Kwanini bara la Afrika lipo nyuma kwa kila kitu kuliko mabara mengine?

Kwanini bara la Afrika lipo nyuma kwa kila kitu kuliko mabara mengine?

Joined
Apr 7, 2018
Posts
10
Reaction score
14
Habari gani ndugu wananchi?

Kuna jambo limeliwaza sana hasa nilipokuwa nikitazama kombe la dunia hii leo kule Qatar.

Shida hivi ipo wapi kwa nchi za kiafrica? Kwann kila kitu kibaya ni Africa? Uongozi, tunalalamikiana Africa, Sayansi na teknolojia tupo nyuma zaidi ya sana nahisi ndo wa Mwisho kabisa, michezo ndo usiseme, Afya na Miundombinu ni shida tupu.

Shida nini Africa mbona kila siku huwa tunajinadi kuwa Africa tumejaliwa kila kitu na Mungu kwann sisi ndo tunaonekana Ovyo kabisa kwenye kila nyanja ukifananisha na mabala mengine?
 
Tatizo siyo afrika tatizo ni fikra na mtazamo wako.

Tatizo Mnataka Tufanane tufanye kama wao kwani ni lazima

Kwani ni lazima tucheze soka.

Kwani Kupata nafasi ya kujitangaza kimataifa na kuacha alama hapa Duniani lazima. Tufanane na wao.

Tufanye mambo yetu kivyetu .. ova
 
Habari gani ndugu wananchi?
Kuna jambo limeliwaza sana hasa nilipokuwa nikitazama kombe la dunia hii leo kule Qatar.

Shida hivi ipo wapi kwa nchi za kiafrica? Kwann kila kitu kibaya ni Africa? Uongozi, tunalalamikiana Africa, Sayansi na teknolojia tupo nyuma zaidi ya sana nahisi ndo wa Mwisho kabisa, michezo ndo usiseme, Afya na Miundombinu ni shida tupu.

Shida nini Africa mbona kila siku huwa tunajinadi kuwa Africa tumejaliwa kila kitu na Mungu kwann sisi ndo tunaonekana Ovyo kabisa kwenye kila nyanja ukifananisha na mabala mengine?
Uongozi mmbovu kama wa CCM.
 
Ngozi nyeusi tumebarikiwa nguvu za kimwili kuliko race nyingine, ila tumenyimwa akili kuliko race nyingine.

Kwani wengine hawana hizo nguvu, basi Si utumie hizo nguvu zako za "kimwili" kujiletea maendeleo i!!
 
Habari gani ndugu wananchi?
Kuna jambo limeliwaza sana hasa nilipokuwa nikitazama kombe la dunia hii leo kule Qatar.

Shida hivi ipo wapi kwa nchi za kiafrica? Kwann kila kitu kibaya ni Africa? Uongozi, tunalalamikiana Africa, Sayansi na teknolojia tupo nyuma zaidi ya sana nahisi ndo wa Mwisho kabisa, michezo ndo usiseme, Afya na Miundombinu ni shida tupu.

Shida nini Africa mbona kila siku huwa tunajinadi kuwa Africa tumejaliwa kila kitu na Mungu kwann sisi ndo tunaonekana Ovyo kabisa kwenye kila nyanja ukifananisha na mabala mengine?
Why uchukue Cha mtu ukidhani ndiyo chema na kuanza kulaumu motherland yako? Kila mmoja ataishi awwzavyo na usitamani mafanikio ya wengine, any way ngoja nikutie moyo, inawezekana iwapo... -

[emoji116]
1. Africa ingekua moja na si hii mipaka ya tunchi tudogo na masikini kama Burundi

2. Elimu iliyojaa misingi ya kiAfrka

3. Fedha ya pamoja

4. Lugha moja

5. Malengo mamoja mpaka tukae nao mezani wakiomba tufanye nao biashara, yamkini dhahabu, Almasi na mengine, hapa tungekua na timu moja huko Qatar inayotoka nchi ya Africa la yamkini ingesumbua sana.

Labda umeelewa kidogo
 
Siku ukibadili mtazamo wako utaona tuko nyuma kwa sababu unatumia scales za Hao Hao unaoona wanatuzidi.
. Wazungu walikuja wakakuta sisi tuna mila zeru, tuna tamaduni zetu tuna dawa zetu za asili na maisha yanaenda poa kabisa wakatu convince kuwa haya yetu ni ushenzi na ya kwao ndo standard, tukaona hivyo sasa unataka kwenye kuyatekeleza ya kwao tuwashinde, Kweli?

. Wazungu walikuja wakakuta tuna demokrasia zetu na namna yetu ya kutawalana wakaita hii yetu ni ya kishenzi na wakatifundisha mashuleni kuiishi demokrasia yao maana ndo nzuri tukageuka na kujifunza yao, sasa unataka sisi tuliyojifunza na wao ni mtindo wao wa maisha tuwashinde, kweli?

. Wazungu walikuja wakasema lugha yetu ni uzushi na mtu mstaarabu anaongea lugha kama yao tukaamua kujifunza yao, unataka tuwashinde, kweli?

. Hebu chagua kitu kimoja ambacho sisi ni asili yetu na wao wanaiga kutoka kwetu alafu Pima Nani anakifanya kwa weledi zaidi

Mkuu, ni bahati mbaya Sana akili zetu zimefundishwa kufikiri mambo ya wazungu na Wageni ni bora kuliko yetu na yetu ni ya kishenzi. Na bahati mbaya zaidi mnayatumia mambo ya wageni na tamaduni zao kulinganisha aliyeko mbele na aliyeachwa nyuma!
 
Sisi ni wa mwisho kwasababu tumeacha njia zetu za maisha na kuiga njia zao ambazo hatuzielewi. Mfano mmoja japo ni wa kijinga ni sawa nchi zetu kuwekeza kwenye madini wakati hatujui cha kuyafanyia zaidi ya kuwauzia wao. Wakisema hawayataki tutabaki kuyachezea kama goroli. Then leo unajiuliza kwanini wao wanaongoza kwa utajiri wa madini wakati wanayatoa kwetu!! Jibu ni kwasababu wao ndiyo walianza kuyapa thamani kabla yetu so hapo hakuna la ajabu
 
Race nyingine ni kama walikua ahead of time wametumanipulate sisi kila kitu misingi yake tumewekewa na wao kwahio hatuwez kutoka kwenye vivuli vyao tukipga hatua 100 wao watakua na 1000
 
Ngono ngono ngono...mawazo yote mmelekeza huko...hakuna mgunduzi (whites) aliyepata kuwa serious na ngono..anzia Kwa Newton mpaka akina da Vinci...hawajawai hata siku Moja kudili na madem
Ngono ni kwa mataifa yote na viumbe hai vyote kwa namna yake.
Kila jambo kwa wakati wake.
Unataka uandikiwe Isaac Newton alifanya ngono mara ngapi?
Hizi fikra ni sehemu ya changamoto ya kushughulikia.
 
Back
Top Bottom