Ukiwa na watu wengi mnapambania kitu humo kuna matarajio tofauti. Nyerere alikuwa mzalendo ili asiongoze kwa miluzi mingi alibidi ajitenge na wale waliojikuta wazalendo sana na kuamini wanastahili mafao fulani. Kwamba wao wamejitoa na ni first class citizens.
Kati ya nchi zilizofanikiwa, naweza reference Marekani tu iliyokuwa na statesmen waliokubaliana wote na waliaminiana wakitanguliza uzalendo. Kila mtu aliwekewa nguvu zake kwa kujenga taifa. Wakati wajuzi wa sheria ambao ndio walikuwa wengi walisaidia kuunda katiba ambayo inatumika hadi leo, wafanyabishara waliionesha nchi inatakiwa iweje kibiashara na kimataifa, makamanda wa kijeshi walisaidia mbinu za ulinzi, madaktari maarufu na wakulima wakubwa nao walitoa mchango wao. Kati ya walioianzisha Marekani hakukuwa na mbumbumbu au kilaza, kila mtu alikuwa na proffesion yake, smart na alikuwa na ajira kabla wala hakuna aliyekuja kuponea serikalini. Waliendelea hivi hivi na hawakugeukana.
Kinyume chake ni nchi nyingi zinazopitia msuguano. Mfano USSR ilipoanza Lenin hakuwa anawaamini watu kadhaa, akafariki ikatokea mgogoro baina ya team ya Leon Trotsky na Josef Stalin, Trotsky akauwawa baadae na team yake ikauwawa. Stalin alidumu sana kwa mauaji na purges alipokufa ikatokea mgogoro tena, Lavrentiy Beria aliyekuwa mkuu wa usalama alikuwa anaandaa maafisa wake kwenye msiba wakimaliza tu wateke top government officials. Nikita Khrushchev akafanikiwa kumshawishi General Zhukov amkamate Beria ambaye alikuwa ni the worst kuongoza nchi kati ya wote waliokuwa na uwezekano. Beria akasomewa mashtaka haraka akahukumiwa kifo. Hali iliendelea hivihivi kukaa chonjo.
I suspect Nyerere asingefanya vile ingekuwa hali kama Nigeria, alilazimika tu