Kwanini CDF aitwe Mkuu wa Majeshi wakati Polisi, Magereza na Uhamiaji wana wakuu wao?

Kwanini CDF aitwe Mkuu wa Majeshi wakati Polisi, Magereza na Uhamiaji wana wakuu wao?

Nimekuwa nikishuhudia CDF akiitwa mkuu wa majeshi ilihali jeshi la Magereza,Polisi na Uhamiaji yanao wakuu wao.

Sasa ni ipi sababu hasa ya CDF kuitwa mkuu wa majeshi?
mada za genta aka popoma.
 
Mada hii tamu sana na imekuwa ni kawaida sasa kukija mada ya ulinzi na usalama basi lazima kuingie malumbano ya hoja...

Hata mleta mada nadhani amebaki kaduwaa tu sasahivi akicheki majibu ya uzi wake
 
Ni mazoea tu ila polisi hawakutakiwa waitwe"jeshi la polisi".uhamiaji,askari wa wanyama pori,,zimamoto hizo ni taasisi za kutoa huduma,na polisi pia wapewe jina litakalo endana na kutoa huduma wasiwe jeshi,hadhi ya jeshi ni kubwa wabakie hao hao mboga mboga JW.
 
Nimekuwa nikishuhudia CDF akiitwa mkuu wa majeshi ilihali jeshi la Magereza,Polisi na Uhamiaji yanao wakuu wao.

Sasa ni ipi sababu hasa ya CDF kuitwa mkuu wa majeshi?
Majeshi yanayoongelewa kwenye cheo cha CDF ni Navy (La Maji), Air force (La Anga) na Infantry (La ardhi).

Polisi, Uhamiaji na Magereza siyo majeshi. Zile ni idara chini ya Wizara ya mambo ya ndani zinazovaa uniform na buti na zinazotumia silaha kwa ulinzi.

Hata Hospitali siyo kila anayevaa koti jeupe ni Doctor, wengine ni manesi tu
 
Nimekuwa nikishuhudia CDF akiitwa mkuu wa majeshi ilihali jeshi la Magereza,Polisi na Uhamiaji yanao wakuu wao.

Sasa ni ipi sababu hasa ya CDF kuitwa mkuu wa majeshi?
Ikitokea vita kati ya nchi yetu na nyingine (mwenyezi Mungu atuepushe) ndio utarkewa maana ya mkuu wa Majeshi.
 
As long as wanaitwa force basi hawana tofauti na fire and rescue[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]

Tofauti Yao ni majukumu tu
Wewe utakua polisi!

Military ni jeshi na Force ni kikosi tu!

TISS,PCCB,Uhamiaji na hao Polisi hawafundishwi matumizi ya siraha nzito! Mfano huwezi kuta kifaru kipo kwenye kikosi cha Polisi,PCCB au Uhamiaji!

Rais anapokua anakabidhi madaraka kwa mwingine kwa nini CDF ndiyo hua anasimama na Rais na sio IGP,DG-TISS DG-PCCB,CGI,CGF au CGP??
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] umetoa tafsiri toka dictionary gani?
Hiyo ndio maana yake,kama unatafsiri neno la kingereza kwa neno la kiswahili kama lilivyo,yaani force=nguvu,,ndio maana nikakuomba rudi shule

Military=Jeshi lizaa force=vikosi na ndio maana unapata mtoto kama Air force =Jeshi la anga,unapata mtoto Army force =Jeshi la Ardhi,unapata Navy=jeshi la baharini nk
 
Hao akina wambura na mzee ni wanamgambo kama wale wa taliban.
Hao taliban waliwafurumusha USSR na NATO huko Afghanistan sasa hilo jeshi lako ndo ulifananishe na taliban!!!acha ujinga huo
 
Siki moja alipita Jwtz ni private wa kawaida hana cheo kabisa akapishana na Maofisa magereza wama Nyota 2 wale nadhanii hakuwapigia salute wala nini kapita mkavuu..[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jamaa walianza kujiongelesha yani hawa Jw wanajiona wao ndo wao kama huyu katupita bila hata kubana mikono acha salute..
Itakua huyo JWTZ hakuelewa somo la salute.Nimeshuhudia mara kadhaa,polisi wakipigiwa salute na JW.Tatizo ni ujinga wa baadhi wa wananchi na kua na mentality mbovu.
 
Nimekuwa nikishuhudia CDF akiitwa mkuu wa majeshi ilihali jeshi la Magereza,Polisi na Uhamiaji yanao wakuu wao.

Sasa ni ipi sababu hasa ya CDF kuitwa mkuu wa majeshi?

Mkuu wa Majeshi ndio Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa Taifa ( national defense council) ; na katika hali ya Vita au dharura command inatoka kwake… au kwenye operesheni za pamoja
 
Wewe utakua polisi!

Military ni jeshi na Force ni kikosi tu!

TISS,PCCB,Uhamiaji na hao Polisi hawafundishwi matumizi ya siraha nzito! Mfano huwezi kuta kifaru kipo kwenye kikosi cha Polisi,PCCB au Uhamiaji!

Rais anapokua anakabidhi madaraka kwa mwingine kwa nini CDF ndiyo hua anasimama na Rais na sio IGP,DG-TISS DG-PCCB,CGI,CGF au CGP??
Hizi ni akili na majibu ya Askari wa Rank and File ndiyo wanajazwa ujinga huu wakiwa training, huwezi kuta Afisa akawa ana malumbano ya kijinga kiasi hiki katika kuwadharau wengine ilihali wote wanafanya makujumu yenye mrengo sawa wa kuhakikisha Tanzania inakuwa salama.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom