Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,051
Kwa mazingira ya TZ Kiswahili lazima tu utaongea. Kwa hiyo mkazo uwekwe kwenye Kiingereza. Kiswahili kiwe somo tu. Medium of instruction kwa masomo yote yaliyobaki iwe Kiingereza. Ndivyo ilivyo Kenya, Uganda, Malawi... Wao wanaongea lugha zao na Kiingereza kwa ufasaha. Sisi tumeweka mkazo kwenye Kiswahili ambacho hata usipoenda shule utazungumza tu.
Hili ni tatizo la mitaala yetu Wala sio tatizo la wazungumzaji.
Tumechanganyikiwa , msingi tunasoma kwa kiswahili Kisha Sekondari Kiingereza.
Breakthrough (sijui kiswahili chake) ya lugha ni kati ya umri wa 1-10.
Na tuliowengi Kiingereza ni lugha yetu ya tatu. Na hili haliathriri uzungumzaji wetu tu. Linaenda mbali na kuathiri hata confidence yetu.
Tuamue moja, kutumia kiswahili au Kiingereza ngazi zote.