Kwanini Bikra Maria anatumika kuwaombea wakatoliki wakati alishakufa?

Kwanini Bikra Maria anatumika kuwaombea wakatoliki wakati alishakufa?

Sio Bikira Maria tu, Hata Yohane Mtume, Paulo, Mtakatifu Petro, Mtakatifu Luka na wengineo tunawaheshimu na tunaamini wako mbinguni. Halafu kasome Biblia yako vizuri, Si kweli kwamba hakuna sehemu kwenye Biblia Bikira Maria hakuombwa, Walipokuwa kwenye harusi ya kana, Divai ilipoisha, unajua walimfuata nani? Elimu yako ndogo sana kuweza kuelewa mambo hayo.
Tunawaheshimu Yohane wapi? Paulo wapi? Petro wapi? Luka wapi tunawaheshimu.
 
Kwanini Wakatoliki wanamtumia Bikira Maria awaombee wakati Bikira Maria ni binadamu tu wa kawaida kama sisi? Na kwanini kwenye Biblia maisha yake hayajaandikwa sana? .

Mimi hapa najiuliza na nitaendelea kushangaa sana, inawezekaje kumtumia Bikira Maria akuombee kwa Mungu wakati ameshakufa na yuko ardhini?.

Kwenye Biblia hakuna sehemu hata moja aliyotajwa Bikira Maria akiombwa, akitambuliwa kama mpatanishi, au kuambiwa atuombee!.

Maria alikuwa binadamu tu wa kawaida kabisa kama sisi tulivyo, na hata Biblia yenyewe haijamzungumzia sana.
Wala hata Yesu mwenyewe hajawahi kusema au kuagiza mahali popote kwamba tumtumie Bikira Maria kama daraja la kufikia maombi yetu..

ASA KWANINI?
Au ndo kujiamulia Mambo stori za wazungu.
Kama sio Mkatoliki hata kama ukieleweshwa huwezi kuelewa. Ni kama mimi Mkatoliki eti unieleweshe kuwa Kitimoto ni haramu; nakuelewaje? Ahahahahaha!!
 
MOJA WAPO YA KAZI ZA WATAKATIFU NI KUPOKEA MAOMBI NA KUPELEKA KATIKA KITI CHA ENZI KUPITIA MALAIKA. SOMA.
UFUNUO WA YOHANA SURA YA 8.
3.Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.
Bikira maria ni mtakatifu ukisoma utajua hayo Maono ya Yohana alipomwoma Bikira Maria katika Ufalme wa Mbingu akipewa jukumu la Duniani namna atakavyomleta Yesu na Changamoto atakazo pambana nazo duniani lakini mkono wa Mungu utamlinda.
UFUNUO WA YOHANA 12. MAONO YA KUZALIWA YESU-MARIAM

1.Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
 
Back
Top Bottom