Kwanini Balozi Mulamula alikuwa anaonekana smart sana na kuheshimika huko Ugenini?

Kwanini Balozi Mulamula alikuwa anaonekana smart sana na kuheshimika huko Ugenini?

Jaribu kuangalia uwekezaji wa Marekani nchini China kuanzia mwaka 1980 hadi 2015 tu ndio uje uongee. Hayo mataifa yasingefika hapo yalipo bila uwekezaji mkubwa toka Marekani, sasa nashangaa eti wewe unapinga wakati wenyewe wanakiri hilo.
Tunaongea vitu viwili tofauti. Kwani ni nani aliyezuia wawekezaji kuja Tanzania? Kujitembezatembeza duniani ndiyo kuvutia wawekezaji? Wekeni mazingira bora ya uwekezaji katika nchi yenu (umeme wa uhakika, skilled personnel, barabara bora, n.k) wawekezaji watakuja tu. Mulamula kupiga picha na Biden na Obama ndiyo amevutia wawekezaji hapo?
 
Utashangaa sana kusikia wewe hukuwa smart simply because unaji associate na hao unawa perceive kuwa smart...Any smart person can still be smart even with his people na bado akaleta chanhe kubwa kubwa tu bila hizo associations za kitapeli wa dunia...Kina Abraham Lincoln na Franklin Roosevelt Wa huko walikuwa wana associate na akina nani hadi walipofanikiwa kuzifanya nchi zao kuwa powerful? Sana sana walijiepusha na kila aina ya European influence chini ya Kingdomship ya U.K na Roman Empire mpaka kutengeneza kitu ambacho hakikuwepo duniani, yaani Democratic governance....Sasa kama kuwa smart kunamaana ya uchawa basi hapo na log off.....

Africans mind zina ukoko na kutu hasa ya kutawaliwa...Hazina confidence wala haziwezi kuamini katika wao wenyewe...Nadhani tukihangaika na hili tatizo itakuwa njema zaidi...Nasikitika kuzaliwa nchi inayoamini ya kuwa kiwa smart ni kuwa chawa wa watu weupe...A parasitic kind of association ..
In short tuna ushamba wa maendeleo
 
Kama wazungu walikuwa hawamuelewi Samia kwasababu ya kuwa makamu wa Rais wa Magufuli aliyeharibu uhusiano wetu wa kimataifa, huyu mama alikuwa kiungo mzuri sana.

Kwenye mazingira kama haya kuleta habari za "collective responsibility" ni ujinga mtupu, hiyo "collective responsibility" ndio iliharibu mwanzo ikashindwa kumshauri vizuri yule aliyeharibu, then unamteua anayeaminika huko nje ili akatengeneze, ajabu baadae nae unamuondoa kwasababu ya kukumbatia mawazo ya wale waliofeli!.

Huyu mama alikuwa anatengeneza connection nzuri ya kurudisha imani ya wazungu kwa Samia na serikali yake, lakini kwa kuondolewa kwake, naona Samia ataendelea kupokewa na kina Mange kila akienda US.

Hakuna jipya hapo! Hata alipoenda na huyu Mullermuller bado alipokelewa na akina Mange Kimambi, sasa sijui huyu nishomire aliconnect vipi hapo mpaka akina Kimambi wakampokea mama!
 
Kutakuwa kuna jambo zito hapo, usichukulie kimzahamzaha.

Inawezekana hilo ndilo limemkaba shingoni huyo mama na kupoteza kazi

Ni kweli ndiyo maana Rais alipowaapisha wale aliowateua baada ya huyu kutemwa, aliwakumbusha kwa mafumbo kuwa wazingatie viapo vyao! Hapo tu fikiri na chukua tahadhari!
 
Kama wazungu walikuwa hawamuelewi Samia kwasababu ya kuwa makamu wa Rais wa Magufuli aliyeharibu uhusiano wetu wa kimataifa, huyu mama alikuwa kiungo mzuri sana.

Kwenye mazingira kama haya kuleta habari za "collective responsibility" ni ujinga mtupu, hiyo "collective responsibility" ndio iliharibu mwanzo ikashindwa kumshauri vizuri yule aliyeharibu, then unamteua anayeaminika huko nje ili akatengeneze, ajabu baadae nae unamuondoa kwasababu ya kukumbatia mawazo ya wale waliofeli!.

Huyu mama alikuwa anatengeneza connection nzuri ya kurudisha imani ya wazungu kwa Samia na serikali yake, lakini kwa kuondolewa kwake, naona Samia ataendelea kupokewa na kina Mange kila akienda US.
Sisi wa Africa bado tunao vibaraka wa Wazungu mpaka leo.
Nenda wewe kaishi kwao.
 
Kwa taarifa yako
Hizo Picha na Obama huyo Mama Mula Mula na familia yake wamepiga kitambo, Hawakupiga Picha kwa sababu ya cheo chake cha uwaziri hatujui amekosea wapi Akatumbuliwa Mh Raisi anafahamu zaidi
Ni Mama muungwana sana hasie na majivuno
Alikua ni balozi wa Tanzania na uhusiano wake ulikua ni mzuri na viongozi wa Marekani
Wapi nimesema kuwa alipiga kwasababu ya uwaziri wake. Na wapi nimesema kuwa zimepigwa hivi karibuni?
 
Binafsi sikuwa namwona ana weledi wa kupindukia wa kidiplomasia, wala mwingine, typial ya watu wa UN! Nilichoka pale alipofasiri kwa KIiingereza 'Kongoni' kuwa ni 'aina ya paa' (gazelle) badala ya (flamingo) mbele ya wageni na rais aliyekuwa ametoa zawadi hiyo....na vikosa vingine vidogo vidogo chungu nzima.
Ila kitendo cha kumwuuzulu mara tu baada ya kukutana na Biden hakikuwa kitendo cha hekima, hata kama alikuwa na kosa lisilosameheka. Timing is so critical in politics. This act, had sent a wrong message to USA, though it had been driven by an internal agenda.
 
Kote huko mnazunguka, Samia anataka misaada ikija anataka Zanzibar ipate fungu kubwa, kama zile hela covid-19 kwahiyo balozi alikuwa na misimamo, ukimsikiliza Samia ataona anatetea Zanzibar kama nchi sio sehemu ya muungano. Kilicho kuondoa balozi, maslahi ya Zanzibar kama Samia anavyotaka, ndiyo balozi akamkumbusha hua iko hivi, Samia ndiyo maana akasisitiza hana utii kwa mamraka zilizomzidi, akaamua kumla kichwa.
 
Aliemuheshimu Mulamula nje ya nchi ni nani?

Na kwa lipi hasa alilofanya hadi apewe heshima nje ya nchi

Hana andiko lolote linalotumiwa kimataifa kama reference katika political references.

Hana impact yeyote kama mwanadiplomasia acting as a mitigator for anyone to refer to proposition aliyotoa.

She is just plain
 
Naelewa sio vyuo vyote vinatoa research skills kwa wanafunzi wao kama mandatory module (otherwise vyuo vingi utoa ilo somo kama voluntary participation) hata ulaya watu wengi vyuo vya kawaida awawezi andika report wasiopitia hilo somo can’t do research properly until dissertation year wanapofundishwa kufanya research.

Likewise msingi wa hiyo module ni kujua credibility sources; based on criteria za ku define worthiness ya mtu au referencing unazoweza mtaja mtu (Usually it has to do with their academic reputation or expertise Worthiness).

Sasa Mulamula unaweza mtaja kama credible source kweli. On what merit, labda kama anaongelea government policy ambayo ipo wazi kuhusu mambo ya nje (yeye akiwa kama waziri au balozi) kama angekuwepo serikalini ana merit ya kusikilizwa zaidi kwa wasio ielewe hiyo policy that’s when you are allowed to quote her given her position.

Otherwise hana credibility internationally as a political analysts wala hana paper ambayo inatoa mwangaza wowote (even to referred to in local diplomacy), Mulamula hana kitu chochote special kushinda mtu mwingine anaepitia succession planning wizara aliyotokea kwa sasa she is just Vanilla alielamba asali kupelekwa marekani kama balozi kurudi akapewa uwaziri that’s about it. But she is not special in any other way.
 
Beberu ukimtumikia kwenye maslahi yake mbona kila siku atakuita mnywe chai na kupiga picha, siyo swala la kuwa smart.......mkishakinzana kwenye mitazamo tu, labda useme wewe hauungi mkono ushoga, lazima beberu akuone nuksi na atafute njia za kuku blacklist.
 
Aisee! Siku Max akipoteza ufungua wa I'd zetu tutafungwa bila kesi mahakamani.
Matusi gani haya unashindwa kuheshimu kiongozi mkuu wa nchi
Kiongozi mkuu wa nchi huwa anahamasisha ufisadi?Au unamaanisha kiongozi mkuu wa nchi yako na mkeo?
 
Ngoja nikwambie kitu, no any country that can succeed in isolation. After the second world war the European economy had totally collapsed and they only needed the famous "Marshall Plan" to return their battered economies back on track.

The economic input that the US put on the 17 European Countries that led to the recovery of the economies of those countries made them to maintain landmark ties with the US politically, economically and socially.

Needless to say, the countries like China, Japan, South Korea, Germany etc couldn't have attained the level of economic prosperity they currently enjoy without massive foreign investment mainly from USA and if they could pursue the self isolating policy like one you're advocating, they could not have achieved the economic milestone of today.

I believe, in most uncertain terms, that had Iran not have a chilly relationship with the US, the country's level of development would have surely been at par with that of South Korea or even surpassed.
Umeandika kitu muhimu sana sana. Watanzania wanatazama lakini hawaoni. Wanakwenda kila mahali duniani lakini hawarudi na funzo lo lote. Wanatazama lakini hawaoni. Hongera sana!!
 
Back
Top Bottom