Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Kuna uwezekano mkubwa wa kuishi maisha mazuri na yenye raha hapa duniani. Lakini ajabu kuna watu wanaridhika kuishi maisha duni. Wasiokubali kuishi maisha ya kimaskini wanapambana hadi mwisho.
Wanaoridhika kubaki maskini huamini kwamba walizaliwa kwa bahati mbaya na hawana uwezo wa kubadilisha hali yao. Wasiokubaliana na mtazamo huo, hata wakikutana na changamoto nyingi, huendelea kupambana mpaka "watoboe." Msingi wa tofauti hii mara nyingi hutokana na mtazamo wa ndani wa mtu kuhusu mustakabali wa maisha yake.
Katika maisha ya kiroho, kuna watu wanaokubali kukaa katika hali duni ya dhambi na kuna wanaotafuta mabadiliko ili waishi maisha yenye raha nafsini mwao. Je, unahitaji raha nafsini mwako? Yesu anakuita akupe raha hiyo:
Mathayo 11:28-30
“Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha...nanyi mtapata raha katika nafsi zenu..."