Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,629
- 34,199
Hata South Africa, Kenya, Malawi na Zimbabwe wana matatizo ya English.Zimbabwe na South Africa English ni lugha ya pili kwa waliowengi.
Lugha ya pili ni rahisi saana kujifunza. Mfano sisi watanzania tunaanza kuongea lugha zetu kwanza kabla ya kiswahili.
Tukijifunza kiswahili ni rahisi na wengi tunakiongea na kukiandika bila tatizo lolote.
Sasa tatizo linakuja unapoongezewa English tena ukiwa na miaka 14.
Binafsi, ninachoona kina-miss ni kidogo sana hasa juhudi binafsi za kujifunza lugha.
Mtu akiamua kukaza kujifunza lugha anaijua vizuri tu.
MIfano halisi ni WAMASAI tena ambao hawakwenda shule kabisa.
Kuhusu lugha ya kufundishia, mkitaka mkae gizani kwenye huu ulimwengu kijiji ipotezeeni English.