Mkuu vitu vikipanda bei si bado hela nayo itakuwa nyingi mtaani kwahiyo suala la mfumuko linakuwa halina mashiko tena.
Mfumuko wa bei nijuavyo ni pale bidhaa zinakuwa bei juu halafu mzunguko wa hela mdogo.
Mfano mfuko wa cement 35,000 lakini mzunguko wa hela mdogo.
Sasa hela ikiwa nyingi mtaani hata huo mfuko wa cement ukiuzwa 50,000 si bado watu watakuwa na uwezo wakununua!!!
Jinsi hela inavyozidi kuongezeka bila uzalishaji kuongezeka, ndivyo mfumuko wa bei nao unavyozidi.
Kwa mfano, ukisema uongeze hela katika uchumi ili watu waweze kununua simenti ya sh 35,000/=kwa mfuko, bila kuongeza uzalishaji wa simenti, kitakachotokeq ni kwamba kila mtu qtamudu kununua simenti kwa sh 35,000/=.
Simenti haitaongezeka, lakini hela zitaongezeka.
Matokeo yake kuna watu watamudu kununua simenti kwa 70,000/=, bei ya simenti itapanda nankuwa 70,000/=.
Wauzaji wakinua watu wananunua simwnti kwa 70,000/=, wanaweza kupandisha zaidi simenti ifike 100,000/= kwa mfuko.
Na hapo hapo watu wengine watamudu kununua simenti kwa 100,000/= kwa mfuko.
Bei itaendelea kupanda na kupanda mpaka simwnti ifike sh milioni moja kwa mfuko.
Halafu, ukijaza pesa kila mtu, hakuna atakayetaka kwenda kuhangaika kwenye mavumbi kiwanda cha simenti.
Matokeo yake uzalishaji utasimama.
Na hata ukiwa na sh milioni kumi hutapata mfuko wa simenti.
Hapo utaona kwamba, bila kuongeza uzalishaji, kuongeza hela tu katika mfumo hakusaidii kitu, kutashusha thamani ya fedha bila kuongeza tija yoyote katika uchumi.
Idi Amin alijaribu kutatua matatizo ya uchumi ya Uganda kwa kumuamrisha Waziri wa Fedha wa Uganda kuchapisha fedha zaidi.
Kilichotokea ni kwamba shilingi ya Uganda ilianguka thamani vibaya sana, mpaka leo haijarudi ilipokuwa kabla ya Idi Amin.