UWEPO WA EXPERTS KAMA SCIENTISTS NA ENGINEERS WA KUTOSHA
China ndio taifa linaloongoza duniani kwa kuzalisha graduates wa STEM (Science, Tech, Enginering, Maths)
Uwepo wao (skilled personnel) umefanya kuwe na wataalamu wa kutosha kwenye industrial sector.
Pia kumefanya kuanzishwa kwa centers nyingi za R&D ambazo nazo zimesaidia wazalishaji wa viwandani kufanya innovations katika uzalishaji na kupunguza cost of production.
Tim Cook C.E.O wa Apple alitaja kuwa uwepo wa skilled personnel ni sababu nyingine iliyowavutia Apple kuwekeza nchini China iko hivyo pia upande wa Tesla.
"In the United States if we have a meeting of tooling engineers and we might not fill a room. In China, we would fill multiple football fields."
– Tim Cook (Apple CEO)
Tesla Shanghai gigafactory wafanyakazi wote waliopo kutia ndani skilled, 99.9% ni Wachina hakuna uhitaji wa experts kutoka nje ya China. Hii ni sababu nyingine imepunguza gharama za uzalishaji kiwandani hapo.
BENKI ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA CHINA ZINATOA MIKOPO NAFUU KWA RIBA NDOGO KWA WAZALISHAJI WA VIWANDANI
Sera nzuri katika taasisi za kifedha iliyowekwa na serikali ya China katika kuwakopesha wamiliki na wewekezaji wa viwanda kwa kuwapa riba ndogo imechangia bei za bidhaa za viwandani nchini China ziwe ndogo kwa sababu wawekezaji hawahitaji kurudisha riba kubwa kwa benki walizokopa.
VIWANDA NA KAMPUNI ZINAZOMILIKIWA NA SERIKALI YA CHINA, CHINA'S STATE OWNED ENTERPRISES (SOEs)
Kama tujuavyo China ni nchi ya socialism with Chinese characteristics, hivyo 40% ya makampuni yaliyoko China yanamilikiwa na serikali
Makampuni haya yanapata ruzuku lakini pia yanasaidiwa na serikali kwenye huduma muhimu kama energy, mining, transportation, telecommunications etc. Matokeo imepunguza cost of production na bei za bidhaa kwa ujumla.
Serikali ya China pia hutoa ruzuku kwa makampuni binafsi kama vile Tesla n.k
SERIKALI YA CHINA IMEWEKEZA SANA KWENYE MIUNDOMBINU BORA SANA NA YA KISASA
Hii ndio tofauti kati ya socialism with Chinese chatacteristics na capitalism. Wabepari wao wanaangalia tu maximizing profit, socialism with Chinese characteristics inaangalia kwanza ku-serve the economy and society kwa ujumla.