Artifact Collector
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 6,617
- 10,205
Unafikiri sawa sawa mtu ametoka huko ulaya amekukuta unachezea madini bao unafikiri mko nae sawaSiku ukibadili mtazamo wako utaona tuko nyuma kwa sababu unatumia scales za Hao Hao unaoona wanatuzidi.
. Wazungu walikuja wakakuta sisi tuna mila zeru, tuna tamaduni zetu tuna dawa zetu za asili na maisha yanaenda poa kabisa wakatu convince kuwa haya yetu ni ushenzi na ya kwao ndo standard, tukaona hivyo sasa unataka kwenye kuyatekeleza ya kwao tuwashinde, Kweli?
. Wazungu walikuja wakakuta tuna demokrasia zetu na namna yetu ya kutawalana wakaita hii yetu ni ya kishenzi na wakatifundisha mashuleni kuiishi demokrasia yao maana ndo nzuri tukageuka na kujifunza yao, sasa unataka sisi tuliyojifunza na wao ni mtindo wao wa maisha tuwashinde, kweli?
. Wazungu walikuja wakasema lugha yetu ni uzushi na mtu mstaarabu anaongea lugha kama yao tukaamua kujifunza yao, unataka tuwashinde, kweli?
. Hebu chagua kitu kimoja ambacho sisi ni asili yetu na wao wanaiga kutoka kwetu alafu Pima Nani anakifanya kwa weledi zaidi
Mkuu, ni bahati mbaya Sana akili zetu zimefundishwa kufikiri mambo ya wazungu na Wageni ni bora kuliko yetu na yetu ni ya kishenzi. Na bahati mbaya zaidi mnayatumia mambo ya wageni na tamaduni zao kulinganisha aliyeko mbele na aliyeachwa nyuma!
Mtu amekuja amekuchukua na kukuuza unafikiri ulikua naye sawa, mwafrika ni mtu dhaifu kuliko race zote sababu kubwa ni uwezo mdogo wa kutumia akili