Kwa yeyote yule ambae amekasirika na kitendo cha Samia ni bora kwanza angelijiuliza ni kwa sababu gani Rais amekwenda huko ubelgiji? Kwani rais alfika ubelgiji kufanya shoping, matibabu au mapumziko? Jawabu ni rahisi sana, amekwenda kikazi na kila mmoja anajua lengo kuu ni kutafuta/kuomba mikopo ya miradi mbali mbali ambayo daima huwa chini ya mwamvuli wa "kudumisha mahusiano ya nchi mbili hizi". Sasa kwenda kuomba misaada katika nchi ambayo inaamini kabisa kuwa Tanzania haihishimu uhuru wa vyama vingi, nchi ambayo imefanya kila hali kuhakikisha wanamtoa nchini kiongozi wa upinzani kwa sababu wanaamini kuwa serikali haitamtendea haki, unadhani jambo la kwanza watakalo lijadili kabla ya kukubali kutoa aina yeyote ile ya misaada na mikopo? Jawabu ni kuwa "uhuru wa vyama vya upinzani", bila ya shaka serikali ilisisitiza kuwa inaheshimu hilo, na wakaambiwa "prove it" kwa kukutana na kiongozi wa upinzani. Na kama wanavyosema watu "almuhitaji khanith" Samia mkono wake ulipindwa aidha alikuwa arudi patupu au aonane na Lisu na apewe misaada.
Serikali ya Tanzania itajaribu kuipaka hii issue rangi watakazo, waseme lissu ndie aliomba kukutana na Samia na mengineyo, lakini la ukweli ni kuwa Samia kukutana na Lissu ni masharti alopewa na serikali ya ubelgiji kabla ya kukubaliana kurudisha uhusiano mzuri baina ya nchi mbili hizi.