Nimeona raia wa nchi za Afrika wengi wanajipa umuhimu kwenye mashirika ya habari ya nchi za magaharibi, kutaka yaripoti hivi au vile, bila kujua ama kujali mambo niliyoyaorodhesha hapo chini.
Kwenye mashirika ya kiserikali, matakwa haya yanakosa nguvu zaidi.
Kwa sababu:-
1. Mashirika hayo yanaendeshwa kwa kodi za wananchi wa hizo nchi.
2. Mashirika hayo hayalazimiki kuripoti habari zozote ambazo hayataki kuripoti kwa mujibu wa interests za nchi zao.
3. Ni wananchi wa nchi hizo tu, wanaolipia kodi zinazoendesha mashirika hayo, ndio wana haki ya kuyataka mashirika hayo yaripoti nini na vipi.
4. Ikiwa mashirika hayo yatasikiliza maoni ya watu wasio raia wa nchi hizo, hilo ni kwa ukarimu na utashi wa hayo mashirika tu.
5. Ikiwa matakwa ya watu wasio raia wa nchi hizo yatagongana na matakwa ya raia wa nchi hizo, matakwa ya raia wa nchi hizo yatashinda.
Raia wa Afrika, badala ya kulalamikia vyombo vya magaharibi havifanyi hivi na vile, wajikite kuanzisha vyombo vyao vitakavyoripoti habari wanazotaka wao.
Ama sivyo, watakuwa wanafanya sawa na kwenda nyumbani kwa watu, halafu wao wageni wanawalazimisha wale wenyeji wao wapike wanavyotaka wao wageni, watumie viungo hivi na vile, hata kama wale wenyeji wao hawataki.
By the way, mimi nasikiliza BBC World Service wanafanya live coverage ya hii case.
BBC wana habari nyingi hawawezi kusimamisha habari zote ku cover habari unayotaka wewe, muda unaotaka wewe, kwa style unayotaka wewe.