Kwanini Askofu Bagonza hakamatwi ila Sheikh Ponda? Tunaomba Serikali itoe ufafanuzi

Waislam wa siku hizi wengi wao ni waoga sana, hivyo mtaendelea kuteswa hadi pale akili itakapowakaa sawa.
Halafu wakifanya kweli mnakuja na kauli ya wanaleta vurugu! Wanataka kuharibu amani ya nchi! Au kwa vile yupo Bw. Yule asiyependwa?!
 

Hoja yako ni dhaifu isiyo na mashiko. Sheikh Ponda amekamatwa kwa sababu ya ugomvi wake binafsi na wake zake nyumbani hadi tuache kuhusisha kukamatwa kwake na Uislam?

Waraka umetoka kwa Shura ya Maimamu Tanzania, sio Uislam huo?
 
Umeuliza wewe umejibu wewe, sasa mimi niseme nini zaidi?

Upo huru kwa mawazo yako.
 
Anzisheni hivyo vikundi vyenu vya kigaidi tuwaoneshe kazi ! !!

... Kawaulinze wezenu wa kibiti wako wapi . Toka nyuma ya keyboard anzisha hicho kikundi chenu alfu muone
Tumia akili kiufasaha kwa kuielewa mantiki. Huyo uliyemkoti katolea mfano. Ila haya mambo ya dini moja ikisema wanaanchwa dini nyengine ikisemwa wanaipata si jambo shwari. Kwa sababu dini ni kama ukabila.

Siku wakiamua hali ikashika hatamu nchi inaweza kubadilika. Kwa sababu hata hivyo vyombo vya dola waliyopewa dhamana ya kulinda nchi nao wana dini. Hali ikiwa ya ukomavu mambo yataparaganyika zaidi.
 
Kwa hiyo unapanga kuwa gaidi kwa sababu ya Ponda kukamatwa?Imani yako inakufundisha ugaidi? Id yako ni ya muda mrefu humo,nitarejea ulivyokuwa unachangia. Kwa nini viongozi wamekana waraka?
 
Hembu ❌
Eka❌

Ndo maana mnaandika waraka kama vilaza.
Hili ni tusi!
Kuchunga adabu ni suala zuri pia. Kosa la mmoja uliyemkoti unatukana na jopo la viongozi wa Waislam? Hata kama hilo jopo taarifa yao ni ya uchochezi lakini bado ulichokitenda ni utovu wa nidhamu.
 
Anzisheni basi hivyo vikundi vya kigaid ndani ya tanzania hii chini ya magufuli tuwaone mnavyo sambaratishwa ndani ya sekunde.
 
Kudai haki ni jambo jema pia kukemea uovu ila kuunda vikundi vya ugaidi ni kuchupa mpaka
 
Ndugu Unayejiita Assad wa Syria, mimi ni muislamu mwenzako, kwanza ni kukosoe njee ya mada, utaniwia Radhi, unatumia jina la Asaad huyu aliyekuwa mtawala wa Syria, kweli kama una uchungu na binadamu wenzako au watu wa dini yako, au hupendi dhuluma na upendeleo, Ndugu yangu , hata siku moja usingelitumia jina la huyu Dhalim aliye fariki, Assad Aliupiga Mji Mzima mabomu na Missiles kwa sababu kulikuwa na upinzani na pia mji huo ulikuwa na wenyeji wengi wa madhehebu tofauti na yake.

Twende kwenye Mada, Ndugu tusiwalaumu Watawala ambao tunawapa power ya kutudhalilisha, hatupingi wala hatusemi tunapochaguliwa kiongozi wa Bakwata tusiyemtaka au asiyefaa, Hatuna ushirikiano waa maana kama makanisa yanavyo washirikisha waumini wao na kuwafanya wamoja katika mambo yao muhimu.

Makanisa, Maaskofu yanaheshimiwa na kuogopewa kwa sababu wako very well Organized, wana Msimamo, hawalambi viatu vya Raisi wala serekali yake. Tena wakristo hawana haja ya kupiga kelele, msimamo wao na namna walivyo jijenga unawaogopesha viongozi.

Tuko waislamu wengi sana hapa TZ, tunao uwezo wa kubadilisha mfumo wa utawala, Tukitaka tuwe na sauti au power ya kuweza kuhakikisha Serekali inawatendea haki wananchi wote bila ya ubaguzi ni lazima tuwe na mfungamano na tuweze kuwachagua viongozi wazuri na tunaowalipa mishahara ili waweze fanya kazi.

Ndugu ni wakati muafaka waislamu tukasimama kidede na kujijenga bila kumtenga mtanzania yoyote yule.

Tusiwalaumu wengine kwa makosa yetu wenyewe. Awamu hii imevunja kila mila ya kiserekali, inatuletea udini kwa manufaa ya watawala na wala sio kwa watu wa dini fulani.
 
Una uhakika yule wa Bukoba ni Mkatoliki?

Mbona mnakurupuka sana Waumin wa Allah S.A.W?
Nadhani alimaanisha Askf Severine Niwemugizi wa Rulenge aliyekuwa akikosoa sana baadae akatumiwa Immigration kuhoji uraia wake, baada ya hapo simsikii sana.
 
Eti anasema vikund vya ugaid aisee suo kwa tanzania hii ninayo ijua mimi, na vikundi vyenu mtakakamatwa kabla hata hamjakaa kupanga mipango , iacheni tanzania iendelee
 
Point taken
 
Halafu wakifanya kweli mnakuja na kauli ya wanaleta vurugu! Wanataka kuharibu amani ya nchi! Au kwa vile yupo Bw. Yule asiyependwa?!
Na Kikwete alivyokuwa Rais ilikuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…