Kwanini Bikra Maria anatumika kuwaombea wakatoliki wakati alishakufa?

Tunawaheshimu Yohane wapi? Paulo wapi? Petro wapi? Luka wapi tunawaheshimu.
 
Kama sio Mkatoliki hata kama ukieleweshwa huwezi kuelewa. Ni kama mimi Mkatoliki eti unieleweshe kuwa Kitimoto ni haramu; nakuelewaje? Ahahahahaha!!
 
MOJA WAPO YA KAZI ZA WATAKATIFU NI KUPOKEA MAOMBI NA KUPELEKA KATIKA KITI CHA ENZI KUPITIA MALAIKA. SOMA.
UFUNUO WA YOHANA SURA YA 8.
3.Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
4 Na moshi wa ule uvumba ukapanda mbele za Mungu pamoja na maombi ya watakatifu, kutoka mkononi mwa malaika.
Bikira maria ni mtakatifu ukisoma utajua hayo Maono ya Yohana alipomwoma Bikira Maria katika Ufalme wa Mbingu akipewa jukumu la Duniani namna atakavyomleta Yesu na Changamoto atakazo pambana nazo duniani lakini mkono wa Mungu utamlinda.
UFUNUO WA YOHANA 12. MAONO YA KUZALIWA YESU-MARIAM

1.Na ishara kuu ilionekana mbinguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota kumi na mbili.
2 Naye alikuwa ana mimba, akilia, hali ana utungu na kuumwa katika kuzaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…