Kwanini Barabara mpya kwa Jiji la Dar es Salaam zinajengwa kwa njia 4?

Kwanini Barabara mpya kwa Jiji la Dar es Salaam zinajengwa kwa njia 4?

Hakuna na bajeti ni uvivu wa kufikiri. Miradi hii inajengwa kwa fedha za mikopo sasa kwa nini tusikope fedha za kutosha na tukafanya jambo kwa kumaliza kabisa? Unaweza kuta baada ya miaka 4-5 unasikia wanaongeza ukubwa tena wa barabara ile ile waliyojenga.
Wakimaliza tatizo watakula wapi wakati wanawaza kuiba tu,,,ni sawa uende Kwa mganga eti akutibu upone kabisa wakati matatizo yako ndiyo faida yake tuendelee kula mtori nyama ziko chini😜
 
Kipimo cha uwezo wa mwanadamu kama anafikiri sawasawa ni namna anavyofanya mambo yake kulingana na wakati husika.

Dar es Salaam ndo Jiji Kuu la Biashara la Tanzania. Sio hivyo tu, ndo Jiji lenye watu wengi zaidi Tanzania na kadri siku zinavyozidi kwenda idadi ya watu inazidi kuongezeka.

Kwa binadamu ansyefikiri sawasawa, sikutegemea kama katika karne hii ya 21 tena mwaka 2023 kwenye Jiji hili barabara kuu zingeendelea kujengwa kwa njia 4.

Nipo Dar es Salaam na nimesikitishwa sana maana imejengwa barabara mpya kabisa kutoka mbagala hadi posta ila bado imejengwa kwa njia 4( mbili kwenda na mbili kurudi na katikati mwendokasi). Nimetembea pia njia ya kutoka Posta hadi Uwanja wa ndege nimeona ujenzi unaendelea na hali ni hiyo hiyo.

Swali langu kwenu Viongozi wa Tanzania. Je uwezo wenu wa kufikiri ndo umeishia hapo?

Kwa namna Jiji hili lilivyo na linavyotakiwa kuwa yaaani kama Jiji bora na la mfano Afrika Mashariki na Kati, nilitegemea barabara hizi kujengwa kwa Njia 6 hadi 8 pamoja na mwendokasi.

Kiufupi barabara zote kubwa za Dar zinazoingia Posta kuelekea Kibaha, Pugu, Mbagala, Bunju na inayotoka Morroco hadi Keko bila kusahau ya Mwenge- Ubungo hadi Bandarini zinatakiwa kuwa za njia 3 mpaka 4 kila upande na njia ya mwendokasi/ treni ya umeme katikati.

Ifike wakati nchi hii watu tufikiri kama tunaishi katika dunia wanayoishi wenzetu warabu na nchi za ulaya. Inasikitisha sana kuwa na mipango ya mwaka 1950/ 60 katika karne hii ya 21.

Naomba Viongozi wa Tanzania mbadilike kwa kweli.
Ujengaji wa miundo mbinu huendana na 40% sasa wakijenga leo barabara zote then baadae 40% watapata wapi?

Kuimba kupokezana acha leo wajenge mbili ikizinduliwa mpige makofi, 40% wale, then baadae mkilia sana itaongezwa moja jumla ziwe tatu then 40% iliwe.

Baadae wanao wakilia then kizazi cha akina Qylallah nacho ndo kitafikisha ya 4 then na 40 na wao watakula🤣😆😂.
 
Haiingii akilini kabisa. Njia 4 tungejenga njia za ndani kubwa kama ilivyo barabara ya Shekilango ila Barabara kubwa zote za Dar es Salaam zitakiwa kuwa njia 6 hadi 8 pamoja na barabara ya mwendokasi katikati.
Yaani nyie watu wa bongo lala mnataka njia sita nane wakati huku kwetu jiji la miamba hata njia mbili tu tia maji tia maji daah 🤔
 
Back
Top Bottom