Ili kukuza uchumi, unatakiwa kuzidisha uzalishaji.
Ukizidisha kuchapisha pesa tu, kitakachotokea ni kwamba ,hela zitakuwa nyingi, lakini vitu vitapanda bei sana (inflation).
Boss nimepitia replies kibao, ila jibu liko hapa, ingawa Kiranga kakujibu kwa kifupi.
Nitajaribu kujazia kwa kifupi na kwa mifano ya "kibishi". Kiranga kakutajia aspects mbili za haraka ambazo ni PRODUCTION na INFLATION, hapa katika inflation weka kichwani aspect ya bei(PRICE).
Huu imagine ni kama mzani PRODUCTION(uzalishaji) ya nchi na PRICE huwa vinatakiwa kuwa katika uwiano fulani, kumbuka ukizalisha kidogo na pesa zikiwa nyingi baada ya kuziprint unapata mfumuko wa bei(INFLATION) na ukizalisha sana na ukawa na pesa kidogo, unakuwa na bidhaa nyingi zinakimbizwa na pesa kidogo hapo unapata anguko la bei(deflation).
***Turudi katika issue yako,kwanza utakapo print pesa na kuwalipa wadau kudai na kufanyia miradi,pesa hiyo tayari imeshaingia katika mzunguko wako hata kama umewalipa wajerumani baada ya ku convert kuwa dollar,kwa sababu iwe umewapa pesa ya kigeni au ya kwako wakaikubali basi hawaendi kuikalia kama friji ndani,itatumika tu katika mzunguko duniani.
****Sasa baada ya ku print na kuwalipa na wenyewe kuingiza pesa hiyo katika mzunguko, kumbuka kule juu katika mfano wa mahusiano ya uzalishaji na bei,yani unatakiwa uwe katika uwiano fulani, kwa kesi hii hali itakuwa hivi umezalisha pesa nyingi(print) ili ukanunue dollar(bidhaa) ili ukawalipe wanaokudai bidhaa yao na bidhaa nyingine utumie kwa miradi yako,matokeo yake yatakuwa pesa nyingi inakimbiza bidhaa kidogo(dollar), matokeo yake utatoa pesa nyingi-shilingi kupata dollar moja,na hapo utakuwa umepata anguko la thamani ya pesa yako.
***Matokeo yake kwa kuwa hauna uzalishaji wa kutosha utakosa uwiano mzuri wa malipo(Balance Of Payment) na biashara (Balance Of Trade). Na hii ni kitu inatesa nchi nyingi za kiafrica unauza malighafi mfano pamba halafu unanunua nguo hapa lazima wafaidike wale wa kule wanaotengeneza nguo(finished goods).
***Mkuu nimejaribu kugusia fasta hii ni topic nzito,kuna mambo kama High Power Money Supply n.k ambazo decision zake hufanywa na benki kuu.
Mwisho,pole yetu kwa sera mbovu za kijani zinazofanya mpaka sasa tuulizane maswali yanayoonyesha tumechoshwa na "umasikini wa makusudi" unaotokana na ukosefu wa ubunifu wa viongozi wetu.