Pre GE2025 Kwanini CCM inalazimisha kuingiza Jeshi la Tanzania (JWTZ) kwenye Siasa? Je, inalipa? Chonde Chonde Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Yaani JWTZ limegeuka kuwa jeshi la kwanza Afrika kugeuzwa kampuni ya kusafisha uchafu jijini ikiwamo vinyesi, kuzoa taka, kuzibua vyoo na maji taka. Nadhani ili kuongeza mapato wapewe na kandarasi kutuhudumia kwa pesa vyoo vyetu vikiziba maana CCM inataka kuwapa uzoefu.
Ukiona mtu anajisaidia mtaroni muache tuu usafi utafanyika kwa AMRI YA RC DAR

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
 
Duh wakiona una misimamo wanakupa ubalozi 😀😀😀
 
Heshima ya JWTZ tunayoijua halafu inaagizwa na mwanasiasa kusafisha uchafu! Kwani kampuni binafsi zinazolipwa na serikali mfano Kajenjere nk haziwezi kusafisha?
 
Why now?...

Jeshi kutumika kisiasa ndio kupoje ?....je ikitokea mwanajeshi akapewa Ukuu wa mkoa au eneo fulani la kiraia akiwa bado hajastaafu ndio kutumika kisiasa huko ?

JokaKuu zitto junior
 
Utatu mtakatifu wa CCM,NEC na vyombo vya usalama!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Why now?...

Jeshi kutumika kisiasa ndio kupoje ?....je ikitokea mwanajeshi akapewa Ukuu wa mkoa au eneo fulani la kiraia akiwa bado hajastaafu ndio kutumika kisiasa huko ?

JokaKuu zitto junior
Kutumika kisiasa ni kama huku kusema wanafanya usafi muda mfupi baada ya CHADEMA kutangaza maandamano, kwani wanaogopa nini?
 
Hivi kati ya wote mliyochangia humu kuna ambaye amekusudia kweli kwenda kuandamana au wote tutafuatilia maandamano tukiwa JF?
 
Tatizo la bakabaka wetu nao hawana akili wataingia mtego kwakua hawajielewi sifa zimewajaa ila mwisho unakaribia kwenye picha walivyo serious utadhani kweli kumbe mandezi tu
 
Aisee ccm imeonesha udhaifu wa wazi wazi.

Hata aibu sasa hawana tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…