Kwanini asilimia kubwa ya viongozi wanawake wakubwa Serikalini na taasisi zake wengi hawana waume?

Kwanini asilimia kubwa ya viongozi wanawake wakubwa Serikalini na taasisi zake wengi hawana waume?

Wanaume ni wakarimu sana. Tukipata pesa la kwanza tunawaza kushea na kinadada kwa kuongeza warembo wa kutumia nao.

Wanawake ni wabinafsi, wakipata pesa tu la kwanza wanawaza kujiengua toka kwa wanaume kwa kuhisi watakula pesa zao.
 
Ikiwa umefanya tafiti Nadhani ingependeza Za Kama ungekuja na takwimu sahihi ili kutupa Wigo na mapana ya kujadiri.

Mwisho kuwa na waume ama kutokuwa nao si shida,Nadhani ungetupa tathmini ya utendaji wao,ufanisi wao,Mapungufu kiutendaji Kama yapo,Ushauri nini kifanyike watoke kwenye mapungufu..Kama kuna maeneo ya pongezi pia tuwape..
 
Hivi kwa nini asilimia kubwa ya viongozi Wanawake wakubwa serikalini na taasisi zake wengi hawana waume
Swali ni je wanaowapa vyeo wanapenda zaidi Wanawake wasiooleea au? Huu ni ubaguzi wa wazi

Wanawake Unakuta hata viongozi wa vyama vya siasa ni hivyo hivyo wa juu kama ni Wanawake wengi utakuta hawana waume wa ndoa

bungeni pia hivyo hivyo wengi hawana waume wa ndoa
Mwanamke akipata pesa au elimu kubwa ni ngumu kumsikiliza mwanaume
 
Wanaume ni wakarimu sana. Tukipata pesa la kwanza tunaweza kushea na kinadada kwa kuongeza warembo wa kutumia nao.

Wanawake ni wabinafsi, wakipata pesa tu la kwanza wanawaza kujiengua toka kwa wanaume kwa kuhisi watakula pesa zao.
Si mnaona hizi propaganda zenu za uongo dhidi ya wanawake ili ionekane wanawake ni wabinafsi, lakini tofauti ni kwamba wanawake wakipata pesa wanakula na watu muhimu kwao kwanza, ila wanaume wakipata pesa wanatanguliza kula na watu wasio na umuhimu kwao halafu wale wenye umuhimu wanakumbukwa baadaye huko

Mwanamke akipata pesa hali na wanaume lakini atakula na wanaye, wazazi, ndugu na jamaa ila mwanaume akipata pesa atakula na wanawake na washkaji mara moja moja ndio atawakumbuka hao wengine, yes ni wanaume wangapi wakipata pesa wanakimbilia kuhonga wanawake ila wazazi wao wakiomba hela wanapigwa kalenda, ni wanaume wangapi wakipata pesa wanatelekeza watoto na kuwaachia wake ila wanawake ni ngumu kufanya hayo

Hata wazazi wengi wenye watoto wa jinsia zote huwa wanakiri kwamba wana kumbukwa zaidi na watoto wao wa kike kuliko wa kiume, kwahiyo ninyi wanaume mnawaita wanawake wabinafsi kwa sababu tu wakipata hela hawali na ninyi maana ninyi siyo priority kwao na si kwa sababu eti wanawake ni wabinafsi, ninyi kama mkipata pesa wanawake ndio priority kwenu hizo ni shida zenu binafsi na tamaa zenu za kijinga ila msilazimishe iwe hivyo na kwa wanawake
 
Hivi kwa nini asilimia kubwa ya viongozi Wanawake wakubwa serikalini na taasisi zake wengi hawana waume
Swali ni je wanaowapa vyeo wanapenda zaidi Wanawake wasiooleea au? Huu ni ubaguzi wa wazi

Wanawake Unakuta hata viongozi wa vyama vya siasa ni hivyo hivyo wa juu kama ni Wanawake wengi utakuta hawana waume wa ndoa

bungeni pia hivyo hivyo wengi hawana waume wa ndoa
Kummanage mwanamke mwenye akili anaetumia logic uwe na akili mara 2 yake vinginevyo wanaume wengi ni vilaza hawawezi
 
Back
Top Bottom