Kwanini BBC hawaonyeshi live genocide case Afrika Kusini dhidi ya israel?

umejimix sana kiranga, hoja sio kama huna kabisa hapana hoja ipo ila uwasilishaji wako mimi naona sio sahihi kwa hoja niliyoitoa. Maana sio kwamba coverage haikupatikana maana hata sky news wamebroadcast.

Point kubwa wanalalamikiwa na wengi sio mimi tu
 
Nimejimix wapi? Kivipi?

Nakwambia cha mtu mavi, anzisha chako, ukiendeshe unavyotaka wewe.

Mtegemea cha ndugu hufa masikini.

Nilipojimix wapi?

Hoja kusemwa na wengi hakuifanyi kuwa sahihi. Kufikiri wingi ndio usahihi ni logical fallacy, inaitwa "appeal to populism".
 
kiranga wewe una mainstream media?
 
Nionavyo mimi ni kwamba vyombo vikubwa vya habari vya nchi za magharibi vinajitahidi kuilinda taswira ya Israel mbele ya jamii zao ili isipoteze kuungwa mkono . Reporters wao wapo imbeded na jeshi la Israel kwenye vita kule Gaza,taarifa lazima zipewe green light na Israel ndipo zirushwe hewani.

Naifutilia sana BBC na CNN,wakati wa vita ya Russia/Ukraine jamaa walikua kwenye battlefield,wanahoji wahanga,kuonyesha majeruhi na uharibifu mkubwa. Wakielezea ukatili wa Russia vitani,hii ilikua kampeni ya ku-boost support kwa Ukraine kwa raia wao ili misaada ya silaha na pesa isiwe na vikwazo.

Leo mauaji ya kutisha ambayo Israel imefanya ndani ya muda wa miezi mitatu ni makubwa kuliko ya vita vya Russia/Ukraine vya miaka miwili . CNN, BBC na wengineo vichwa vya habari na habari zao kamili ni kuhusu Israel victimhood, Israel can do no wrong in their eyes.

Kesi ya leo hawajarusha live kwa sababu ingeathiri taswira ya Israel mbele ya raia wao,ule ni mtaji ambao Israel haitakiwi kuupoteza .
 
ANakaza akili tu huyo
 

Naweza kusema kuwapangia BBC warushe nini live na wasirushe nini live si sawa.

Kwamba hata wakitoa hourly updates wamefanya coverage pia.

Lakini hata nisiposema hivyo.

Fine.

BBC wako biased tuseme.

Anzisheni vyenu basi mrushe mnavyotaka.

Kwa nini mnataka BBC wafanye mnavyotaka nyie Watanzania wakati this is the British Broadcasting Corporation, not the Tanzanian Broadcasting Corporation?

Mbona hamuwaambii Tanzania Broadcasting Corporation wafanye hiyo live coverage mnayotaka, mnawaambia BBC waifanye?
 
Kila la kheri mkuu
Umeanzisha hoja ambayo hata ku define terms huwezi?

Au unafikiri watu wanapaswa kukubaliana tu "mainstream media" ni nini bila hata ya definition?

Au unarusharusha tu hayo maneno "mainstream media" bila hata wewe mwenyewe kujiuliza na kuelewa unamaanisha nini unavyosema "mainstream media"?
 
Kubishana na wewe sitaweza mkuu, nimetupa taulo jeupe mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…