Kwanini baada ya Uhuru, Nyerere aliwatema waliopambana tangu mwanzo

Kwanini baada ya Uhuru, Nyerere aliwatema waliopambana tangu mwanzo

Kwanini aliwatema watu Kama
Abdulwahid Sykes
Bibi Titi
Na baadhi katika serikali yake

Nawasilisha
Wengi wao ni waswahili maneno mengi hawakuwa na elimu dunia bali elimu akhera.

Wasingeweza kufaa chochote katika kujenga serikali..mana kuendesha serikali sio maneno bali ni elimu na usomi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa nini samia amewatema wazalendo kama ndugai,kabudi na lukuvi?
Hawa nao ni wazalendo. Hujui Kama kabudi alitwambia pesa tunazodai kuwa aliudanganya uma ili mungu wake jpm afurahi? Hujui ndugai alifurahia kutaka kuuawa kwa lisu? Mzalendo ni mmoja tu nchi hii ambaye ni lisu tu mwenye kusema ukweli bila kujali kupigwa lisasi
 
Wao walitaka wawe WAKOLONI namba mbili, na nchi iwe ya kidini.

Wakati Nyerere alitaka nchi IWE Mali ya Kila MTU na ISIYO na DINI.
Sasa kama ni hivyo basi wasingeshirikiana na Nyerere toka mwanzo ambaye alikuwa dini tofauti na wao, maana hata kama Nyerere angekubali nchi iwe ya kidini ndio ingekuwa ya dini gani?
 
Ukiwa na watu wengi mnapambania kitu humo kuna matarajio tofauti. Nyerere alikuwa mzalendo ili asiongoze kwa miluzi mingi alibidi ajitenge na wale waliojikuta wazalendo sana na kuamini wanastahili mafao fulani. Kwamba wao wamejitoa na ni first class citizens.

Kati ya nchi zilizofanikiwa, naweza reference Marekani tu iliyokuwa na statesmen waliokubaliana wote na waliaminiana wakitanguliza uzalendo. Kila mtu aliwekewa nguvu zake kwa kujenga taifa. Wakati wajuzi wa sheria ambao ndio walikuwa wengi walisaidia kuunda katiba ambayo inatumika hadi leo, wafanyabishara waliionesha nchi inatakiwa iweje kibiashara na kimataifa, makamanda wa kijeshi walisaidia mbinu za ulinzi, madaktari maarufu na wakulima wakubwa nao walitoa mchango wao. Kati ya walioianzisha Marekani hakukuwa na mbumbumbu au kilaza, kila mtu alikuwa na proffesion yake, smart na alikuwa na ajira kabla wala hakuna aliyekuja kuponea serikalini. Waliendelea hivi hivi na hawakugeukana.

Kinyume chake ni nchi nyingi zinazopitia msuguano. Mfano USSR ilipoanza Lenin hakuwa anawaamini watu kadhaa, akafariki ikatokea mgogoro baina ya team ya Leon Trotsky na Josef Stalin, Trotsky akauwawa baadae na team yake ikauwawa. Stalin alidumu sana kwa mauaji na purges alipokufa ikatokea mgogoro tena, Lavrentiy Beria aliyekuwa mkuu wa usalama alikuwa anaandaa maafisa wake kwenye msiba wakimaliza tu wateke top government officials. Nikita Khrushchev akafanikiwa kumshawishi General Zhukov amkamate Beria ambaye alikuwa ni the worst kuongoza nchi kati ya wote waliokuwa na uwezekano. Beria akasomewa mashtaka haraka akahukumiwa kifo. Hali iliendelea hivihivi kukaa chonjo.

I suspect Nyerere asingefanya vile ingekuwa hali kama Nigeria, alilazimika tu
 
Hakuna aliye achwa na walishika nafasi mbaimbali wao na ndugu zao...

Kuna mpaka ndugu zao walikuwa mabalozi na wengine walienda ishi ulaya na marekani na kusoma huko pia

Hivyo walipata mafanikio zaidi yako
 
Sasa kama ni hivyo basi wasingeshirikiana na Nyerere toka mwanzo ambaye alikuwa dini tofauti na wao, maana hata kama Nyerere angekubali nchi iwe ya kidini ndio ingekuwa ya dini gani?
Walikuwa na elimu za hapa na pale na walitaka support ya kanda ya ziwa na maeneo mengine. Walienda Bukoba wakamtumia mzee Sued Kagasheki ambaye ni mwislamu kwenye idadi ndogo ya waislamu, na walienda maeneo ya Kilimanjaro wakiungana na waislamu wachache uko wakati wengi ni dini nyingine.
Exposure ilikuwa muhimu pia, Nyerere kasoma Uingereza. Bado alikuwa na mahusiano mazuri na wakoloni.
Walitaka kijana na msomi wakawa na imani naye. Hata hivyo hawakuwa na udini kwenye struggle, udini ufuata baada ya kupata mlichotaka
 
Kwahiyo wazo la kutaka kufanya nchi ya kidini lilikuja baadaye na lipi lilifanya waone uwezekano huo upo?
 
Kwahiyo wazo la kutaka kufanya nchi ya kidini lilikuja baadaye na lipi lilifanya waone uwezekano huo upo?
Of course radicalism ya kidini ilikuja baadaye. Hata ukiangalia wanawake was zamani was kiislam walikuwa hawafuniki vichwa wala kuvaa hijab.

Lakini baadaye likajitokeza kundi LA kina Mohamed Said wanaojifanya wanaijua sana dini. Mpaka sasa Sikh bizi mashuleni ukifika unajua mkrisisto nani, muislam nani ndio wakaona wao kama wao kina kitu walistahili ambacho Nyerere hakuwapa.. Zikaanza SIASA ZA MASJID kuwaka MOTO.
 
Back
Top Bottom