Pre GE2025 Kwanini CCM inalazimisha kuingiza Jeshi la Tanzania (JWTZ) kwenye Siasa? Je, inalipa? Chonde Chonde Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Nadhani bado kuna watu wenye hekima wamebaki watamsaidia Rais kumwambia kuwa huko nchi inakoelekezwa Jeshi kuingilia michakato ya amani ya kisiasa siyo sehemu ya utawala bora. Orodha ya madudu ya kiutawala inazidi kuongezeka. Historia itawahukumu mkiwa bado hai!
 
Ni jambo jema wakafanye usafi
Wanakaa tu makambini na kulishwa na kuvishwa kwa kodi zet huku wakitutisha kuwa wanatulinda na uvamizi wakati walituabisha huko Mozambique
 
Ni dharau tu za watawala kwa Jeshi letu.
Baada ya kuona wameshawashika masikio sasa wamewatoa kwenye majukumu yao ya Ulinzi wa nchi na kuona wanafaa kutumika kwenda kufagia barabara kama Budege ili kupamnana na Mbowe.
Yaani yale maonyesho yote ya kuvunja matofali kwa vichwa, kuruka na kutua kwa helcopter wanaishia kubebeshwa mafagio wakapambane na Mbowe na CHADEMA?
 
Inasikitisha sana kwa hii Misuse of power inayofanywa na CCM.

Kiukweli leo Ccm wameniudhi sana.
 
Nadhani ni baada ya swaiba wao Polisi kushindwa

 
Huyo aliyeleta hilo wazo hana akili hata kidogo akapimwe kinyesi na ubongo wake, what if kila chama kitaanzisha jeshi lake?
 
Wakunya wakanye barabarani hata usiku, wakufungulia vyoobfungulieni mana tuna jeshi la usafi.
 
Kumbe mazoezi yote Yale ni kwaajili ya CHADEMA.
 
Wataandamana waliotumwa na RC.

Yaani ccm umekuwa na woga kiasi hiki?
Tunajuana humu huwa tunaadamania JF ndio maana nashangaa hii hofu ya jeshi tunaitoa wapi wakati sie kazi yetu ni kufuatilia maandamano tukiwa JF?
 
JWTZ is a neutral organ,credible and reputable to protect our sovereignty against any foreign intrusion. lisichezewe.
 
Hilo jeshi na hao wwnajeshi ndio wapumbavu.... Hawajui majukum yao mama?, Kwamba wao wanafurahia ndugu zao na familia zao kuongozwa kipuuzi?.... Hakuna jeshi la hovyoo Dunia hii Kama la Tz, wao wenyewe ni waonevu wakubwa.
 
Hilo jeshi na hao wwnajeshi ndio wapumbavu.... Hawajui majukum yao mama?, Kwamba wao wanafurahia ndugu zao na familia zao kuongozwa kipuuzi?.... Hakuna jeshi la hovyoo Dunia hii Kama la Tz, wao wenyewe ni waonevu wakubwa.
Tatizo kubwa liko kwenye Serikali yenyewe. Miswada ambayo ndiyo kisa cha maandamano ya Chadema inahusu mjadala wa uchaguzi kuwa huru au kutokuwa huru kwa maana kama Serikali ina sifa au haina sifa ya kusimamia uchaguzi kwa sababu kwa mujibu wa wasilisho la TEC kwenye Kamati ya Bunge kuna mifano ambayo Serikali inaonesha siyo refa. Cha kushangaza, ndugu yangu Mwalimu ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa anatoa amri ambayo ikitelezwa itakuwa ni ushahidi mwingine ya hoja ya TEC na wadau wengine kuwa Serikali imeegemea upande mmoja hata kabla Bunge lenyewe halijakaa kupitia mapendekezo. Yaani wakati kesi inaendelea mwenzetu RC anatoa ushuhuda unaomfunga! Sijawahi kufikiri jambo linaweza kutokea kwenye ngazi ya Serikali yenye wanasheria wengi tu! Ndiyo maana nasema Rais wetu asaidiwe aendeshe Serikali yetu isiabike!
 
Haijakaa vema Jeshi kutumika kisiasa.

CDF alitazame hili, heshima ya Jeshi itashuka sana. Hatujazoea mambo kama haya.

CDF huko uliko kaa na Rais mkumbushe Jeshi halipo kwa ajili ya agenda za kisiasa lipo kwa ajili ya Ulinzi wa Nchi, najua ni ngumu kwa sababu aliyekuteua ni Rais lakini nakukumbusha Tanzania ni muhimu kuliko Rais, kuliko CDF, kuliko mimi na mtu mwingine awe ni Chadema au CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…