Kwanini benki hakuna vyoo/maliwato kwa ajili ya wateja?

kakamukubwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
203
Reaction score
27
BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyoo vya wateja.
Kwanini?
---
---
Waziri mwenye mamlaka,asikie kilio chetu.
Vyoo ni muhimu sana bank,unakuta umepewa mkwanja mrefu tu na Bi mkubwa anakwambia nipelekee bank nifate mzigo, sasa ukibanwa na tumbo lzm utafute public toilet kitu kinachohatarisha usalama wa pesa
---
---

===
BAADHI YA MAJIBU YALIYOTOLEWA NA WADAU

---
-----
Niliwahi kusikia kuwa ni masuala ya kiusalama zaidi.
Kukiwa na choo wateja wezi / majambazi wanaweza kutumia eneo hilo (choo) kwa kubadirishia sura (kuvaa vinyago) na au kuweka siraha zao sawa humo msalani.
(hapa najiongeza).
---
---
---
 
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyø vya wateja.
Kwanini?

Ndo mazoea ya Watanzania. kama shule zinakosa vyoo iwe benki? hakuna miongozo mizuri ya kusimamia utoaji huduma wa kirafiki kwa mteja.
 
Ni kwa ajili ya security!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hili swali nimetumiwa kwenye sms kwa jina la "jahazi" Anyways, ushawahi kuulizau umefuatilia kimykimya?
 
Vyoo vipo unadhani wafanyakazi wanapata huduma zao wapi? Ukibanwa na kuuliza unapata huduma si lazima waandike vyoo vya wateja.
 
Nimefatilia Muda mrefu sana na kubaini kuwa ni karibu Bank zote hazina vyø vya wateja.
Kwanini?
Ulishawahi kujiuliza ni kwa nini sisi wateja tunaziamini sana bank zote na kuweka hela (pengine hata mamilioni ya hela) zetu kwao ila wao hawatuamini hata chembe kiasi kwamba hata kalamu(pen) wanazifunga kamba. Hii imekaaje?

Tukazitoe hela zetu wao hawatuamini hata kidogo!
 
Ila kunapaswa kuwepo vyoo kwa ajili ya wateja kwani bank zingine unakaa sana kupata huduma. Hivyo ni busara kuwa na vyoo vya wateja, hiyo sababu ya ulinzi mimi bado sijaiona kuwa imekaa vizuri kwani wanapoingia hapo ndani ya bank kufanya huduma hawawezi kuhatarisha huo usalama?
 
Ni kwaajili ya security!

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Tiririka Mkuu, funguka tujuze, sababu za kiusalama kivipi?!!!, si lazima vyoo viwe ndani ya bank, nadhan hata vikiwa nje, let say jirani na sehemu wanyokaa walinzi wa nje! Pia nimuhimu kuandika huduma ya choo ili watu wajue inapatikana upande upi, nijuavyo mimi hii ni huduma muhimu sana!

Halafu si kweli kuwa wateja hawakai muda mrefu, nakumbuka nilispend 4 hrs NMB Temeke sudan just kudraw hela, nilikuwa nahitaji kiwango zaidi ya kile cha kutoa kwa ATM! Binafsi naona haja ya kuwa na sheria ya kulazimisha bank ziwe na vyoo kwa ajili ya wateja!!
 
Benk nyingi zimepanga kwenye majengo ambayo sio yao, na kwa jinsi majengo hayo yalivyojengwa kuna vyoo tayari vipo kwa ajili ya watumiaji wote wa jengo au ghorofa husika, kwa hiyo ukiulizia watakuonyesha tu.

Sio rahisi kuwepo ndani ya bank maana chumba chenyewe cha bank hudesigniwa baada ya jengo kuwa lishakamilika.
 
Ha ha haaaa dah!! Ni hivi kwa habari ya kalamu, inafungiwa kamba kwasababu wateja wengi mara kadhaa hutembea bila kalamu, basi ile kalamu isipofungiwa kamba wengine tunaweza kujisahau na kuibeba akija mteja mwingine, atatumia nini? ile ni "public" pen mdau...
 
Je, hili ni tatizo kwa bank za Tanzania pekee? What about our neighbouring contr and abroad?
 
Heshima yenu wakuu,

Moja ya sehemu zenye msongamano mkubwa wa watu ni benki lakini cha kushangaza ni kukosekana kwa huduma muhimu ya choo kwa wateja.

Na kama vyoo vipo basi vimejificha sana na ni maalum kwa wafanyakazi wa benki. Hawa jamaa walione hili ni kero kwa wateja hasa siku ambazo kuna foleni humo.

c.c: Patrickn
 
Last edited by a moderator:
Niliulizaga hili nikajibiwa nikiwa naenda bank natakiwa niwe nimemaliza haja zangu zote!

Unaweza kuchafukwa na tumbo muda wowote au ukabanwa na mkojo muda wowote, benki zenyewe wateja wanakaa katika foleni masaa kibao.
 
Waziri mwenye mamlaka, asikie kilio chetu. Vyoo ni muhimu sana bank,unakuta umepewa mkwanja mrefu tu na Bi mkubwa anakwambia nipelekee bank nifate mzigo, sasa ukibanwa na tumbo lazima utafute public toilet kitu kinachohatarisha usalama wa pesa.
 
Sijawahi kuona bank yenye choo, i have been around a bit.


The King.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…