemu kubwa ^imenyooka,^ tofauti ya Bongo ^imenyonyoka.^
Zimbabwe na South Africa English ni lugha ya pili kwa waliowengi.

Lugha ya pili ni rahisi saana kujifunza. Mfano sisi watanzania tunaanza kuongea lugha zetu kwanza kabla ya kiswahili.

Tukijifunza kiswahili ni rahisi na wengi tunakiongea na kukiandika bila tatizo lolote.

Sasa tatizo linakuja unapoongezewa English tena ukiwa na miaka 14.
 
Kuna mahala tulikwama toka enzi za uhuru...

Uamuzi ni wetu either tuchague kiswahili msingi mpaka chuo kikuu au kienglish msingi mpaka chuo kikuu.. tukiendelea na huu unafiki tutaendelea kuishi kama wachawi milele..
 
Mleta mada kwenye kiswahili ndiyo kuna makosa makubwa mno yanafanywa na wazungumzaji kuliko hata kwenye kiingereza. Lkn kwa kuwa watanzania hawakijali kiswahili na wanakinyenyekea sana kingereza ndiyo maana hawoni.

Mfano; Nimemkuta hayupo, n.k

Hii sentensi ina makosa makubwa mno. Kama ingesemwa kwa kingereza mzungumzaji angetangazwa na TBC kuwa amezungumza broken. Lkn kwa kuwa ni kiswahili ambacho hakuna anayekinyenyekea husikii watu wakipoga kelele.

Mleta mada ni miongoni mwa watu wanaokinyenyekea zaidi kingereza. Hii inashangaza sana. Na tabia hii ipo nchi zilizoathiriwa na tabia ya kuabudu vya wakoloni.

Ndiyo maana ukienda Uingereza huwezi kusikia waingerza wakizodoana kwa kushindwa kuongea kijerumani, kihispania, kifaransa, kiitaliwno l, kochina,.n.k

kutoamua kuwa na lugha moja ndio makosa yalipo ndio maana hatujui kiswahili wala kienglish tupo tupo tu....
 
Kiukweli tatizo kubwa kwangu naloliona ni lugha ya kufundishia.

Nikilinganisha na mataifa ninayoyafahamu bado naona wanapotushindia ni lugha ya kufundishia.
Personally, naona tatizo liko kwenye mfumo wa elimu na ufundishaji. Kama huamini nachosema, pls tembelea shule yoyote ya serikali, msingi au hata sekondari, then fanya hata ^utafiti mboga,^ utaelewa nachosema.

Tatizo la ujinga kwenye nchi yetu linaanzia walimu na wakufunzi wanaofundisha mashuleni na vyuoni. It's pathetic, kwa sehemu kubwa! Nyerere aliposema maadui wetu wakuu ni ^UJINGA, MARADHI & UMASKINI,^ hakukosea hata kidogo kuanza na ^ujinga^ kwenye orodha yake.
 
Back
Top Bottom