Miss Madeko
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 4,364
- 5,609
Unadhani huyo anayeng'ang'ana na kuprint hela ataelewa unachomwelezea? Yeye anataka hela iprintiwe kama mitihani.Labda nikupe mfano... mfano mimi kazi ninazozifanya nalipwa kwa dollar. Ina mana nimefanya kazi, mzungu ananilipa assume dollar 500 ambayo kwa tshs ni kama 1.2 mils, anafanya wire transfer inafika bank local bank wanapokea dollar ila mimi kwenye my account wanaweka tshs: ambayo 1.2 mls. wao dollar wanabaki nazo na mwisho zitaenda BOT maana wana kiasi cha pesa ya kigeni wanachoruhusiwa kuwa nacho kikizidi wanapeleka BOT.
Hay assume umeuza kitu nje viatu vya kimasai, umeuza mzigo wa dollar 1000, mnunuzi kalipa, lakini wewe kwenye account utawekewa Tshs. Hapo unaona kupitia shughuli zetu za kiuchumi serikali inapata pesa pia. Kuna kuuza madini pia yanauzwa kwa foeign currency. Hata Kahawa na kadhalika.
Siyo kila anayeuza bidhaa nje akilipwa ananunua kitu analeta huku. Na ndiyo maana uchumi illi ufanye vizuri export inabidi iwe kubwa kuliko import, ikiwa na maana tunaingiza pesa ya kigeni nyingi kuliko tunayotoa.
Watanzania bwana haya ngoja Jamal printers waje wakuelekeze