Kwanini Bikra Maria anatumika kuwaombea wakatoliki wakati alishakufa?

Kwanini Bikra Maria anatumika kuwaombea wakatoliki wakati alishakufa?

Jitu la kienyeji

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,445
Reaction score
7,987
Kwanini Wakatoliki wanamtumia Bikira Maria awaombee wakati Bikira Maria ni binadamu tu wa kawaida kama sisi? Na kwanini kwenye Biblia maisha yake hayajaandikwa sana? .

Mimi hapa najiuliza na nitaendelea kushangaa sana, inawezekaje kumtumia Bikira Maria akuombee kwa Mungu wakati ameshakufa na yuko ardhini?.

Kwenye Biblia hakuna sehemu hata moja aliyotajwa Bikira Maria akiombwa, akitambuliwa kama mpatanishi, au kuambiwa atuombee!.

Maria alikuwa binadamu tu wa kawaida kabisa kama sisi tulivyo, na hata Biblia yenyewe haijamzungumzia sana.
Wala hata Yesu mwenyewe hajawahi kusema au kuagiza mahali popote kwamba tumtumie Bikira Maria kama daraja la kufikia maombi yetu..

ASA KWANINI?
Au ndo kujiamulia Mambo stori za wazungu.
 
Attachments

  • FB_IMG_1792436456492.jpg
    FB_IMG_1792436456492.jpg
    456.9 KB · Views: 9
  • FB_IMG_1792436435630.jpg
    FB_IMG_1792436435630.jpg
    88.8 KB · Views: 8
Kama kuna eneo ambalo wakatoliki wamebuma ni suala Bikira Maria.

Tafuta vitabu vyote katika Biblia Takatifu hakuna sehemu tumeambia Maria ana uwezo wa kutuombea.
Tafuta mistari yote ya Biblia hakuna mstari ambao unatutaka au kutuambia Maria ni mponyaji ?.
 
Sio Bikira Maria tu, Hata Yohane Mtume, Paulo, Mtakatifu Petro, Mtakatifu Luka na wengineo tunawaheshimu na tunaamini wako mbinguni. Halafu kasome Biblia yako vizuri, Si kweli kwamba hakuna sehemu kwenye Biblia Bikira Maria hakuombwa, Walipokuwa kwenye harusi ya kana, Divai ilipoisha, unajua walimfuata nani? Elimu yako ndogo sana kuweza kuelewa mambo hayo.
 
Weka aya tuthibitishee
 
Mimi kama Mkristo ninaposema "Bikira Maria utuombee," simchukulii Maria kama Mungu na wala simwabudu hata kidogo.

Namwabudu Mungu pekee, lakini namwomba Maria aniombee kwa Mungu (uombezi) kwa sababu naamini yuko hai mbinguni karibu na Mwanae Yesu Kristo, na maombi yake yana nguvu kubwa kutokana na utakatifu na nafasi yake ya kipekee kama Mama wa Mwokozi. Huu ni uombezi wa kawaida kama ule ninaomwomba rafiki au mchungaji wangu aniombee ninapokuwa na shida, isipokuwa tu Maria yuko mbinguni na ana ushawishi mkubwa zaidi mbele za Mungu.

Imani yangu hii inasimama imara juu ya mistari ya Biblia. Katika Yakobo 5:16, neno la Mungu linaniambia kuwa “kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.” Kwa kuwa Malaika Gabrieli katika Luka 1:28 alimwambia Maria “Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe,” najua kabisa kuwa Maria ni mwenye haki mkuu aliyekamilika, na maombi yake kwenda kwa Mungu kwa ajili yangu yana nguvu sana. Zaidi ya hayo, kitabu cha Ufunuo 5:8 kinanionyesha wazi kuwa watakatifu mbinguni wanashikilia “vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu” (yaani maombi yetu sisi tulio duniani), jambo linalonithibitishia kuwa Maria ana uwezo wa kupokea maombi yangu na kuyawasilisha mbele za Mungu.

Mimi pia najifunza kutoka kwenye Injili ya Yohane 2:1-11 katika Harusi ya Kana, ambapo naona nguvu ya uombezi wa Maria waziwazi. Maria alipoona wenye harusi wameishiwa divai, aliingilia kati na kumwambia Yesu, “Hawana divai.” Licha ya kwamba wakati wa Yesu ulikuwa bado, alisisitiza na kuwaambia watumishi, “Lo lote atakalowaambia, fanyeni,” na Yesu akasikiliza ombi la Mama yake na kufanya muujiza wake wa kwanza. Hii inanipa ujasiri wa kumwambia Maria aniombee leo, nikijua kuwa kama vile Yesu alivyomsikiliza duniani, ndivyo anavyomsikiliza na mbinguni.
Ninapomwomba Maria aniombee, ninatenda sawasawa na unabii uliopo kwenye Luka 1:48 ambapo yeye mwenyewe alisema, “Kwa maana tangu sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa.” Mimi nikiwa miongoni mwa vizazi hivyo, namtaja kama mbarikiwa na kumkimbilia kama Mama yangu wa kiroho aliyekabidhiwa kwetu na Yesu pale msalabani (Yohane 19:27), nikiwa na amani moyoni kuwa ananiombea baraka na neema kwa Mungu Baba.
 
Kama kuna eneo ambalo wakatoliki wamebuma ni suala Bikira Maria.

Tafuta vitabu vyote katika Biblia Takatifu hakuna sehemu tumeambia Maria ana uwezo wa kutuombea.
Tafuta mistari yote ya Biblia hakuna mstari ambao unatutaka au kutuambia Maria ni mponyaji ?.
Bikira maria alipata mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Huyo roho mtakatifu kwanini hawapi mimba Wanawake wagumba?
 
Kuna wana ambao hawakufa walipalizwa mbinguni

Ikiwemo, Eliya na Mussa, hawa hawakufa walipaa mbinguni

Wakatoliki wakajongela kuw Bikira Maria Mpalizwa mbinguni
 
Kwanini Wakatoliki wanamtumia Bikira Maria awaombee wakati Bikira Maria ni binadamu tu wa kawaida kama sisi? Na kwanini kwenye Biblia maisha yake hayajaandikwa sana? .

Mimi hapa najiuliza na nitaendelea kushangaa sana, inawezekaje kumtumia Bikira Maria akuombee kwa Mungu wakati ameshakufa na yuko ardhini?.

Kwenye Biblia hakuna sehemu hata moja aliyotajwa Bikira Maria akiombwa, akitambuliwa kama mpatanishi, au kuambiwa atuombee!.

Maria alikuwa binadamu tu wa kawaida kabisa kama sisi tulivyo, na hata Biblia yenyewe haijamzungumzia sana.
Wala hata Yesu mwenyewe hajawahi kusema au kuagiza mahali popote kwamba tumtumie Bikira Maria kama daraja la kufikia maombi yetu..

ASA KWANINI?
Au ndo kujiamulia Mambo stori za wazungu.
Kuna watu wanaomba mizimu, wanatambika na kutoa kafara mbalimbali ili wasaidiwe, na wanafanya hivyo...je ni wapi imeandikwa? Na majina ya hiyo mizimu imetajwa wapi?
Hili jambo la wakatoliki limekaa kiimani kweli kweli, na wanaofanya hivyo wanajua na kuna matokeo wameyapata. And btw wakiomba hata kupitia Bibi wa Bibi zao, wewe kinachokuuma ni nini? Mtu akiwa na imani na kitu flani wewe unawashwa kwa sababu gani? Hata wewe una imani yako, amini kuomba hata kupitia mgomba.
 
Back
Top Bottom