Kwanini bidhaa za China zina gharama nafuu katika soko la dunia? Sababu sio cheap labour kama wengi wanavyodhani

Kwanini bidhaa za China zina gharama nafuu katika soko la dunia? Sababu sio cheap labour kama wengi wanavyodhani

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Kuna maoni kutoka wachambuzi wa uchumi wa nchi za Magharibi kama Marekani yakidai kuwa bidhaa za viwandani za China ni za bei rahisi kwa sababu wafanyakazi nchini China hawalipwi vizuri.

Na members fulani humu JF wana maoni hayo. Hilo si kweli.

20250216_130125.jpg

Mishahara nchini China ni mikubwa zaidi kuliko katika nchi jirani za SE Asia.


China inazalisha bidhaa kwa bei nafuu kwa sababu:


CHINA IMETENGENEZA COMPLEX SUPPLY CHAIN (MANUFACTURING ECOSYSYEM) ILIYOJITOSHELEZA KUHUDUMIA WAZALISHAJI WA VIWANDANI.

"Complex supply chain" au mnyororo changamano wa ugavi ulioko China ni wa hali ya juu na unajitosheleza kwa kiwango kikubwa sana.
  • Mataifa mengi yenye viwanda yanategemea kuagiza baadhi ya bidhaa, components au critical processed minerals kutoka kwa wazalishaji (suppliers) wa mataifa mengine ili kutengeneza bidhaa zao. Gharama za usafirishaji na ununuzi wa hizo components imefanya mwisho wa siku end products ziwe na bei kubwa.​
  • Lakini upande wa China kumekuwa tofauti, uwepo wa suppliers ndani ya China ambao wanacompete kuzalisha kila aina ya components imefanya China isiwe na uhitaji wa kuagiza sana components kutoka nje ya China katika uzalishaji viwandani. Hii kitaalamu inaitwa "complex supply chain" au "complex manufacturing ecosystem."
  • Mfano jiji la Shenzhen maarufu kama Shenzhen Silicon Valley kuna viwanda ambavyo vinatengeneza kila aina ya vifaa au components za kila aina ya chombo cha umeme (electronic device) unachokijua wewe duniani.​
  • Hii ndio sababu hata makampuni kutoka nchi zingine yanavutiwa kuwekeza China kwa sababu wanajua watapunguza gharama za uzalishaji kwa kutoagiza critical components kutoka nje ya China. Tuzungumzie mfano wa Apple na Tesla:​
"No supply chain in the world is more critical to us than China. We're not in China for low labor costs."
– Tim Cook (Apple C.E.O)

Components za magari yanayotengenezwa na Tesla Shanghai gigfactory zaidi ya 95% zinatengenezwa na Chinese suppliers, Tesla wanafanya kuzinunua kutoka kwa hao Chinese suppliers.


Ndio maana haishangazi kuona magari ya Tesla yanayotengenezwa China yana gharama nafuu kuliko yanayotengenezwa Marekani.

Na hii ni sababu inayofanya Toyota kuamua kujenga kiwanda cha magari ya EV ya Lexus nchini China.


UZALISHAJI KATIKA VIWANDA VINGI CHINA UNAFANYWA KUPITIA ROBOTS (AUTOMATED)
Serikali ya China imeanzisha program ya kuanzisha smart factories yaani kutumia robots na industrial digitalization.
  • Na kufikia sasa China imetengeneza basic level smart factories zaidi ya 30,000.​

  • Matumizi ya robots yamepunguza sana gharama za uzalishaji nchini China na kuongeza ubora wa bidhaa.
20250216_130147.jpg





INAENDELEA....

 
UWEPO WA EXPERTS KAMA SCIENTISTS NA ENGINEERS WA KUTOSHA
China ndio taifa linaloongoza duniani kwa kuzalisha graduates wa STEM (Science, Tech, Enginering, Maths)
  • Uwepo wao (skilled personnel) umefanya kuwe na wataalamu wa kutosha kwenye industrial sector.​
  • Pia kumefanya kuanzishwa kwa centers nyingi za R&D ambazo nazo zimesaidia wazalishaji wa viwandani kufanya innovations katika uzalishaji na kupunguza cost of production.​
Tim Cook C.E.O wa Apple alitaja kuwa uwepo wa skilled personnel ni sababu nyingine iliyowavutia Apple kuwekeza nchini China iko hivyo pia upande wa Tesla.

"In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
– Tim Cook (Apple CEO)


Tesla Shanghai gigafactory wafanyakazi wote waliopo kutia ndani skilled, 99.9% ni Wachina hakuna uhitaji wa experts kutoka nje ya China. Hii ni sababu nyingine imepunguza gharama za uzalishaji kiwandani hapo.
BENKI ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA CHINA ZINATOA MIKOPO NAFUU KWA RIBA NDOGO KWA WAZALISHAJI WA VIWANDANI
  • Sera nzuri katika taasisi za kifedha iliyowekwa na serikali ya China katika kuwakopesha wamiliki na wewekezaji wa viwanda kwa kuwapa riba ndogo imechangia bei za bidhaa za viwandani nchini China ziwe ndogo kwa sababu wawekezaji hawahitaji kurudisha riba kubwa kwa benki walizokopa.​



VIWANDA NA KAMPUNI ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA CHINA, CHINA'S STATE OWNED ENTERPRISES (SOEs)

Kama tujuavyo China ni nchi ya socialism with Chinese characteristics, hivyo 40% ya makampuni yaliyoko China yanamilikiwa na serikali

  • Makampuni haya yanapata ruzuku lakini pia yanasaidiwa na serikali kwenye huduma muhimu kama energy, mining, transportation, telecommunications etc. Matokeo imepunguza cost of production na bei za bidhaa kwa ujumla.​

  • Serikali ya China pia hutoa ruzuku kwa makampuni binafsi kama vile Tesla n.k​


SERIKALI YA CHINA IMEWEKEZA SANA KWENYE MIUNDOMBINU BORA SANA NA YA KISASA
  • Kadiri miundombinu inavyokuwa bora na ya kisasa ndivyo inapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza kasi ya uzalishaji.
  • Kwa mfano kati ya bandari 10 kubwa duniani na za kisasa na the most busiest ports in the world 7 ziko China.

  • High Speed Railway iliyosambaa kwa zaidi ya km 45,000 chini China imesaidia kuharakisha mwingiliano kati ya miji yenye viwanda na kuchochea uzalishaji.

Hii ndio tofauti kati ya socialism with Chinese chatacteristics na capitalism. Wabepari wao wanaangalia tu maximizing profit, socialism with Chinese characteristics inaangalia kwanza ku-serve the economy and society kwa ujumla.
 
Kama maroboti ndio wanaofanya kazi nyingi za viwandani huko China raia wa China wanafanya kazi zipi?? Ni wakulima mashambani, wavuvi au wachimba madini?
China kuna zaidi ya 6 million mfg industries na sio viwanda vyote vinatumia robots full

Na hata kiwanda kikiwa ni automated bado wafanyakazi watahitajika pia japo si wengi kama kusingekuwa na robots kabisa

Halafu program ya China ya smart industries ililenga for the future pia. Idadi ya watu inakadiriwa kuwa itapungua na hii ni tatizo linalozikumba nchi za the Far East Asia kama Japan na S.K

Kwa hiyo ni kama wanaongeza nguvu kazi kwa baadaye
 
Unahitaji Complex supply chain gani kwa ajili ya kutengeneza nguo, viatu, furniture, mabati na urembo wa simu?
Huko kwenye kutengeneza bidhaa za aina hiyo China ilishapita.

Kwa sasa China iko kwenye kutengeneza high tech goods ambazo zinahitaji uwe na complex supply chain ili kuminimize cost
 
China kuna zaidi ya 6 million mfg industries na sio viwanda vyote vinatumia robots full

Na hata kiwanda kikiwa ni automated bado wafanyakazi watahitajika pia japo si wengi kama kusingekuwa na robots kabisa

Halafu program ya China ya smart industries ililenga for the future pia. Idadi ya watu inakadiriwa kuwa itapungua na hii ni tatizo linalozikumba nchi za the Far East Asia kama Japan na S.K

Kwa hiyo ni kama wanaongeza nguvu kazi kwa baadaye
Bidhaa za China zipo rahisi kwa sababu ya cheap labour na inferior material zisizozingatia usalama na na quality kwa mlaji. Kwa mfano kuna hizi zinazoitwa ''fast fashion'' kuna maduka mengi Europe wamezipiga marufuku kwa sababu hazidumu na zina toxic materials. Na hapa unatakiwa ujue kuwa bidhaa zinazokwenda Europe ni nzuri kuliko zinazokwenda Afrika.
 
Bidhaa za China zipo rahisi kwa sababu ya cheap labour na inferior material zisizozingatia usalama na na quality kwa mlaji. Kwa mfano kuna hizi zinazoitwa ''fast fashion'' kuna maduka mengi Europe wamezipiga marufuku kwa sababu hazidumu na zina toxic materials. Na hapa unatakiwa ujue kuwa bidhaa zinazokwenda Europe ni nzuri kuliko zinazokwenda Afrika.
Mazingira ya uzalishaji ni ya hovyo sana pia China na yanayowaweka raia katika hali mbaya za afya. Kwa mwaka moshi wa viwandani/air pollution unaua raia million 2 na visa mamilioni vya magonjwa ya mfumo wa upumuaji China.
Kuna miji moshi huwa unatoka viwandani mpaka watu wanashindwa kuonana wanapoteana mitaani.
 
Unafikiri ni kwa nini Afrika inashindwa kutengeneza hizo bidhaa na ina cheap labour?
Kutengeza bidhaa rahisi siyo cheap labour tu. Cheap labour ni factor ndogo sana. Unahitaji ujuzi, unahitaji jamii yenye culture ya uchapakazi, unahitaji mazingira mazuri ya uzalisha, unahitaji supply chain nzuri, unahitaji infrastructure za ubora, unahitaji nchi stable. Hizi nchi za kina Samia wanazoshindwa hata kujenga vyoo na kununua madawati sembuse kuendesha bandari wataweza?
 
Back
Top Bottom