Kwanini Barabara mpya kwa Jiji la Dar es Salaam zinajengwa kwa njia 4?

Cha kusikitisha hata njia muhimu sana ya kuelekea International Airport, reception ya Taifa inajengwa njia 4, tena finyu likitangulua roli huwezi kuliovertake!!! Hakuna vituo vya daladala, inasikitisha sana, viongozi wetu wana matatizo makubwa sana.ukiangalia njia kuelea Airport nafasi kubwa bado ipo pembeni!!! yakutosha kabisa,

Sitashangaa baadaye itabomolewa tena kuitanua.
 
Wanafanya hivyo mikaka michache ijayo wapige tena.

Kwani world bank si watu kama watu wengine? Unafikiri hakuna wapigaji mule?
Nakubaliana na wewe kabisa dada yangu.

Kutakuwa na upigaji mkubwa sana kuanzia kwa hao wataalam wa World Bank hadi kwa watu wetu. Ndo mana pale jangwani palipojengwa kituo cha Mwendokasi miaka michache tu iliyopita leo kimetolewa alafu linatengwa daraja

Maana kusema kweli haiingii akilini kabisa.
 
Nimepita juzi ndo hadi nimetaka kutoa machozi. Kwa namna ile njia ilivyo na nafasi pembeni alafu unaona watu wanajenga njia 4 unakubali kabisa acha wazungu watuite manyani
 
Labda afufuke magufuli ndiyo zijengwe hizo 6 to 8
 
Kuondoa msongamano au foleni ya magari ni kitu kinachohitaji combination ya vitu vingi. Unaweza kuweka hata barabara nane au kumi na ukazidisha tatizo badala ya kuongeza. Kujenga barabara nne kukiambatana na hatua nyingine kunaweza kuleta ufanisi zaidi badala ya kung'ang'ania tu kwenye barabara.
 
Upo sahihi kabisa. Ila suala la kujenga barabara kuu pana haliepukiki katika dhana ya kuondoa foleni kwenye miji mikubwa pamoja na kurahisisha shughuli za maendeleo
 
"imejengwa barabara mpya kabisa kutoka mbagala hadi posta ila bado imejengwa kwa njia 4( mbili kwenda na mbili kurudi na katikati mwendokasi)."

2 kwenda+2 kurudi+mwendo kasi =6.

Kwanini upate 4? Kwani mwendo kasi siyo barabara?

Bado kuna treni ya Mwakyembe

Hata Kivukoni-Kibaha ni njia 6 hadi 8.

Mbagala Posta ni njia 6.

Njia ya kwenda Pugu ni 6.
 
Rudi shule
 
Ndio shida ya kuwapa uongozi wa nchi makada na wapiga debe wa chama.
 

sasa kwa dargiza uwe na barabara 8 za kwenda wapi na ktkea wapi? dargiza asubuhi watu wote wanaenda posta/kariakoo jioni wanarudi sasa ulitaka barabara 10 kuingia posta?
 
Huko world bank ndiyo kuna upigaji mkubwa kuliko kokote.
 
sasa kwa dargiza uwe na barabara 8 za kwenda wapi na ktkea wapi? dargiza asubuhi watu wote wanaenda posta/kariakoo jioni wanarudi sasa ulitaka barabara 10 kuingia posta?
Tafuta exposure ndugu
 
Ndio shida ya kuwapa uongozi wa nchi makada na wapiga debe wa chama.
Kusema kweli wanaturudisha nyuma sana. Wanafanya watu weusi tudharauliwe sana kwa kuwa tunaonekana kama thinking capacity zetu zina mushkeli
 
Tafuta exposure ndugu

haujajibu swali langu, barabara za njia 10 dargiza kwenda wapi na kutokea wapi? hiyo miji mingine ya nje wameplan vizuri na miji ina centers nyingi sasa dar kila mtu asubuhi ankwenda posta jioni anarudi, ofisi zote ziko posta hizo njia nane zitapitia wapi na kutoka na kuelekea wapi? nenda hata nairobi tu hapo utaona mji una center mbalimbali angalau, sasa dargiza wote wanafurika posta watapaki wapi hayo magari?
 
Barabara ya kwenda bandarini kutokea Ubungo kupita Buguruni na Tazara haina foleni?

Kwenda Kimara from Ubungo hakuna foleni?

Kwenda ubungo from Mwenge hakuna foleni?

Hizo nazo zinaenda Posta?

Unaishi Dar kweli au unahadithiwa kuhusu Dar?
 
Njia nane Kwa eneo lipi bongo mkuu,Hilo la nne lenyewe wamepata Kwa jasho,watu kuvunjiwa makazi na kipigo juu.Dar imejaa,dar inafukuta imefurika watu wengi wasio na ajira na wengi ni wale watuma Kwa namba hii,Nashauri Dar ipunguzwe wengine wapelekwe kulima bush
 
Kama njia ya Shekilango- Bamaga imewezekana kutoa njia 4 unashindwaje kuweka njia 6-8 barabara ya mbagala- Posta? Au Bunju- Posta? au Mwenge - Ubungo- Kurasini? au Posta- Pugu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…