Kwanini BBC hawaonyeshi live genocide case Afrika Kusini dhidi ya israel?

Kwanini BBC hawaonyeshi live genocide case Afrika Kusini dhidi ya israel?

Ungetazama kupitia Aljazeera mkuu,kesi ni ngumu sana kwa Israel. Tuwashukuru makafir wenzetu toka South Africa kwa kuwatetea wapalestina.
Kesi imemkalia vibaya israel kuchomoa labda utumike ubabe wa maswahiba zake.
 
Bbc kesho akibrodcast utetezi wa kina netanyahu, litakua suala la muda tu bbc kufata nyayo za cnn
 
Hayo maswali yanahusiana vipi na swali langu.
Nimeona raia wa nchi za Afrika wengi wanajipa umuhimu kwenye mashirika ya habari ya nchi za magaharibi, kutaka yaripoti hivi au vile, bila kujua ama kujali mambo niliyoyaorodhesha hapo chini.

Kwenye mashirika ya kiserikali, matakwa haya yanakosa nguvu zaidi.

Kwa sababu:-

1. Mashirika hayo yanaendeshwa kwa kodi za wananchi wa hizo nchi.

2. Mashirika hayo hayalazimiki kuripoti habari zozote ambazo hayataki kuripoti kwa mujibu wa interests za nchi zao.

3. Ni wananchi wa nchi hizo tu, wanaolipia kodi zinazoendesha mashirika hayo, ndio wana haki ya kuyataka mashirika hayo yaripoti nini na vipi.

4. Ikiwa mashirika hayo yatasikiliza maoni ya watu wasio raia wa nchi hizo, hilo ni kwa ukarimu na utashi wa hayo mashirika tu.

5. Ikiwa matakwa ya watu wasio raia wa nchi hizo yatagongana na matakwa ya raia wa nchi hizo, matakwa ya raia wa nchi hizo yatashinda.

Raia wa Afrika, badala ya kulalamikia vyombo vya magaharibi havifanyi hivi na vile, wajikite kuanzisha vyombo vyao vitakavyoripoti habari wanazotaka wao.

Ama sivyo, watakuwa wanafanya sawa na kwenda nyumbani kwa watu, halafu wao wageni wanawalazimisha wale wenyeji wao wapike wanavyotaka wao wageni, watumie viungo hivi na vile, hata kama wale wenyeji wao hawataki.

By the way, mimi nasikiliza BBC World Service wanafanya live coverage ya hii case.

BBC wana habari nyingi hawawezi kusimamisha habari zote ku cover habari unayotaka wewe, muda unaotaka wewe, kwa style unayotaka wewe.
 
Bbc kesho akibrodcast utetezi wa kina netanyahu, litakua suala la muda tu bbc kufata nyayo za cnn
Tatizo Waafrika mnakaa sana kufuatilia BBC na CNN wanaripoti vipi habari, badala ya kuanzisha vyombo vyenu vya habari mripoti mambo mnavyotaka nyinyi.

Kwa nini mnakuwa hivyo?

Kwa nini mnataka vyombo vya habari vya watu wengine viripoti mambo mnavyotaka nyie, badala ya nyie kuanzisha vyombo vyenu mkaripoti mnavyotaka wenyewe?

Kama Mmarekani ana chombo chake cha habari kinatoa kipaumbele kwenye habari za kesi za Trump na uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024 kuliko kesi ya South Africa dhidi ya Israel, kwa sababu demographics za watazamaji wake ndio wanaona kipaumbele hivyo, wewe Mtanzania unajiona vipi una haki ya kuwapangia Wamarekani habari gani ni muhimu na gani si muhinu?

Wamarekani wana VOA, Waingereza wana BBC, Wafaransa wana RFI, wa Canada wana CBC, wa Japan wana NHK, wa Jerumani wana DW, wa Qatari wana Al-Jazeera, wataliani wana RAI, wa Rusi wana RT, wa Hindi wana Prasar Bharati,

Nyie Waafrika mna nini?

Nyie wa Tanzania mna nini?
 
Vyombo vyote vikubwa vya habari vinaonyesha live kesi inayoendelea genocide case iliyofunguliwa na serikali ya Afrika kusini dhidi ya Israeli lakini BBC ni kama hawajui kinachoendelea kwa sasa.
Wacha tuwaombe TBC waionyeshe live
 
Mambo mengine ni kulaumu tu bila kujua.

BBC ni Public broadcaster wa Waingereza hivyo priority Yao iko kwa Waingereza kwanza.

Wiki hizi mbili UK kuna scandal kubwa sana inaendelea wa wafanyakazi wa Posta ambao walifungwa kwa wizi kumbe shida ilikuwa software.

Sasa leo kuna public inquiry ndio imeanza tena leo na mhusika mkuu ndio anatoa ushahidi. Kwahiyo karibu vyombo vyote vya habari vya Uingereza vimeelekeza nguvu huko.

Hata shughuli nyingi za serikali zinesimama ili waziri mkuu na mawaziri wengine kutoa muda wa kutosha kushughulikia scandal hii na kuhakikisha wote waliofungwa wanaachiwa na kulipwa fidia.
Wenzetu wapo mbele sana kwenye haki
 
Wenzetu wapo mbele sana kwenye haki

Kwanini mnapenda kushoboka kwa kuwaita "wenzetu" wakati wao hawajawahi kuwaita nyie wenzao hata kwa bahati mbaya?
 
Kwanini mnapenda kushoboka kwa kuwaita "wenzetu" wakati wao hawajawahi kuwaita nyie wenzao hata kwa bahati mbaya?
Utumwa sio mchezo mkuu...pingu ziliwatoka mikononi na miguuni ila KICHWANI bado bongo zimefungwa hatar
 
Tatizo Waafrika mnakaa sana kufuatilia BBC na CNN wanaripoti vipi habari, badala ya kuanzisha vyombo vyenu vya habari mripoti mambo mnavyotaka nyinyi.

Kwa nini mnakuwa hivyo?

Kwa nini mnataka vyombo vya habari vya watu wengine viripoti mambo mnavyotaka nyie, badala ya nyie kuanzisha vyombo vyenu mkaripoti mnavyotaka wenyewe?

Kama Mmarekani ana chombo chake cha habari kinatoa kipaumbele kwenye habari za kesi za Trump na uchaguzi wa rais wa Marekani wa 2024 kuliko kesi ya South Africa dhidi ya Israel, kwa sababu demographics za watazamaji wake ndio wanaona kipaumbele hivyo, wewe Mtanzania unajiona vipi una haki ya kuwapangia Wamarekani habari gani ni muhimu na gani si muhinu?

Wamarekani wana VOA, Waingereza wana BBC, Wafaransa wana RFI, wa Canada wana CBC, wa Japan wana NHK, wa Jerumani wana Deutschewelle, wa Qatari wana Al-Jazeera, wataliani wana RAI, wa Rusi wana RT, wa Hindi wana Prasar Bharati,

Nyie Waafrika mna nini?

Nyie wa Tanzania mna nini?
Walioipuuza cnn majority ni waamerica wenyewe, kwenye global stage mainsteram media inapata malalamiko mengi ya bias-ness ya coverage, namimi nimetoa mawazo yangu tu.

Japo hoja uliyoandika hapo hata mimi hua nalia nayo kila siku kama ulivoandika wewe mkuu

Swali je nini kifanyike
 
Vyombo vyote vikubwa vya habari vinaonyesha live kesi inayoendelea genocide case iliyofunguliwa na serikali ya Afrika kusini dhidi ya Israeli lakini BBC ni kama hawajui kinachoendelea kwa sasa.
Wanapambana na TB Joshua,mengine hawayajui
 
Walioipuuza cnn majority ni waamerica wenyewe, kwenye global stage mainsteram media inapata malalamiko mengi ya bias-ness ya coverage, namimi nimetoa mawazo yangu tu.

Japo hoja uliyoandika hapo hata mimi hua nalia nayo kila siku kama ulivoandika wewe mkuu

Swali je nini kifanyike
CNN inajiendesha kibiashara bado. Marekani imegawanyika sana, hakuna kitu kinachokubalika na Wamarekani wote. Hata bendera ya nchi tu raia wengine wanataka kuichoma.

So, hayo ya CNN kama huipendi usiangalie, the forces of the market will speak. Mbona Al Gore alianzisha network yake ya TV na redio ikashindwa kupata watu akaifunga?

Kwenye hoja ya nini kifanyike, chukua jukumu mwenyewe kuanzisha kitu.

Si lazima uanzishe chombo cha habari, au uwe mwanahabari, unaweza hata kuanzisha pressure group ya grassroots level itakayodai mambo fulani kwenye habari tu. Hususan kwenye vyombo vya nchi yako au vinavyolipiwa kwa kodi yako.

Kabla ya Millard Ayo, uanahabari wa aina ya Millard Ayo ulikuwa haupo na wala haukuonekana kama unawezekana. Millard Ayo kajilipua, kaanzisha kitu, kafanikiwa kiasi chake.

Muandishi wa habari wa Kiingereza aliyehamia Marekani, Christopher Hitchens, aliona kuwa kila habari ya vita anayoifuatilia haiandikwi vizuri vile anavyotaka yeye.

Akatumia falsafa ya Kiingereza "If you want something done well, do it yourself". Christopher Hitchens akajitumbukiza katika uandishi wa habari za vita. Akaja kuwa muandishi maarufu anayeheshimiwa sana mpaka anafariki.

Je, sisi tunaangalia mapungufu kama fursa ya kuanzisha kitu kipya? Au tunawalalamikia wengine wafanye tu, sisi tuwe watumiaji tu?

Sisi Waafrika wengi tatizo letu ni kutaka mtu mwingine afanye kazi, sisi tufurahie matunda tu.

Kuanzia mtu binafsi mpaka serikali zetu collectively.

Ndiyo maana maendeleo magumu. Kila mtu anamtegea mwenzake majukumu, na wananchi wanaitegea serikali, na serikali inawategea wananchi. Matokeo yake majanga, halafu tunamtafuta mchawi wetu ni nani? Tunawalaumu CNN na BBC hawaripoti habari tunavyotaka sisi, bila aibu.

Ulishawahi kumsikia Muingereza anailalamikia TBC hairipoti habari za umuhimu kwa watu wa Northumberland County, opioid crisis yao huko, anavyotaka yeye?

Tunataka CNN aripoti hivi, tunataka BBC aripoti hivi, hatujui hata gharama za kuripoti hivyo ni zipi, hatujui hata prioroties za demographics za vyonbo hivyo ni zipi.

Mtu anataka BBC ikatishe programs zake ioneshe kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel live, hata hajui kipaumbele cha BBC, hajui gharama, hajui kwamba BBC wanafanya hourly updates za hiyo habari. Yeye anataka kuwalazimisha tu waripoti live, kwa masaa anayoyataka yeye.

Hata huyo mlipa kodi wa Uingereza mwenyewe anaye i fund BBC hana privilege hiyo.

Africa tutengeneze siasa zetu, tutengeneze chumi zetu, haya mambo yatakuja kukaa vizuri tu. Kwa sasa hivi, sababu za kiuchumi na kisiasa tu zitazuia Africa kuwa na vyombo imara vya habari. Hata ukiwa na hela useme unataka kuanzisha CNN ya Afrika, siasa za Afrika hazitakuruhusu. Atatokea mwanasiasa atataka umfanye yeye awe habari siku zote hata kama anachofanya hakina umuhimu wala mvuto wa kuwa habari. Wenzetu wana autonomy kwa kiasi kikubwa katika habari.

So, you have to fix the politics first, then fix the economies, from there, demand ikiwepo, industry itatoa tu supply ya news networks kubwa.

News ni biashara, huwezi kuwa na vyombo vya habari vyenye nguvu katika nchi ambazo hazina siasa na chumi madhubuti.
 
Vyombo vyote vikubwa vya habari vinaonyesha live kesi inayoendelea genocide case iliyofunguliwa na serikali ya Afrika kusini dhidi ya Israeli lakini BBC ni kama hawajui kinachoendelea kwa sasa.
*Gaza has been reduced to rubbles due to Hamas militants' mischievous monster acts toward others resulting in innocent civilians being inflicted with collective punishment by the rivals, whilst the malicious group leaders enjoy a haven life underground the metro tunnels!!!
 
Back
Top Bottom